Taifa Stars yaelekea uwanjani tayari kuivaa Burundi
Jumatano, Septemba 04, 2019
Taifa Stars yaelekea uwanjani tayari kuivaa Burundi

 Msafara wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' unaondoka hotelini mchana huu kuelekea kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwagasore jijini Bujumbura tayari kwa mchezo wao dhidi ya Burundi leo saa 10 jioni kwa saa za Tanzania.

Mechi hiyo ni ya kwanza ya hatua ya awali ya mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwa 2022 zitakazofanyika Qatar.

Safari hiyo ya kuelekea uwanja wa Intwari imeanzia katika Hoteli ya Belair Residence ambako timu ilifikia.

Takribani magari saba yapo kwenye msafara huo ambapo kati ya hayo, mabasi ni manne likiwemo lile lililobeba wachezaji na magari madogo ya kawaida mawili.

Mabasi mawili yamebeba mashabiki waliosafiri kutoka Tanzania kuja Burundi kuipa sapoti Taifa Stars huku moja likiwa limebeba waandishi wa habari

MwanaSpoti