Rwanda yatafuta kuendeleza miradi yake ya miundombinu
Jumatatu, Septemba 07, 2020
Rwanda yatafuta kuendeleza miradi yake ya miundombinu

Gazeti la (The New Times) liliripoti kwamba Baraza la Seneti la Rwanda liliidhinisha -kwa kauli moja- muswada wa kuthibitisha kujiunga Rwanda kwa Taasisi ya Fedha ya Afrika (IFC), na ambayo ni taasisi ya kifedha ya kimataifa ili kuendeleza miradi ya miundombinu barani Afrika, na gazeti hilo lilimnukuu Waziri wa Fedha na Mipango wa Rwanda kwamba "Kwa kujiunga na taasisi hii ya kifedha kama mwanachama, Rwanda itaweza kupata uzoefu katika kupanga miradi mikubwa na itafaidika na mikopo mipya ili kufadhili miradi yake ya miundombinu", na gazeti hilo lilielezea kwamba taasisi hiyo ya kifedha, ambayo inajumuisha nchi 26 wanachama, inafanya kazi kukidhi mahitaji ya dharura ya bara ya miundombinu kupitia kuchangia maendeleo ya sekta za tasnia, nishati na usafirishaji.

 

Gazeti la Rwanda  (The New Times)