Ajenda ya 2063
Alhamisi, Aprili 11, 2019
Ajenda ya 2063

Wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 50 kwa kuanzisha Umoja wa Afrika, Umoja huu ulizindua maono mapya kwa bara la Afrika chini ya kichwa cha "Ajenda ya 2063", ambayo imeweka lengo lake na lengo hili ni "Afrika tunayotaka". Mpango huu uliwasilishwa na wajumbe 54 wa Umoja, kama mwaliko wa kufanya kazi katika jamii zote za Kiafrika ili kujenga bara lenye mafanikio na umoja na ambao ni msingi wa maadili wa mustakbali wa pamoja.

Afrika tunayotaka" inategemea Benki ya Maendeleo ya Afrika, uongozi wa kisiasa na kimkakati, ushirikiano wa kikanda, kutoa nafasi za ajira kwa Waafrika wote, ikiwa ni pamoja na wanawake na vijana, na kutatua migogoro.