Balozi wa Misri huko Yaounde akutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Cameroon kujadili njia za kuboresha uhusiano wa nchi mbili
Jumanne, Julai 07, 2020
Balozi wa Misri huko Yaounde akutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Cameroon kujadili njia za kuboresha uhusiano wa nchi mbili

 

Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri huko Yaounde, "Medhat Kamal El-Meligy", alikutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Cameroon, Lejeune Mbella Mbella, kujadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili za kindugu.

Waziri wa Mambo ya nje wa Cameroon alisisitiza  heshima ya  nchi yake katika uhusiano wa kihistoria unaohusisha nchi hizo mbili, akisifu uongozi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi wakati wa urais wake wa Umoja  wa Afrika, na mwelekeo wa Rais juu ya njia za kukuza bara la Afrika, kupambana na rushwa na kusuluhisha mizozo ya Afrika.

Ukurasa wa Wizara ya Mambo ya nje