"Mahusiano kati ya Misri _ Afrika" Kuanzia 1952 hadi 2014
Jumapili, 3 Machi 2019
"Mahusiano kati ya Misri _ Afrika"  Kuanzia 1952 hadi 2014



Kuanzia 1952 hadi 2014

Kwanza: Mapinduzi ya Julai .. Na kutilia umuhimu Bara la Afrika:

 

 Tangu mapinduzi ya Julai mwaka wa 1952, sera ya Misri imetoa umuhimu mkubwa kwa bara la Afrika kwa miongo miwili, na kwa sababu ya imani ya Misri kwa  utambulisho wake wa Kiafrika, Misri imefanya jitihada nyingi  katika masuala mengi na nyanja ambazo zinaimarisha na zinaonesha umuhimu wa masuala ya Afrika kama ifuatavyo:

1- Misri .. na kuondokana na ukoloni  barani Afrika

Mapinduzi ya Julai yamechukua nafasi inayoongoza  tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1952, kuhusiana na haki ya watu kujitawala, na waliitambua haki hii Sudan ambayo ilipata uhuru wake mwaka wa 1956, Misri imeunga mkono katika vikao vyote vya  harakati za uhuru wa kiafrika katika mapambano yao kwa ajili ya haki ya kujitawala  na uhuru.

 

Na kupitia kipindi kilichoanzia 1952 hadi 1967, Misri ilichangia katika  kuunga mkono uhuru wa nchi 34 za Kiafrika, miongoni mwazo ni nchi tano za Kiarabu - kiafrika, kupitia kuunga mkono harakati za uhuru wa kitaifa katika nchi hizi: kisiasa, kidiplomasia, vyombo vya habari na kijeshi.

 

Katika muktadha huo, sera ya Misri kuelekea Afrika – kupitia wakati huo -  ilikuwa na msingi mkuu, hasa: kutoingilia kati katika masuala ya ndani, kuzuia kutoa msaada kwa pande za migongano, na kutotoa nafasi yeyote ya nje inayolenga  kudhoofisha usalama na utulivu wa bara, na kutoshiriki katika migogoro ya maslahi ya nchi kubwa, na ufumbuzi  wa amani kwa migogoro kupitia Shirika la Umoja wa Afrika.

Mtazamo wa diplomasia wa pamoja ni chombo muhimu zaidi cha hatua za Misri kwa ajili ya kukabiliana na ukoloni barani Afrika, kwani Misri imeunga mkono Kamati ya kuondokana na ukoloni ya Umoja wa Mataifa, na aidha Misri ilishiriki katika mikutano yote ya "watu wa Afrika" kuanzia 1958 hadi 1961, kwa lengo la kuunga mkono kwa umoja kati ya watu wa bara la Afrika, pia  ilianzisha Sekretarieti kuu ya Mkutano nchini Ghana ... pamoja na nafasi ya Misri inayoongoza katika harakati za watu wa "Afro-Asia" tangu mwaka wa 1955.. Mfumo wa kuondokana na mahusiano ya kidiplomasia na baadhi ya nchi za ukoloni ulikuwa moja kati ya zana ambazo Misri ilitumia ili kuunga mkono maswala ya kiafrika.

2- Msaada wa harakati za uhuru wa kitaifa wa kiafrika

Chini ya uongozi wa kiongozi Gamal Abdel Nasser, Misri  ilitilia umuhimu zaidi suala la kuondokana na ukoloni na kutoa msaada kwa harakati za uhuru wa kitaifa wa Kiafrika, kama tafsiri ya vitendo ya vipaumbele vya huduma tatu za usalama wa kitaifa wa Misri: Kiarabu, Afrika na Kiislamu.

 

Sera ya Misri iliunga mkono harakati za uhuru wa kitaifa wa Afrika katika miaka ya sabini kwa njia zote na taratibu zinazowezekana, na mojawapo ya jitihada maarufu zaidi za Misri katika Nyanja hii:

Kusaidia juhudi za uhuru wa nchi hizi : Morocco, Tunisia na Algeria.

Kuzingatia mwaka wa 1960 ni mwaka wa Afrika.

Kuanzisha Kamati ya uratibu inayofuata Shirika la Umoja wa Afrika kwa ajili ya

Ukombozi wa Afrika.

Kuimarisha mahusiano na viongozi wa uhuru wa kitaifa.

Kusaidia mapinduzi ya Libya mwaka wa 1969, na kutoa msaada wa kiutamaduni   na vyombo vya habari kwa wananchi wa Libya.

Kusaidia muungano wa kitaifa wa Somalia ili kudumisha utambulisho wa watu wa Somalia na umoja wa ardhi zake.

Kuunga mkono mapambano ya watu wa Eritrea.

Kuanzisha unganisho la Kiafrika mwaka wa 1955 ili kusaidia harakati za ukombozi.

Misri ilijiunga kama mwanachama mwanzilishi  katika Kamati ya Uratibu inayofuatilia Shirika la Umoja wa Afrika katika mwaka wa 1963 kwa ajili ya ukombozi wa Afrika.       

Kuunga mkono mapambano ya harakati ya " Mao" nchini Kenya,  kupitia kampeni ya vyombo vya habari na ya kideplomasia  iliyozingatia dhidi ya ukoloni wa Kiingereza nchini Kenya, na Misri ilitoa idhaa ya redio kwa jina la "Sauti ya Afrika" ili kusaidia watu wa Kenya katika mapambano yao kwa ajili ya ukombozi wa nchi yao.

 

Kuchangia katika kukomesha ukatili wa jeshi la Chombe dhidi ya Uganda.

Kufungua ofisi ya Umoja wa Kidemokrasia wa kitaifa kwa ajili ya Msumbiji mjini Kairo.

Msaada wa kifedha kwa harakati ya ukombozi nchini Kongo.

Kusaidia mapambano yenye silaha ya harakati ya Uhuru wa Watu wa Angola.

Ilisaidia Burundi kwa silaha ndogo wakati wa mapambano yenye silaha kwa ajili ya kupata uhuru.

Kutoa msaada kwa mapambano ya watu wa nchi za: Zimbabwe, Afrika ya Kati, Kameruni na Rwanda.

        (MPLA)       

Mwaka wa 1965, ofisi ya kwanza ya kikanda kwa Chama cha Harakati cha Watu kwa ajili ya Uhuru wa Angola  ilifunguliwa mjini Kairo kwa uongozi wa Mheshimiwa / Paulo George Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, na hayo kwa ajili ya kuunga mkono harakati za ukombozi wa Angola dhidi ya ukoloni wa Ureno.

3- Uanzishaji wa Shirika la Umoja wa Afrika

Misri ilijaribu kuanzisha na kujenga muungano wa kiafrika wenye harakati katika Nyanja mbalimbali, kwa ajili ya usalama na utulivu wa bara,Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza zinazochangia katika kuanzishwa Shirika la Umoja wa Afrika mwaka wa 1963 kabla ya kuwa Umoja wa Afrika, na Misri ilichukua urais wa Shirika la Umoja wa Afrika katika  miaka ya 1964, 1989 na 1993.

Misri ilishiriki katika mikutano ya nchi za Kiafrika ambazo zilikuwa kabla ya kuanzishwa kwa Shirika tarehe Mei 1963, na miongoni mwake ni Mkutano wa kwanza wa Nchi za Afrika zilizopata uhuru wao nchini Ghana mwaka wa 1958, ambao ulilazimisha nchi za Kiafrika zilizopata uhuru wao kwa kushiriki moja kwa moja katika ukombozi wa bara la Afrika.

Rais Abdul Nasser alisisitiza kwa nguvu juu ya  wazo la mshikamano wa Afrika, kama kanuni na wajibu, kwa kuzingatia kuwa ni kiungo wa karibu kati ya watu wa Afrika na kati ya maslahi yao ya pamoja, na katika hotuba yake katika Mkutano wa kilele cha kwanza cha Shirika la Umoja wa Afrika, ambacho kilifanyika mjini Addis Ababa Mei 24, mwaka wa 1963, "Jumla ya kanuni za sera ya Misri ya Kiafrika", alisema kwamba "migawanyiko yote ya jadi ambayo ukoloni ilijaribu kuiweka katika bara na kuigawanya Sahara ya kaskazini na Sahara ya kusini, kwa Afrika nyeusi na nyeupe na kahawia, Mashariki na Magharibikwa nchi za Afrika zinazozungumza Kifaransa na nyingine zinazozungumza Kiingereza na zote zilianguka na zilipoteza ukweli wa kiafrika wa awali, na haijabaki barani Afrika isipokuwa lugha moja ambayo ni lugha ya hatima ya pamoja bila kujali njia tofauti za kujieleza. "

 

Pili: Miaka ya sabini .. na kuamsha utaratibu wa mahusiano ya Kiarabu - Kiafrika:

Wakati wa miaka sabini, hasa wakati wa vita vya Oktoba 1973, ilikuwa ni hatua maalum katika historia ya mahusiano ya Misri na Afrika, na mshikamano wa Kiarabu -Kiafrika ulikuwa dhahiri, wakati nchi za Kiafrika zilisimama pamoja na Misri katika vita vyake ili kupata uhuru kwa ardhi yake, na nchi zote za Kiafrika wakati huo zilitangaza kukata mahusiano wao na Israeli, isipokuwa nchi tatu tu, na  nchi za Afrika  Kaskazini na Sudan zilikuwa na jukumu la kutoa msaada wa kifedha na kijeshi wakati wa vita.

Wakati wa "miaka ya sabini"  ulishuhudia mwanzo wa hatua mpya katika sera ya Misri-Afrika ; wakati wa kuanzishwa mfumo wa mahusiano ya Kiarabu na Afrika, na moja ya sifa muhimu zaidi ilikuwa mawasiliano na mashauriano kati ya Nchi za Kiarabu na Shirika la Umoja wa Afrika.

Kwa upande mwingine, kipindi hicho kilishuhudia kuanzishwa kwa taasisi za kifedha kusaidia ushirikiano wa Kiarabu na Afrika nazo ni: Mfuko wa Kiarabu wa Usaidizi wa Ufundi kwa Nchi za Kiarabu za Kiafrika, Mfuko wa Kiarabu wa Mikopo barani Afrika na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.

Jitihada hizi zilifanya Misri kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kilele cha kwanza cha Kiarabu - kiafrika huko Kairo mwaka wa 1977, ambacho kilitoa nyaraka nne kuu  zinazothibitisha udhibiti wa misingi ya mahusiano ya Kiarabu -  Kiafrika. Na nyaraka hizi ni:

Azimio la Kisiasa: lililoelezea msingi wa kisheria na kisiasa kwa ushirikiano wa Kiarabu na Kiafrika.

Mpango wa ushirikiano wa Kiarabu na Kiafrika: na jambo muhimu zaidi lililotajwa hapa ni kujitoa kwa nchi za Kiarabu na za Kiafrika kuendeleza mahusiano yao ya pande mbili yenye malengo kadhaa.

Azimio la Ushirikiano wa Kiuchumi na Kifedha la Kiarabu - Kiafrika.

Mashirika na taasisi zinazohusika na uwezekazo wa utekelezaji wa Mpango wa Kazi kwa ushirikiano wa Kiarabu na Kiafrika.
Na Misri imekuwa na nia ya kushiriki kwa nafasi muhimu katika Mikutano ya  vilele vyote  vya Kiarabu na Kiafrika, kuanzia na Mutano wa Kilele cha Kairo, kisha Mkutano wa Kilele cha Sert  nchini Libya mwaka wa  2010, na Mkutano wa Kilele cha Kuwait mwaka wa  2013, na hatimaye Mkutano wa Kilele cha Malabo mwaka wa 2016.

Tatu: Miaka ya Sabini na Themanini.. na kuendeleza mifumo ya maendeleo ya Misri-Afrika

 

Miaka ya Sabini na Themanini yalianzishwa yanayoweza kutajwa kama msaada wa Misri kwa juhudi za maendeleo barani Afrika, na Sera ya Nje ya Misri huko Afrika na ilishughulikia maendeleo na kujenga nchi za Afrika, na Mfuko wa Misri wa Ushirikiano wa Ufundi na Afrika ilianzisha maoni ya Misri kwa ajili ya maendeleo katika bara la Afrika ... na Misri haijasahau Suala la madeni ya Afrika, zaidi ya  utekelezaji wa Mkataba unaoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Kiafrika mwaka wa  1991 na kuidhinishwa mwaka wa 1994 ... Mipango mingi pia imeanzishwa katika mwelekeo huu, ikiwa ni pamoja na:

1- "Mfuko Kimisri kwa Ushirikiano wa Kiufundi pamoja na Afrika"

Misri ilianzisha Mfuko tarehe Desemba 16, 1980, na Mfuko ulianza shughuli yake mwaka 1981, kwa lengo la kusaidia nchi za Kiafrika kufikia maendeleo endelevu kupitia malengo yafuatayo:

  • Kutoa msaada wa kiufundi kwa nchi za Afrika kwa njia ya kupeleka wataalamu wa Misri.
  • Utoaji wa masomo na mafunzo ya kulipwa kwa watu wa bara  huwezesha kutumia  rasilimali katika sekta mbalimbali.
  • Kuchangia katika miradi ya maendeleo katika nchi za Afrika.
  • Kutoa misaada kwa nchi za Afrika zilizoathirika na majanga au vita.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1980 mpaka kubadilishwa kwake na Shirika la Misri la Ushirikiano kwa Maendeleo mwaka 2013, Mfuko huo umetuma wataalamu 8,500 kwa nchi za Kiafrika katika nyanja mbalimbali, Pia uliwafundisha maafisa 10,000 wa Kiafrika huko Misri, pamoja na kutoa misaada ya kifedha na usaidizi wa kibinadamu Hasa katika kukabiliana na majanga ya mazingira pamoja na kupelekwa kwa misaada kadhaa ya matibabu kwa nchi za Kiafrika.

- Misri na mwisho wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini

Mwanzoni mwa miaka ya sitini, Kairo ilipokea ujumbe wa wawakilishi wa harakati saba za uhuru kutoka Afrika Kusini ili kupata msaada wa Misri kwa ajili ya mapambano yao nchini Afrika Kusini dhidi ya mazoea ya ubaguzi kwa serikali ya wachache weupe dhidi ya wengi weusi, na ziara hii ilikuwa mwanzo wa msaada wa serikali ya Misri kwa harakati za ukombozi wa Afrika Kusini, ambapo   Misri ilikubali mahitaji ya halali ya watu wengi weusi katika uanzishwaji hali ya kidemokrasia nchini Afrika Kusini, na Misri na Afrika Kusini zinahusishwa na historia ndefu ya ushirikiano na Chama cha Kongamano la Kitaifa ( NCP) wakati wa mapambano yake  dhidi ya serikali ya zamani ya ubaguzi.

Kupitia  miaka ya sabini, Misri iliwasilisha maazimio kadhaa ya rasimu ndani ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya dhuluma ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, hususan mwaka wa 1965 wakati Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilikubali azimio la Misri pamoja na nchi 44 na lilitambua  kwamba hali nchini Afrika Kusini ni hatari kwa amani na usalama wa kimataifa.

 

Misri ilishiriki tarehe  Mei 1992 kama mwangalizi katika majadiliano ya Codexa, ambayo ni majadiliano kwa ajili ya Afrika Kusini ya kidemokrasia, bila ya ubaguzi kati ya mamlaka ya Pretoria na majeshi ya kisiasa ya Afrika. Wakati wa mwisho wa ubaguzi wa rangi, Rais wa zamani Nelson Mandela na baraza la mawaziri wake  walikuwa na heshima maalum kwa Misri kuelekea nchi yake, na Misri ilikuwa nchi ya kwanza iliyotembelewa na Mandela baada ya kuchukua uingozi wa nchi mwaka 1994, na alitangaza haja ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Afrika Kusini na Misri katika nyanja zote.

3– Misri.. na kusaidia uhuru wa Namibia:

Misri imechangia kupitia Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) kwa uhuru wa Namibia mwaka 1990, na Misri ilikuwa nchi za kwanza iliyotambua SWAPO kama mwakilishi pekee wa haki wa watu wa Namibia, na iliruhusu ufunguzi ofisi ya SWAPO huko Kairo.

Uhuru wa Namibia ulitokea wakati ule ule wa urais wa Misri kwa Shirika la Umoja wa Afrika, (Julai 1989 - Julai 1990) kwani Kairo ilikuwa na hamu ya kukomesha sheria zote za ubaguzi wa rangi, na kutolewa kwa wafungwa wote wa kisiasa kutoka kwa watu wa Namibia.

 

Na zaidi ya hapo juu, Misri ilichangia kutolewa kwa kiongozi wa Afrika Nelson Mandela katika mwaka wa 1990.. Na Kairo pia imechangia ufumbuzi wa mgogoro uliojitokeza kati ya Mauritania na Senegal katika mwaka 1989 kupitia kusainiwa  makubaliano ya amani kati ya nchi hizo mbili kwa msaada wa Misri mwaka 1992.. Na  katika kipindi hiki Misri ilifanya jitihada ili kukomesha migogoro nchini Angola na Msumbiji, na imefanya  zaidi ya mkutano mmoja kwa ajili ya upatanisho nchini Somalia. Miaka ya 1994 na 1997.

  1. Misri na Urais wa Umoja wa Afrika kwa vipindi viwili:

Nchi za Afrika ziliichagua Misri kama Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Afrika kwa vipindi viwili : (1989-1990) na (1993-1994) na wakati wa urais wa Misri kwa Shirika, mfumo wa kwanza wa kuzuia na usimamizi wa migogoro mwaka wa 1993 ili kukabiliana kwa njia ya utaratibu na ufanisi pamoja na migogoro inayotokea kati ya nchi za bara na kuitatua kwake kwa njia za amani.

Misri  ilitilia umuhimu zaidi kwa suala la madeni ya bara la Afrika ili kuhudumia mchakato wa maendeleo; kwani Misri imekaribisha Mkutano mdogo wa Kilele cha Kiafrika  mwaka 1987,  ili kujadili hali za kiuchumi katika bara; Pia ilizindua mazungumzo pamoja na nchi saba za kiviwanda katika mwaka wa 1989 kuhusu suala la madeni, Misri pia imekaribisha Kongamano la Kimataifa kuhusu Madeni ya Afrika Mnamo Agosti 1989, ili kujadili suluhisho zinazofaa zaidi katika suala hili. Pia imechangia katika Mpango wa Urejesho wa Uchumi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa katika kipindi cha ( 1986-1990).

Uanzishaji wa Mfumo wa kukomesha migogoro ya Afrika ni mojawapo ya mipango muhimu zaidi ya Misri tangu kuanzishwa kwa Shirika na ambao Misri ilitaka kuanzishwa kwake wakati wa mkutano wa Kilele cha 28 na juhudi zake ziliendelea mpaka mfumo huo ulianzishwa tarehe 7 Juni 1993. Misri pia ilipendekeza wakati wa Mkutano wa Kilele cha 30  cha Afrika  (Tunisia - Juni 1994) uanzishwaji wa kituo cha Kimisri ili kulinda amani na kutoa mafunzo kwa maafisa wa Kiafrika na  kilianzishwa mwaka wa 1995.

Na kwa ngazi ya kibinadamu, wakati wa urais wake wa 25 kwa Shirikisho la Umoja wa Afrika (OAU), Misri iliwasilisha maoni ya kimkakati kwa ajili ya kutatua suala la wakimbizi kwa kuzingatia mihimili mitatu: msaada wa nchi mwenyeji kwa wakimbizi  - msaada wa nchi asili ya wakimbizi  - msaada kwa haki za mwanadamu mwafrika.

Kwa upande wa usalama, Mnamo 1990, Misri ilizindua mpango wa ukuoaji Afrika na Mashariki ya Kati kutoka silaha za nyuklia na silaha za uharibifu mkubwa, na Mkutano wa Kilele cha 31 cha Afrika mwaka wa 1995 ulifikiri usalama wa Mashariki ya Kati ni sehemu muhimu ya bara la Afrika.

Nne: Misri.. na Umoja wa Afrika

  1. Kutoka kuanzishwa hadi mageuzi ya miundo

Katika miaka ya 1990, viongozi wa Kiafrika walijadili haja ya kurekebisha miundo ya Shirika la Umoja wa Afrika ili kutafakari changamoto za dunia inayobadilika. Na katika mwaka wa 1999, Maraisi wa Nchi na Serikali katika Shirika la Umoja wa Afrika walitoa " Azimio la Sirte" linalotoa wito kwa kuanzishwa Umoja mpya wa Afrika.

Maoni ya Umoja, ambayo Misri ilichangia kuanzishwa kwake, ilikuwa kuanzisha taasisi inayoweza kuharakisha mchakato wa ukamilifu katika Afrika, na pia kusaidia na kuwezesha Mataifa ya Afrika katika uchumi wa dunia, na kushughulikia na matatizo mengi ya kijamii, ya kiuchumi na ya kisiasa yanayokabili bara hili.

Na Misri imechangia katika  kuanzishwa kwa muundo wa Umoja wa Afrika      

kwa kuwasilisha ombi la marekebisho mengine kwenye waraka wa rasimu, hususan: marekebisho ya Ibara ya 4 (h), na kupunguza haki ya Umoja kuingilia kati katika masuala ya Nchi za Mataifa ya Wajumbe  katika kesi tatu maalum: mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa vita. 

Misri ina asilimia 12 ya jumla ya mchango wa Nchi za Mataifa ya Wajumbe  katika bajeti ya Umoja wa Afrika, kwa kuizingatia  mojawapo ya nchi tano ambazo zina mchango mkubwa zaidi katika bajeti ya Umoja wa Afrika (Angola, Afrika Kusini, Algeria na Nigeria), na  Misri ilikaribisha kikao cha 11 cha kawaida cha Mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Sharm El-Sheikh Juni/ Julai 2008.

Misri imeidhinisha mikataba 21 chini ya Umoja wa Afrika, na imetia saini juu ya makubaliano saba ya Umoja wa Afrika bila ya kuidhinishwa.

2 - Mipango maarufu zaidi ya Misri ndani ya Umoja wa Afrika :

  • Kutia saini juu ya mkataba wa uelewa kati ya Mfuko wa Misri wa Ushirikiano wa Kiufundi na Afrika (Shirikisho la Misri la Ushirikiano kwa Maendeleo – sasa hivi) na Tume ya Umoja wa Afrika, kwa lengo la kujenga uwezo wa wafanyakazi wa Tume kupitia kupeleka wataalamu wa Misri kwa ajili ya kutoa mafunzo katika Makao Makuu ya kamishna.

 

  • Misri imetoa mpango kwa kuanzisha Kituo cha Umoja wa Afrika cha Ujenzi mpya na Maendeleo ya Baada ya kipindi cha Migogoro, kwa imani kwamba ni muhimu kujaza pengo katika mfumo wa amani na mfumo wa usalama wa Afrika kwa kuanzisha mfumo wa kibara ili kushughulikia na hali za nchi zinazojitokeza kutokana na  migogoro na kuimarisha amani ndani nchi hizo. Na inayotarajiwa kwamba utekelezaji wa kituo hicho utaanza katika mwaka huu 2019.

 

  • Mnamo 2005, Misri ilipendekeza kuanzishwa kwa Kituo cha Kiafrika cha Magonjwa magumu na ya kuambukiza na UKIMWI kilichofanyika mjini Kairo. Pia ilionesha nia yake ya kuhamisha utaalamu wake katika Nyanja ya viwanda vya dawa, Utengenezaji wa chanjo kwa nchi za bara na kuhamisha utaalamu wake katika kuondokana na polio.
  • Misri imetaka kuanzishwa Baraza la Afrika la Mawaziri wa Umeme, linafuatia Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Afrika, kwa sababu ya umuhimu wa sekta ya umeme na nishati kama injini ya kukua kwa sekta nyingine za uchumi wa kitaifa.. Mpango huo uliendeleza hadi ikajulikana kama ( Kongamano la Kiafrika la Pili kwa Mitandao)

 

  • Misri ilishiriki kwa njia ya kikamilifu katika Azimio la Roma Novemba 2014 katika mpango wa Umoja wa Ulaya na Pembe ya Kiafrika kuhusu njia za Uhamiaji ili kutoa msaada kwa nchi za eneo la Pembe ya Kiafrika katika Kupambana na Usafirishaji wa Wanadamu na Utorokaji wa Wahamiaji.

 

  • Misri ilishiriki katika "Kilele cha Valletta kuhusu Uhamiaji" tarehe (Novemba 2015), kwani ilitetea mtazamo wa Kiafrika kwa kuzingatia Mwenyekiti wa mipango ya Umoja wa Afrika­ ­- Pembe ya Kiafrika na Umoja wa Ulaya – Pembe ya Kiafrika,  kwa utaratibu pamoja na Tume ya Umoja wa Mataifa.

 

  • Wakati wa Mkutano wa Kilele cha Umoja wa Afrika kilichofanyika mjini Addis Ababa mnamo Januari 2015, Misri ilitoa pendekezo la kuanzisha kitengo cha upatanishi na kuzuia migogoro katika muundo wa Tume kwa lengo la kuimarisha uwezo wa upatanishi wa Kiafrika, na Mkutano wa Kilele uilikubali pendekezo la Misri na uratibu unaendelea pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika kuhusu pendekezo hilo.

Taasisi za Kiafrika nchini Misri  :

  • Ofisi ya Umoja wa Afrika kwa Nchi za Kiarabu mjini Kairo.
  • Umoja wa Vyomba vya Kiafrika kwa Biashara, Viwanda, Kilimo na kazi za Umoja wa Afrika
  • Shirika la Uwekezaji wa Kikanda kwa KOMESA
  • Umoja wa Vyomba vya Kiafrika kwa Biashara, Viwanda, Kilimo na kazi
  • Benki ya kuuza nje na kuagiza ya Kiafrika.
  • Ofisi ya nchi kwa Benki ya Maendeleo ya Kiafrika na Mfuko wa Maendeleo ya Kiafrika.
  • Umoja wa Afrika kwa Makampuni ya Makandarasi ya Ujenzi.
  • Kampuni ya Ukarabati wa Afrika.
  • Ofisi ya Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi barani Afrika.
  • Shirikisho la mshikamano wa Watu wa Afrika na Asia
  • Shirikisho la Soka la Afrika.

Na kupitia kuunga mkono  kwa mahusiano ya Misri na makundi ya kikanda ya kibara, Misri ina mahusiano tofauti na makundi mengi ndani ya bara, kama Kundi la Pwani na Jangwa, COMESA, ECOWAS, SIMAC na IAC.