Rais Sisi apokea vithibitisho vya mabalozi wapya sita, na apongeza Canada na Somalia kwa siku zao za kitaifa
Alhamisi, Julai 02, 2020
Rais Sisi apokea vithibitisho vya mabalozi wapya sita, na apongeza Canada na Somalia kwa siku zao za kitaifa

 

Balozi Bassam Radi, msemaji wa ofisi ya Rais wa Jamhuri, alisisitiza kwamba Rais Abdel Fattah El-Sisi alipokea, Jumatano 1/7 katika Ikulu ya Al-itehadia, vithibitisho vya mabalozi wapya sita, ambao ni :

Jose Isono Micha Akeng - Balozi wa Jamhuri ya Guinea Ikweta.

Elie Caby - Balozi wa Jamhuri ya Senegal

Meja Jenerali Anselim Shigongo Bahati - Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hisham bin Mohammed Al-Jowder - Balozi wa Ufalme wa Bahrain

Elmars Predix - Balozi wa Jamhuri ya Latvia.

Giorgi Borisenko - Balozi wa Shirikisho la Urusi.

Rais aliwakaribisha mabalozi hao wapya na akawatakia mafanikio katika majukumu yao Cairo, akisisitiza hamu ya Misri ya kuongeza uhusiano  pamoja na  nchi zao katika nyanja zote. 

Katika muktadha mwingine, Rais Abdel Fattah Al-Sisi alituma barua ya pongezi  kwa Bibi : Julie Payet, Gavana Mkuu wa Canada, kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya kitaifa ya Canada. Pia alituma Barua ya pongeza kama hiyo kwa Rais Mohamed Abdullah Mohamed Faramago, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya kuasisiwa Jamhuri.

 

Tovuti rasmi ya Ofisi ya Rais wa Jamhuri, ukurasa wa msemaji Mkuu wa Ofisi ya Rais.  Bawabatu -Al-Ahram