Baraza la Manispaa Mjini laweka mikakati ya kuusafisha mji
Jumatatu, Januari 20, 2020
Baraza la Manispaa Mjini laweka mikakati ya kuusafisha mji

MJI Mkongwe wa Zanzibar ni mji wa kihistoria kama ilivyo miji mingine kama hiyo duniani.


Kiuhalisia mji mkongwe yaani (Stone town) umebeba historia kubwa ya visiwa hivi viwili vya Unguja na Pemba.


Sambamba na hilo lakini pia mji huu ambao umeingizwa katika kumbukumbu ya urithi wa dunia na shirika la sayansi na mipango la umoja wa mataifa (UNESCO) kutokana na mambo muhimu na ya kihistoria yanayopatikana katika mji huo.


Aidha mji mkongwe huo ni kitovu cha utalii visiwani Zanzibar na umekuwa ukiwavutia wageni wengi wanaoingia nchini ili kujifunza historia pamoja na kuangalia haiba na mandhari.


Ndani ya mji huu kunapatikana majengo ya kihistoria ikiwa ni pamoja na kanisa la Mkunazini, jumba la Beit el Ajab, jumba la wananchi (People palace), ngome kongwe nakadhalika.
Sambamba na hilo, lakini pia Mji huo kwa sasa umepambwa na hoteli za kitalii, na maduka mbali mbali yenye bidhaa za tamaduni na asili ya Wazanzibar.


Mandhari na upepo mwanana wa bahari ya hindi ni kitu ambacho pia kinapatikana katika mji huo.


Akizungumza na makala haya, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Said Juma Ahmada, anasema amekusudia kubadilisha mazingira ya mji wa Zanzibar ili uwe wa haiba na kivutio kwa wenyeji na wageni.


Mkurugenzi huyo anasema ili kuutangaza na kuuweka katika hali ya usafi mji mkongwe aliamuru kusitishwa uwekaji wa taka nje katika maeneo hayo sambamba na kuondoa mfumo wa uwekaji wa makontena.

 

Zanzibar Leo