Umoja wa Afrika watangaza kuanza kwa Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika Januari 2021
Jumanne, 8 Desemba 2020
Umoja wa Afrika watangaza kuanza kwa Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika Januari 2021

Balozi Dkt. Namira Najm, mshauri wa kisheria wa Umoja wa Afrika, alisema kuwa matokeo muhimu zaidi ya mkutano wa kilele wa 13 usio wa kwaida wa Umoja wa Afrika huko Afrika Kusini ni kutolewa kwa Azimio la Johannesburg la kuanza biashara kwa mujibu ya makubaliano ya msingi ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika Januari 1, 2021 kwa msingi wa sheria  za asili zilizokubaliwa , na tangazo hili lilitaka  kufanyika vitengo vyote vya Kituo cha Biashara cha Afrika ili kuimarisha kasi ya upatikanaji wa taarifa za biashara na huduma zinazohusiana.

 Najm alisisitiza kuwa hii ni pamoja na kuimarisha uwazi, ufanisi na uadilifu katika soko la biashara ya bidhaa na huduma kwa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, na kwa kufanyika utaratibu wa kielektroniki wa kufuatilia vikwazo visivyo vya forodha na kuvifichua. Tangazo hilo lilipongeza nchi zifuatazo kumi na nane (18) (nchi 7 pamoja na wanachama wa Jumuiya  ya Uchumi na Fedha ya Afrika ya kati  na Jumuiya ya Forodha ya Kusini mwa Afrika) ambazo zimetoa ratiba zao za makubaliano ya kitambulishi  ambazo ni Botswana, Kamerun, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Guinea ya Ikweta, Eswatini, Gabon, Lesotho, Madagaska, Malawi, Mauritius, Namibia, Sao Tome  Na Principe, Ushelisheli na Afrika Kusini, na limezipongeza nchi kumi na mbili ambazo zimetoa huduma  zao za awali kuhusiana na biashara katika huduma, ambazo ni Jamhuri ya visiwa vya Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Mauritius, Namibia, Sao Tome na Principe, Shelisheli, Afrika Kusini na Zambia.

 Uamuzi wa Mawaziri wa Biashara wa Kiafrika uliidhinisha umuhimu wa kukamilisha maswala yote muhimu kuhusu sheria za asili, makubaliano ya kitambulishi na majukumu maalumu kuhusu biashara ya bidhaa na huduma ifikapo Juni 2021, na tangazo hilo liliashiria  kuwa haikuwezekana kukamilisha mazungumzo ya awamu ya pili ifikapo tarehe ya mwisho iliyokubaliwa Desemba 2020 kwa sababu ya kuendelea kwa kuenea  janga la virusi vipya vya corona na tangazo hilo liliruhusu uamuzi wa Mawaziri wa Biashara wa Kiafrika kumaliza mazungumzo kwa hatua ya pili na ya tatu ifikapo Desemba 31, 2021.

Najm aliashiria kwamba azimio hilo lilipongeza nchi wanachama ambazo zilizotia saini makubaliano ya kuanzisha Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika na kuwasilisha fedha zake za kukubali kwa Tume, hivyo idadi ya nchi wanachana imezidi kufikia nchi thelathini na tatu (33), na ksisitiza tena kujitolea kwao kuziba pengo la ufadhili wa miundombinu barani Afrika ndani ya miaka kumi kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Afrika na Mpango wa wafuasi wa Afrika na wadau wengine, na kushirikiana na jumuiya ya kiuchumi  na washiriki.

Balozi huyo aliongeza kuwa azimio hilo lilizitaka taasisi za kifedha za Afrika kufanya ushirikiano wa kweli na  sekretarieti ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika katika kujumuisha rasilimali na kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa nchi wanachama katika kutekeleza makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika na kushughulikia athari mbaya za janga la virusi vya corona.

Kuhusu maamuzi ya  mkutano wa kilele wa   kuanza  biashara katika eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, Najm alisema kuwa mkutano wa kilele huo uliamua kwamba maonesho na ratiba za awali zilizowasilishwa na nchi wanachama zinapaswa kutekelezwa kwa muda mfupi moja kwa moja baada ya makubaliano ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Biashara, ikisubiri saini ya mkutano huo katika kikao chake kijacho cha kawaida, na ratiba inapaswa kuwekwa ratiba maalumu ya wakati kwa upunguzaji wa awali unaoambatana na jedwali la wakati la kila mwaka  linalofuata ratiba ya kila mwaka ili kutoza ada ya sifuri kwa 90% ya vitambulisho pamoja na muda uliowekwa katika hatua na kufuata usawa wa matendo , kwa sharti la  kufuta vitambulisho

ifikapo mwishoni mwa kipindi cha kupunguza taratibu kilichowekwa chini ya njia zinazoakubaliwa, mkutano huo ulihimiza Baraza la Mawaziri, sekretarieti ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika na mamlaka ya forodha kuharakisha utekelezaji wa michakato, taratibu na vyombo vya forodha vinavyohitajika ili kufanyika biashara chini  ya mfumo wa Eneo la Biashara Huria la Bara Januari 1, 2021.

 Balozi alionesha kuwa kubadilishana haya kati ya nchi wachama kutakuwa na sharti juu ya kanuni ya haki sawa kwa upande wa kutosheleza yale yote yanayohitajika kwa uzalishaji na ratiba za kupunguza ushuru wa forodha kulingana na njia zilizokubaliwa, na mkutano huo uliruhusu  kutangaza  hatari za kumaliza mizozo kati ya wawekezaji na nchi zinazohusika na taratibu zinazohusiana na janga la virusi vya Corona kama ifuatavyo na Mawaziri wa biashara Umoja wa Afrika . Na mkutano wa kilele huo ulikaribisha kuanzishwa kwa Baraza la Biashara la Afrika kama sehemu ya mfumo wa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika na kupongeza Ofisi ya Utendaji ya Muda inayoongozwa na Dkt. Amani Asfour

Kwenye mpango wa Azimio la Johannesburg juu ya "Kunyamazisha Bunduki Barani Afrika: Kuunda Mazingira yanayofaa kwa Maendeleo ya Afrika kwenye Mkutano wa kilele 14  usio wa kwaida  Najm alisisitiza kwamba Mkutano huo uliweka wazi kuwa Afrika bado inakabiliwa na changamoto nyingi na ngumu, hasa mapengo ya utawala, ugaidi na itikadi kali ,  utitiri wa wapiganaji wa kigaidi wa kigeni kutoka nje ya Bara, mtiririko haramu wa silaha, ufisadi, mtiririko haramu wa kifedha, uhalifu uliopangwa ukivuka mipaka ya kitaifa, biashara ya dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu, kuzuia raia kufaidika na mapato ya rasilimali asili,uingiliaji wa nje wa kisiasa na kijeshi,  kuzuka kwa magonjwa hatari na janga , mabadiliko ya hali ya hewa, na kasi ndogo ya kuridhiwa  fedha za Umoja wa Afrika, pamoja na mambo mengine Changamoto hizi . zinaendelea kuzuia juhudi za kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya bara.

 Najm alielezea kuwa azimio la mkutano huo limetaka kutekeleza juhudi na kutenga rasilimali zinazohitajika ili kuzuia na kushinda ugaidi na itikadi kali  na vile vile uhalifu uliopangwa wa nje ya mipaka ya kitaifa  katika bara hili na limesisitiza kulazimisha kwake katika swala hili kwa kuongeza  kikosi cha kiafrika  kilichowekwa tayari na rasilimali na vifaa ili  kusaidia juhudi za Afrika za kutokomeza janga la ugaidi, na kuchukua hatua za nguvu , kulingana na  Sheria asili ya Umoja wa Afrika na mkataba wa Baraza la Amani na Usalama, Sera ya Pamoja na mkataba  wa Mataifa wa Ulinzi na Usalama wa Afrika, na pia Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuliepusha bara kutoka tishio la kuingiliwa kisiasa na kijeshi kwa mambo ya ndani ya Afrika, pamoja na zile zinazohusiana na kusaidia vikundi vya kigaidi vyenye silaha na wapiganaji wa kigaidi wa kigeni kutoka nje ya bara.

 Mshauri wa sheria wa Umoja huo ameongeza kuwa mkutano huo wa kilele umesisitiza tena katika Azimio la Johannesburg  kujitolea kwa nguvu juu ya  kuondoa mabaki yote ya ukoloni barani Afrika, uvamizi haramu na kushughulikia shida za wakimbizi, wakimbizi wa ndani, wahamiaji na vikundi vingine vilivyo maskini barani Afrika kwa ujumla na kujitolea kwake kwa kusudi hili, kuondoa sababu za msingi za jambo hili na kuhakikisha ulinzi wao kupitia utekelezaji kamili kwa fedha ya kikanda na kimataifa.

 Balozi aliashiria azimio la mkutano huo katika muktadha wa Ajenda 2063 ya  Umoja wa Afrika  ili kupanua utekelezaji wa ramani kuu ya Umoja wa Afrika  kuhusu hatua za kiutendaji za kunyamazisha bunduki kwa kipindi cha miaka kumi (2021-2030) na kutoa taarifa kila baada ya miaka miwili na uamuzi wake wa kuongeza maadhimisho ya Mwezi wa Msamaha wa Afrika Septemba kila mwaka kwa kipindi cha Miaka kumi  (2021-2030)

 Balozi alisema kwamba moja ya maamuzi muhimu zaidi ya mkutano wa Afrika katika kikao maalumu cha 14 cha kunyamazisha bunduki huko Johannesburg ni uamuzi wa mkutano huo kwamba Baraza la Amani na Usalama, kwa msaada wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Jopo la wataalamu, litakalohakikisha kufuata kwa ukamilifu  Sheria ya msingi  ya Umoja wa Afrika, mkataba wa Baraza la Amani na Usalama na mifumo mingine ya sera husika  wakati wa mizozo inayokuzwa barani ili kuzuia kuongezeka kwake. Na kwa suala hili, Baraza la Amani na Usalama lina jukumu la kufunua na kufichua watendaji ambao wanakanusha mizozo inayoibuka, kama ilivyoainishwa katika ramani kuu ya Umoja wa Afrika juu ya Kunyamazisha Bunduki na kumaliza mchakato wa kuanzisha mfumo wa ushirikiano  Kati ya Baraza la Amani na Usalama na Nchi Wanachama, pamoja na uamuzi wa mkutano huo, Baraza la Amani na Usalama, kwa kushirikiana na vyombo vya kutengeneza sera vya RECs / Utaratibu wa Amani na Usalama wa Kikanda, na kwa mujibu wa kila kesi, inapaswa kuanzisha utaratibu wa uchunguzi wakati wa kuonekana kwa habari juu ya  nchi chanzo,au kupitia habari yoyote  juu ya wale wanaoruhusu  uhamiaji  na utumiaji wa silaha haramu zinazofika Afrika, na uamuzi wa kutumia kikamilifu Mfumo wa Amani na Usalama wa Afrika, Mfumo wa Utawala wa Afrika ,njia zingine za ushirikiano katika kupambana na ugaidi na kuongezeka kwa idadi ya wapiganaji wa kigaidi wa kigeni kutoka nje ya bara , uhalifu uliopangwa usio wa kitaifa , pamoja na Kikosi cha Afrika kilicho tayari , Kituo cha Mafunzo na Utafiti wa Ugaidi na Mfumo wa Ushirikiano wa Polisi (AFRIPOL), huko Algeria,mji mkuu wa Algeria, mchakato wa Nouakchott na Djibouti, na Kamati ya Huduma za Ujasusi na Usalama barani Afrika (SISA)

 

Katika muktadha huu , Tume ya Umoja wa Afrika inalazimishwa kuandaa mkakati kamili wa kupambana na ugaidi barani Afrika ili kuimarisha uratibu na kuimarisha hatua katika kupambana na vikundi vya kigaidi na vya uhalifu, na katika suala hili, mkutano huo uliamua kwamba Tume lazima ichukue hatua za dharura zinazohitajika ili kufanyika Mfuko Maalumu wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi na itikadi kali barani Afrika, na uamuzi wa mkutano huo kufanya juhudi za pamoja kukabili vitisho vinavyosababishwa na uingiliaji wa kigeni katika maswala ya Kiafrika yanayohusiana na amani na usalama, na uwepo wa vituo vya kijeshi vya kigeni katika bara hilo,Mshauri wa sheria wa umoja huo alisisitiza kuwa mkutano huo ulizitaka nchi wanachama zinazokusudia kuanzisha vituo vya jeshi vya kigeni kufanya mashauriano ya awali na Baraza la Amani na Usalama, vikundi vya uchumi wa kikanda / mifumo ya kikanda, nchi jirani na kamesheni  ya Umoja wa Afrika ili kuhakikisha kuwa vituo vya jeshi vya kigeni vinatumikia masilahi na malengo ya Umoja wa Afrika, kulingana na sera  Ulinzi na Usalama wa Pamoja wa Afrika na Mkataba wa Umoja wa Afrika wa kutofanyiwa  uadui.

 Najm aliashiria kuwa uamuzi wa mkutano huo wa kulazimisha Baraza la Amani na Usalama liweke utaratibu wa kufichua nakuweka wazi wahusika wa kweli na taasisi za kigeni zinazoingilia mambo ya ndani ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na vile vile wale wanaodhamini mtiririko wa silaha haramu na wanaonendelea  kutoa msaada wa kijeshi wa siri kwa vikundi vyenye silaha barani ,jambo  linalozuia juhudi za Umoja wa Afrika wa Kuzuia na kumaliza mizozo.

 

 Pana press