Misri.. na muundo wa amani na usalama barani Afrika
Jumanne, Machi 19, 2019
Misri.. na muundo wa amani na usalama barani Afrika

 

Sera ya Misri imetilia umuhimu zaidi suala la amani na usalama barani Afrika, katika ngazi nyingi, kama vile : mipango rasmi, mifumo dhibiti na michango ya kimataifa.

 

Kwanza: mchango wa Misri katika shughuli za kulinda amani barani Afrika                     

Misri imeshiriki katika ujumbe  wa kulinda amani mara 8 miongoni mwa  9   katika ngazi ya  bara la  Afrika katika nchi za Côte d'Ivoire, Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sahara ya Magharibi, Liberia, Sudan Kusini, Darfur na Mali, kama ifuatavyo:                                                                                                                             

 

  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ili kuandaa kura ya maoni Sahara ya Magharibi

MINURSO))

  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kufikia utulivu. (MINUSCA)
  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali ili kufikia utulivu. (MINUSMA)
  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire ili kulinda amani. (UNOCI)
  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia ili kulinda amani. (UNMIL)
  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kufikia utulivu.
  • (MONUSCO)Ujumbe wa pande mbili za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur (UNAMID)
  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Sudan Kusini ili kulinda amani. (UNMISS)                                                     

Na kulingana na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huko Kairo, Misri inachangia kwa  wamisri elfu tatu wanaofanya kazi  chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa katika ujumbe kadhaa ulimwenguni kote, na hilo linafanya Misri kuwa mshiriki wa saba mkubwa zaidi  kwa wafanyakazi wa kawaida katika shughuli za kimataifa za kulinda amani, na nchi ya kiarabu ya kwanza  katika nyanja hii.                  

Pili: Uanachama wa Misri katika Baraza la Amani na Usalama katika Umoja wa Afrika                                                                                                                                             

 

Januari 28, 2016, Misri ilishinda kwa  mara ya kwanza  uanachama wa Baraza la Amani na Usalama katika Umoja wa Afrika kwa muda wa  miaka 3, Kwa msaada wa Nchi 47 za Umoja wa Afrika, wakati wa mkutano wa Baraza la utekelezaji wa waziri la Umoja wa Kiafrika.

Na uanachama wa Misri katika Baraza la Amani na Usalama ulikuja kama  juhudi zake ili  kushiriki katika kusaidia na kuimarisha muundo wa amani na usalama barani  Afrika, hasa kutokana na tishio kubwa la makundi ya kigaidi na vikundi vyenye silaha.

Na uanachama wa Misri katika Baraza la Amani na Usalama katika Umoja wa Kiafrika ulikuja sambamba na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na jambo hilo  lilingana na jukumu la Misri katika kuratibu kati ya ajenda mbili za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika uwanja wa kulinda amani na usalama wa kimataifa na kuonesha mtazamo wa Afrika .                                                                                                 

Diplomasia ya Misri imechangia kupitia Mabaraza mawili katika kutoa maazimio yanayoakisi  maono ya Misri kuhusu kukabiliana na ugaidi, kama vile kupambana na itikadi kali na kuzuia kuwasili silaha kwa magaidi, na  Misri pia ilifanikiwa kufanya mkutano wa kwanza wa mashauriano kati ya Baraza la Usalama pamoja na Umoja wa nchi za Kiarabu kwenye makao Makuu yaUmoja wanchi za Kiarabu huko Kairo katika  mwezi wa Mei 2016.                                                                                                                   

 

Tatu: Mifumo ya Misri ili kuunga mkono amani na usalama barani Afrika

1- Kituo cha kimataifa cha Kairo ili kutatua  migogoro, kulinda na kujenga amani.                                                                                                                    

Mkakati wa "Kituo cha kimataifa cha Kairo ili kutatua  migogoro, kulinda na kujenga amani" unasisitiza juu ya maono ya " Afrika ni bara lenye amani, usalama na mafanikio"  na kituo hicho kinalenga kuunga mkono michakato na taasisi za kisiasa baada ya kipindi cha migogoro, kufundisha vikosi vya kulinda  amani vya kiafrika na wajenzi wa amani, na kuimarisha uwezo wa mashirika ya kitaifa, kikanda na kibara yanayofanya kazi katika uwanja wa amani na usalama.                                               

Shughuli za mafunzo ya Kituo hujadili  mada kama vile :  kushughulikia migogoro, kupambana na biashara ya binadamu, kupambana na kuingia silaha ndogo na silaha hafifu nchini na udhibiti wa mipaka kwa namna kamilifu, pamoja na kozi zinazofanywa na  Kituo katika uwanja wa  habari na migogoro, kwa njia ambayo waandishi wa habari wamisri na waafrika wamefundishwa ujuzi wa ufikishaji wa kitaalamu kwenye migogoro.                                                                                    

2- Kituo cha kikanda ili kupambana na ugaidi kwa nchi za Jumuiya ya Pwani na Sahara.                                                                                                                    

Juni 24, 2018, Misri ilitangaza kukamilisha  uanzishaji wa  Kituo cha kikanda ili kupambana na ugaidi kwa nchi za Jumuiya ya Pwani na Sahara  kupitia kuimarisha ushirikiano wa kuendelea ili kupambana na ugaidi na kusaidia juhudi za usalama na utulivu katika bara.                                                                                                   

Desemba 8, 2018, Kituo kilizindua shughuli zake za kwanza kwa kuandaa harakati za mafunzo ya pamoja katika uwanja wa kupambana na ugaidi kati ya vipengele vya nchi za Jumuiya ya Pwani na Sahara, katika eneo la Kijeshi la Mohammad Najib, pamoja na ushiriki wa wanachama wa vikosi maalum vya Misri , Sudan, Nigeria na Burkina Faso katika kundi la kwanza, kwa mafunzo katika kukabiliana na vitisho mbalimbali vya kigaidi kama vikundi vyenye silaha na kukomboa mateka.               

"Nguvu ya Afrika tarari"                                                                                        - 3

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2005, Misri inashiriki  katika  (ASF), pamoja na ushiriki  katika kutoa mafunzo ya " II AFRICA AMANI", na vikundi vya kazi, na mazoezi ya kijeshi yanayohusiana nayo, pamoja na ushiriki katika uwezo wa Afrika ili kujibu kwa haraka katika (ACIRC). Kwa kuizingatia ni nguvu iliyopangwa tayari kuingilia kwa haraka, vitengo vyake vimewekwa katika Mataifa ya yanayochangia na kuyaeneza katika maeneo ya migogoro kulingana na uamuzi unaofanywa na Baraza la Amani na Usalama wa Kiafrika.                                                                               

                                                                        

Nne: Uanachama wa Misri katika Baraza la Usalama.. na msaada wa amani na usalama barani Afrika                                                                                               

 

Misri imepewa uanachama  wa Baraza la Usalama kutoka 2016 hadi 2017,waka huohuo ilipewa uanachama wake  katika Baraza la Amani na Usalama wa Afrika, na jambo hilo  lilikuwa fursa ya kudhihirisha uwazi wa upeo wa Afrika katika sera ya kigeni ya Misri na jukumu lake kubwa katika kukabiliana na masuala mbalimbali yenye ugumu zaidi  na kufanya kazi ili kutatua  migogoro mbalimbali ndani ya bara.

Na ifuatayo  ni baadhi ya mifano ya jitihada za Misri katika Baraza la Usalama la Kimataifa  - wakati wa uanachama wake usio wa kudumu - katika kuunga mkono  masuala ya bara la Afrika…..                                                                                     

Kusaidia jitihada za kudumisha amani na usalama katika viwango viwili  vya kimataifa na kikanda, na kutilia umuhimu  ufahamu wa sera na dhana zinazohusiana na kulinda  amani katika kiwango cha  Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, na kuchangia mchakato wa ukaguzi maalumu  wa kulinda na kujenga amani.                                                                                                

Misri inasisitiza - Katika vikao na matukio yote ya kikanda na kimataifa – juu ya   umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ili kuzuia migogoro na kuitatua ,  na nia ya Misri kujenga uwezo wa nchi za Afrika katika nyanja za amani na usalama.                                                                 

Ujumbe wa Misri kwa Umoja wa Mataifa huko New York ulifanikiwa kutoa azimio tarehe 25/5/2017  kutoka  Baraza la Usalama kukubali aghalabu ya nchi wanachama wa Baraza kwa ajili ya  kukaribisha mfumo wa kimataifa wa kupambana na hotuba za kigaidi na kuutekeleza, mfumo ambao Misri imefanikiwa kupitishwa kwa uwazi kama waraka rasmi  kutokana na nyaraka za Baraza la Usalama, na azimio lilitolewa chini ya Nambari 2354.                                                                                                      

Tano: Hotuba ya kisiasa ya kimisri katika Umoja wa Mataifa .. na masuala ya Afrika                                                                                                                       

Masuala ya bara la Afrika, hususan masuala ya amani na usalama, yamedhihirishwa  sana katika hotuba ya kisiasa ya kimisri  mbele ya Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha miaka iliyopita, na hilo ni jambo  ambalo lilitafsiriwa katika hotuba za Rais Abdelfattah Al-Sisi mbele ya shirikisho hilo, na masuala yaliyojadiliwa yalikuwa: maendeleo katika Afrika, ugaidi katika Afrika, Mgogoro wa Libya, Suala la mabadiliko ya hali ya hewa.. nk.                                                        

1- Hotuba ya Rais, Mheshimiwa Abdelfattah Sisi

 Mbele ya Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa - tarehe (24/9/2014)

"Kwa kushirikiana na nchi jirani ya Libya, Misri tayari imetoa  mpango ambao huweka hatua maalumu na upeo wa wazi ili kukomesha taabu ya nchi hii ndogo, ambayo inaweza kujengwa ili kufikia suluhisho la kisiasa linalounga mkono taasisi za  Libya zilizochaguliwa na zinaruhusu kufikia ufumbuzi wa kina wa kisiasa, na inahakikisha kukomesha mapigano na kulinda  umoja wa ardhi ya Libya na ili kulitekeleza hili, ni lazima kusimamishwa kuingiza silaha nchini Libya  kwa ufanisi, na  kutoshughulikia kwa ulaini kwa  vikundi venye itikadi kali na ambavyo vinabeba silaha, na hutumia vurugu, na wala havitambui mchakato wa demokrasia"                .

 

"Natoa wito kwenye jukwaa hili kwa nchi zote za kimataifa ili kujiunga na kulingana na ubinadamu wetu wa pamoja  kwa ajili ya  kukabiliana na janga la Ebola , ambalo linakabili idadi  kadhaa za nchi za Magharibi mwa Afrika. Kupambana na ugonjwa huu ni jukumu la pamoja ili kupunguza mateso ya wale ambao hawajiwezi, pamoja na kutoa ulinzi kwa ulimwengu wetu ambao umbali wake unapungua kutokana na hali ya zama na ukubwa wa mawasiliano."                                                                           

 

2- Hotuba ya Rais, Mheshimiwa Abdelfattah Al-Sisi

Mbele ya kikao cha 70 cha Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa, Septemba 2015

Hamu kubwa ya Misri juu ya  siku zijazo za Libya ,amani na utulivu wake .. ilikuwa ndiyo  sababu yake kwanza ili kusaidia juhudi za Umoja wa Mataifa ili kufikia suluhishi la kisiasa kwa mgogoro Libya .. Msaada huu umekuwa na nafasi wazi katika kufikia mkataba huo, "Skhirat", ambayo inapaswa kuwa hatua muhimu sana .. Ili kufikia baada yake kwa  kuunganisha jitihada za jumuiya ya kimataifa na kusimama kwake  nyuma ya utashi wa washiriki waliosaini mkataba kwa ajili ya ujenzi mpya kwa  nchi ya Libya…                                                                                                

3- Hotuba ya Rais, Mheshimiwa Abdelfattah Sisi Hotuba

mbele ya Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa (kwa kipindi cha 71) Septemba 2016

Mwaka jana tulifikia makubaliano kulingana na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa. Na kama mimi ni mratibu wa kundi la maraisi wa Afrika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa,  ningependa kuthibitisha ahadi ya Afrika kwa kukubaliana na  mabadiliko ya hali ya hewa kwa mujibu wa uwezo wake,  na matarajio yake ili kuanzisha taratibu za utekelezaji wa Mkataba wa Uhamisho wa Teknolojia na Fedha Endelevu, na  kwa hiyo Misri imeanzisha njia yake mwenyewe  ya Mpangilio wa Nishati Mbadala na imeutoa  kupitia uwakilishi wake wa Tume ya viongozi wa Afrika ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, na ili kutekeleza maazimio  ya Umoja wa Afrika yanayohusiana. Na Misri inasisitiza juu ya  umuhimu wa mpango huo  ili kutoa msaada kwa Afrika.                                                          

Misri ilijitahidi kuunga mkono kwa muundo wa amani na usalama  wa Afrika,  hasa utekelezaji wa nguvu  tayari wa Afrika. Misri imeongeza ushiriki wake katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa ili kulinda amani  katika bara,kwani  imepata tena nafasi yake kati ya Mataifa 10 ya juu yanayochangia katika ujumbe hizi. Na Misri inatoa wito kwa kupata mtazamo kamili katika kupambana na ugaidi, kwa njia ambayo sio tu kwa mwelekeo wa usalama, lakini ni pamoja na upande wa akili. Kwa hivyo, Misri itakaribisha  Kituo cha Kupambana na Ugaidi  kwa jumuiya ya nchi za Pwani na Jangwa. Misri pia inasisitiza juu ya  umuhimu wa kusoma vyanzo vengine vipya vyenye vya wasiwasi  , kwa kuzingatia uzushi wa uharibifu wa ardhi za kilimo , ukosefu wa maji na mahitaji ya maendeleo yanayohusiana na kushughulikia na maji yanayovuka mipaka.                                                                                                 

 

4- Hotuba ya Rais Abdelfattah Al-Sisi

Katika kikao cha 72 cha mikutano ya Umoja wa Mataifa, tarehe  19 Septemba 2017

Misri ilikuwa mojawapo ya nchi ambazo zinavutiwa sana na uzinduzi wa Mpango wa Bonde la Nile mwaka wa  1999, na  ilijaribu kufikia makubaliano ya pande  tatu kati ya Misri, Sudan na Ethiopia , kwa ajili ya kushughulikia suala la bwawa la maendeleo  kutokana na mtazamo wa ushirikiano,  unaoanzisha mfumo wa sheria zilizo wazi ili kukabiliana na suala hili kwa mujibu wa kanuni za sheria ya kimataifa, na sheria zilizoanzishwa ili kuratibu uhusiano kati ya nchi husika zinazoshirikiana   katika mabonde ya mto yanayovuka mipaka duniani kote.. Mkataba huu unabaki kuwa mfumo wa kisheria wenye uwezo wa kutafsiri mantiki ya ushirikiano kati ya Mataifa matatu,  wakati  malengo yametimia na kujitolea kwao kwa kutekelezwa kikamilifu na kwa uaminifu, hasa muda ni mdogo, na  utekelezaji wa haraka kwa yale yaliyokubaliwa awali ni jambo  muhimu sana, ili kuepuka kupoteza fursa ya kutoa mfano wa mafanikio kwa ajili ya usimamizi wa  uhusiano kati ya nchi tatu ndugu za Bonde la Nile.                                                                                                            

 

5- Hotuba ya Rais Abdelfattah Al-Sisi

Katika kikao cha 73 cha Mikutano ya Umoja wa Mataifa, tarehe  25 Septemba 2018

Kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda, hapa hasa ningependa kutaja majaribio yenye mafanikio ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika,  kama kielelezo cha kugawana mizigo na kutumia fursa za kulinganisha za kila upande ili kukabiliana na matatizo magumu katika bara letu, ambalo ni lengo kuu la juhudi za kimataifa katika uwanja wa kulinda na kujenga amani  na misaada ya kibinadamu na kimaendeleo. Pamoja na  Misri kukaribia kuchukua  Uenyeketi wa Umoja wa Afrika katika  mwaka wa 2019, tunatarajia kutekeleza  ushirikiano wa kimkakati kati ya Umoja wa Afrika  na Umoja wa Mataifa kupitia mipango yenye athari kubwa  katika bara,  na kujenga juu ya maendeleo yaliyofanywa ili kufufua sera ya  Umoja wa Afrika kwa ajili ya kujenga upya na maendeleo baada ya kipindi cha migogoro, pamoja na Misri kukaribisha  Kituo cha Umoja wa Afrika unaohusiana na utekelezaji wa sera hii , na aidha Kituo cha Nchi za Pwani na Sahara ili kupambana na Ugaidi.