Waziri wa Umwagiliaji athibitisha azma ya Misri ya kuimarisha ushirikiano na nchi za Bonde la Mto wa Nile
Alhamisi, 21 Septemba 2023
Waziri wa Umwagiliaji athibitisha azma ya Misri ya kuimarisha ushirikiano na nchi za Bonde la Mto wa Nile

Dk. Hani Sweilem, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, akimpokea Jumamosi tarehe 9/16 Mheshimiwa Pal Mai Deng, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Jamhuri ya Sudan Kusini wakati                   wa ziara yake ya kikazi Cairo, ambayo itadumu kwa siku nne.               

 Dk. Sweilem na Bw. Deng waliongoza Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Kiufundi kati ya Misri na Sudan Kusini, kilichofanyika Mjini Cairo Jumamosi asubuhi, Septemba 16, 2023, kwa kuhudhuria wajumbe wa kamati ya pamoja ya kiufundi kutoka pande zote mbili.                            

Dk Swailem alisema kuwa ziara hiyo inakuja katika mfumo wa ziara mbadala ya pande zote kati ya nchi hizo mbili kwa kiwango cha Mawaziri na mafundi ili kujadili maendeleo katika miradi ya pamoja ya maendeleo katika uwanja wa rasilimali za maji, ambayo inakuja mwanzoni ili kuwahudumia raia wa Sudani Kusini.                                                        

 Mheshimiwa, alisisitiza jukumu la Misri la kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi ndugu  za Bonde la Mto Nile, hasa Jamhuri ya Sudan Kusini, jambo ambalo linadhihirika wazi katika utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo inayowanufaisha moja kwa moja wananchi wa Sudan Kusini.