Sera ya nje ya Misri kuelekeo Afrika Kupitia urais wa El-Sisi
Alhamisi, Machi 14, 2019
Sera ya nje ya Misri kuelekeo Afrika Kupitia urais wa El-Sisi

 

Kupitia urais wa El-Sisi

"Misri ni moyo wa Waarabu unaodunda .. Na akili yake ya kufikiri .. Mnara wa taa ya ulimwengu wa Kiislamu .. Na kituo cha mionzi ya sayansi za dini  .. Kwa ukati kati wake na uwiano wake .. Kwa kukataa kwake matumizi ya nguvu kwa njia yeyote iwayo.. Na kwa kukataa ugaidi kwa nia yake yeyote iwayo.. Misri ina mizizi na kuwepo katika maisha ya Afrika .. Kiongozi  wa  ukombozi na uhuru wa bara la Afrika, mdomo wa Bahari ya Kati, fahari ya ustaarabu, na rekodi ya utukufu wa historia. "

(Kutoka hotuba ya Rais Abdel Fattah Al-Sisi katika sherehe yake ya kukabidhiwa  Urais wa Jamhuri  ya Kiarabu ya Misri, Juni 2014)

 

Kwanza : Misingi na mifumo ya sera ya nje ya Misri kuelekea Afrika kupitia kipindi cha urais wa El-Sisi :

Uchambuzi wa hotuba ya kisiasa ya Rais Abdel Fattah Al-Sisi na harakati ya sera ya nje ya Misri kuelekea bara la Afrika tangu mwaka 2014  inathibitisha kanuni zifuatazo:

 

- Kuimarisha uhusiano wa Misri na Afrika na kuthamini utambulisho wake wa Afrika.. Ni kipengele muhimu zaidi ili kuunda sifa za kitamaduni za utu wa Misri.. Jambo hili limethibitishwa na maandiko na utangulizi wa Katiba ya 2014.

 

Ushirikiano pamoja na nchi za bara ili kupambana na changamoto : Ugaidi, uhalifu wa kupangwa, magonjwa na uharibifu wa mazingira.

 

 • Kuzingatia kanuni za "maendeleo na ushirikiano wa kikanda" ili kuwepo ujumbe wa Misri kwa nchi za bara kwa upande mmoja, na mpango wa Misri katika vikao vya kimataifa kwa upande mwingine.

 

 • Wingi na utofauti ya mfungamano na mahusiano kati ya Misri na nchi zingine za Afrika juu ya ngazi za kitamaduni, vyombo vya habari na kidini, na tunaweza kuita ni mfumo wa "umoja wa ustaarabu".

 

- Uwepo wa Misri kisiasa umepanuka na kujumulisha ushirikiano wote wa kongamano za kimkakati, kikanda na kimataifa pamoja na bara la Afrika, na hasa: Mkutano wa kilele cha Afrika –Washington  huko Marekani  Agosti 2014, Mkutano wa kilele cha India na Afrika Oktoba 2015, Kongamano la China-Afrika Desemba 2015 na Oktoba 2018, na  Mkutano wa kilele cha Ujerumani - Afrika katika miaka ya 2017  na 2018,  Mkutano wa kilele cha Afrika - Ulaya mwaka 2018.

 

 • Misri imekuwa mwenyeji wa Mikutano ya vilele na mikutano kadhaa muhimu ya Afrika kama vile: Mkutano wa kambi tatu (COMESA - SADC - Afrika Mashariki) – Kongamano la Uwekezaji barani Afrika katika vikao vitatu tangu 2016 - Mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Pwani na Sahara -  Mkutano wa Wenyekiti wa Benki Kuu barani Afrika katika mwaka wa 2018.  Na Mkutano wa Watawala wa  Mahakama Kuu ya Katiba barani  Afrika Februari 2018 - na Mkutano wa Onesho la Biashara ya Afrika Desemba 2018.. na mikutano na matukio mengine ya Afrika.

 

- Sera ya Misri - katika kiwango cha Afrika –ni  kanuni ya "Faida  kwa wote", hasa kuhusiana na maono ya Misri kwa ajili ya maendeleo ya nchi za Bonde la Mto Nile, ili kufikia maendeleo halisi endelevu ambayo hutoa maisha mazuri kwa  watu wa Afrika.

 

- Wakati wa uanachama wa Misri wa Baraza la Amani na Usalama wa Afrika tangu 2016, na Baraza la Usalama la Kimataifa  2016 - 2017, na uongozi wake kwa  Tume ya Kiafrika inayohusiana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa (2016-2017), Misri ilikuwa na nia ya kushughulikia  masuala ya Afrika na ilijitahidi kuunga mkono amani na usalama  wa Afrika. Misri imeongeza ushiriki wake katika ujumbe wa  Umoja wa Mataifa ili kuhifadhi amani katika bara hili, kwani Misri ilipata tena nafasi yake kati ya nchi 10 za juu zinazochangia kwenye ujumbe huo.

 

Pili: Diplomasia  ya Mkutano wa kilele.. na kuimarisha mahusiano ya Misri na Afrika :

 

Tangu kuchukua kwake uraisi mwakani  2014, Rais Abdel Fattah Al-Sisi amekuwa na nia ya kujitanua katika bara la Afrika, na kuimarisha mahusiano ya Misri pamoja na nchi za bara katika nyanja zote, na  mpaka mwishoni mwa mwaka 2018, Rais alitembelea nchi 25 za Afrika miongoni mwa ziara 86 za kigeni , na idadi hiyo inawakilisha kiasi cha  asilimia 30 kutokana na   ziara zote za Rais nje.

 1-  Ziara saba kwa Afrika katika mwaka wa kwanza wa urais

 • Kuanzia Juni 8, 2014 hadi Juni 7, 2015, Rais alifanya ziara saba katika Afrika, ziara hizi zimejumuisha nchi : Sudan (ziara 3) - Ethiopia ( ziara 2) - Guinea ya Ikwete ( ziara moja) - Algeria (ziara moja).

Rais alifanya mikutano 45 na viongozi na maafisa kutoka nchi za : Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Morocco, Algeria, Libya, Mali, Burkina Faso, Somalia, Senegal, Comoros, Gine ya Ikwete, Chad, Afrika ya Kati, Tunisia, Burundi, Afrika Kusini, na zingine.

 2- Mikutano 42 na viongozi wa Afrika katika mwaka wa pili wa urais

Kuanzia Juni 8, 2015 hadi Juni 7, 2016, Rais alifanya ziara mbili kwa Ethiopia na India ili kushiriki katika Mkutano wa kilele cha India - Afrika.

Rais pia alifanya mikutano 42 na viongozi na maafisa kutoka nchi za :  Eritrea, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Uganda, Gabon, Niger, Mauritania, Nigeria, Togo, Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Algeria, Libya, Comoros, Guinea ya Ikwete, Chad - Burundi - Afrika Kusini - Morocco - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na zingine.

3- Ziara 6 barani Afrika  mwaka wa  2016

 • Tangu Juni 8, 2016 hadi Juni 7, 2017, Rais El-Sisi alifanya ziara sita, zinazojumuisha kushiriki katika Mkutano wa kilele cha Afrika huko Kigali, na Mkutano wa kilele cha Kiarabu - Kiafrika huko Malabo, na Kilele cha Kiafrika huko Addis Ababa na ziara za pande mbili kwa nchi za Sudan na Uganda, na pia Rais alifanya  mikutano 25 pamoja  na maafisa na viongozi wa Afrika.

 

4- Ziara  kwa nchi nne za kiafrika katika mwaka wa 2017

 • Mwaka wa 2017 ulishuhudia ziara ya Rais El- Sisi kwenda Uganda Juni 22, 2017 ili kuhudhuria Mkutano wa kilele cha Bonde la Mto Nile, pamoja na mahudhurio ya Rais kwa Mkutano wa Kilele cha Ujerumani - Afrika tarehe 3/7/2017, pamoja na ziara ya Rais wakati ambapo alitembelea nchi nne za Afrika: Tanzania, Rwanda, Gabon na Chad, tarehe Agosti 2017.

 • Pia alikutana na Rais wa Zambia, Edgar Lungo, Novemba 2017, na maraisi wa Rwanda, Côte d'Ivoire, Libya na Guinea pembezoni mwa Kongamano la Afrika la 2017.

5- 2018 .. ni mwaka wa Mikutano ya vilele Misri na Sudan

Mwaka wa  2018 ulishuhudia  Mikutano ya vilele vitano vya Misri na Sudan vilivyofanyika katika  miezi ya Januari, Machi, Julai, Agosti na Oktoba .. kwa jumla ya mikutano 24 ya Misri na Sudan tangu mwaka 2014.

 

 • Mwishoni mwa Januari 2018 ulishuhudia ushiriki wa Mheshimiwa Rais katika Mkutano wa kilele cha 30 cha Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, kilichojulikana kama Urais wa Misri kwa Baraza la Amani na Usalama wa Afrika, na kulikuwa na majadiliano makubwa kuhusu suala la marekebisho ya taasisi ya Umoja.

 

 • Rais El-Sisi alifanya Mkutano wa kilele cha nchiTatu pamoja na Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Dessaline ili kujadili njia za kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili, na hasa juhudi za kuanzisha eneo la biashara huru..

 

 • Kupitia mahusiano ya kihistoria ya Misri pamoja na nchi za Pembe ya Afrika, Rais El-Sisi alimpokea Rais wa nchi ya Eritrea Asayas Afewerki, wakati wa ziara yake mjini Kairo Januari 2018, Kairo pia ilimpokea Rais wa Uganda Yoweri Museveni Mei 2018.

 

 • Juu ya ngazi ya kimataifa, Mheshimiwa Rais aliendelea kuhudhuria Mikutano ya Kimataifa inayohusu Afrika, hususan Kongamano la Ushirikiano wa China na Afrika huko Beijing, Septemba 2018,  na Kilele cha Kundi la 20  kuhusu ushirikiano pamoja na Afrika nchini Ujerumani mwishoni mwa Oktoba 2018.

 • Rais alishiriki katika harakati za Kongamano la Ulaya -Afrika, kwani Austria ilikuwa mwenyeji wake Desemba 2018.

Tatu : Afrika katika hotuba ya kisiasa ya Rais El-Sisi :

 

Uchambuzi wa hotuba ya kisiasa ya Rais Abdelfattah Al-Sisi kuhusu bara la Afrika unaonesha vipengele na masuala  yafuatayo:

-  Nia ya Misri ili kukomesha mgawanyiko na kuondokana na tofauti kati ya nchi za Bonde la Mto Nile na haja ya kufanya kazi ili kuondokana na  tofauti yoyote ambayo inazuia ushirikiano wa pamoja ndani ya Mpango wa Bonde la Mto Nile.

- Imani katika uchumi wa ujasiriamali kama utaratibu wa maendeleo ya bara.

- Umuhimu wa kukuza ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi barani Afrika.

- Wito wa Misri ili kushughulikia mtazamo kamili katika kupambana na ugaidi, kwa njia ambayo sio tu kwa mwelekeo wa usalama, lakini ni pamoja na upande wa kifikra.

- Wito wa kupitishwa  maono ya pamoja kulingana na uelewa wa ukweli kwamba kuna rasilimali ya vyanzo vya maji ya pamoja ya kutosha katika bonde ambavyo havijatumiwa kwa njia kikamilifu, na  ushirikiano wa  pamoja na utumiaji wa  njia za kisayansi na ya kisasa ili kufikia njia bora zaidi na endelevu ya matumizi rasilimali hizi.

- Kufikia maendeleo endelevu, kuundwa kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Afrika, kuendeleza miundombinu ya bara, kukuza uhuru wa  biashara huru kupitia Mkataba wa Biashara huru ya Kiafrika, kuendeleza  mfumo wa uchumi wa Afrika na aina zake, na  kuimarisha mfumo wa viwanda, haya yote  ni mambo muhimu ndani ya vipaumbele vya urais wa Misri wa Umoja wa Afrika katika mwaka wa 2019.

Nne: "Shirikisho la Misri kwa maendeleo" .. Nguvu za kimaendeleo za sera ya Misri barani  Afrika :

Shirikisho la Misri la Ushirikiano kwa Maendeleo lilianzishwa mwaka wa  2013,  na lilitangazwa na Rais Sisi katika hotuba yake kupitia Mkutano wa kilele cha 23 cha Umoja wa Afrika huko Malabo Juni 2014.

Na Misri imefafanua kazi za Shirikisho katika kutoa msaada wa kiufundi na misaada ya kibinadamu kwa nchi za Afrika na Kiislamu, na kuandaa mipango ya mafunzo, warsha na kupeleka wataalamu maalumu, na kutoa misaada ya kiufundi na kibinadamu, na kuchangia katika kutoa  fedha na kujumuisha  fedha kwa miradi ya maendeleo ya kiafrika na kuimarisha ushirikiano pamoja na Umoja wa Mataifa na mashirika yake maalumu na nchi zinazoendelea kupitia ushirikiano wa  Kaskazini-Kusini, pamoja na ushirikiano na  nchi kadhaa za Asia na Marekani ya Kusini na pia mashirika ya maendeleo ya kimataifa kupitia Ushirikiano wa Kaskazini - Kusini kwa manufaa ya nchi za Afrika. Na Shirika litafanya kazi zake kulingana na sheria za utendaji wa mashirika ya maendeleo ya kimataifa.

Shirikisho la Misri lina mahusiano ya ushirikiano wa pande tatu pamoja na nchi kadhaa na taasisi za maendeleo ya kimataifa kupitia ushirikiano wa Kaskazini-Kusini na Kusini-Kusini, Shirikisho ambalo lilishiriki katika kupanga programu za mafunzo kwa nchi za Afrika kama vile: Benki ya Maendeleo ya Kiislamu - Mfuko wa Kiarabu kwa Msaada wa Kiufundi kwa nchi za Afrika ulio chini ya Umoja wa  nchi za Kiarabu na Shirikisho la  Ushirikiano  la Kijapani la Kimataifa  (JICA).

 

Kama sehemu ya kujitolea kwake kwa muda mrefu kwa Afrika, Serikali ya Misri imetenga bajeti maalumu kila mwaka kwa Shirika hilo.Kama uhamasishaji wa rasilimali za  nyongeza kutoka kwa mashirika ya wafadhili na mashirika ya kimataifa kulingana na makubaliano ya pamoja na Shirika hilo. Katika hali hii, pia mafanikio hutumika  kuchangia  gharama kupitia ushirikiano wa pande mbili pamoja na nchi ya Afrika inayofaidika, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa pande tatu pamoja na nchi wafadhili (au pamoja na  shirika la Umoja wa Mataifa au shirika la kimataifa).

Tano: Maendeleo ya bara la Afrika .. Kongamano la Afrika na mfano wa ushirikiano «Kusini - Kusini»:

Mfumo ya Ushirikiano " Kusini-Kusini " unawakilisha  mfomu unaofaa kwa mahitaji na changamoto za bara la Afrika, ili kufikia maendeleo endelevu kupitia mipango ya ushirikiano wa kiufundi na program za mafunzo ili kujenga uwezo wa viongozi wa Afrika katika nyanja mbalimbali na ya mwanzo yake ni : kilimo, afya, elimu, usalama, diplomasia, mahakama na vyombo vya habari, pamoja na misaada ya kifedha, hasa katika nyanja za afya na kilimo.
.

Katika hali hii,  na kupitia kipindi cha uongozi wa Raisi El-Sisi , Misri ina nia ya kuzingatia sera yake kuelekea bara lake la asili juu ya faida za kiuchumi na mikakati ya ushirikiano wa kikanda wa Afrika.

Na" Kongamano la Afrika"  katika vipindi vyake vitatu: 2016, 2017 na 2018,  ambavyo vyote vilifanyika  mjini Sharm el-Sheikh, vinawakilisha moja ya nguzo za mkakati wa Misri wakuelekea bara la Afrika, pamoja na ushiriki wa maraisi na  wakuu wa serikali na maafisa wakuu katika serikali barani Afrika na ulimwenguni , pamoja na wajasiriamali wa  kimataifa wa uwekezaji wa sasa wenye uwezo Afrika, na wawakilishi wa taasisi za kifedha za kimataifa na wataalamu na wasomi wanaohusika na uchumi wa Afrika.

1-  Malengo ya  Kongamano la Uwekezaji barani  Afrika:

-  Msaada wa Misri kwa mchakato wa maendeleo barani Afrika, kwa kuzingatia kwamba  nguvu ya Misri ya kiuchumi ni kubwa zaidi katika bara la Afrika.

- Kukamilisha  juhudi  za kuanzisha  eneo la biashara huru, ambalo lilianza hatua zake za kwanza mjini  Sharm El-Sheikh  mwaka  wa 2015, kupitia  kutangazwa  kwa Mkataba huru wa kambi tatu: COMESA, SADC na Afrika Mashariki.

 

- Kutekeleza makubaliano ya kambi tatu, inayozingatiwa hatua muhimu kuelekea kuanzishwa kwa Umoja wa Kiuchumi kwa Afrika ifikapo mwaka wa 2063, ambayo itatoa ushindani barani kuvutia uwekezaji, na kuboresha biashara kati ya nchi zote na kuunganisha ushirikiano mbalimbali wa kiuchumi.

 

- Kujenga hali ya "usawa" katika mahusiano ya kiuchumi kati ya bara la Afrika, na washiriki wa kawaida wa kimataifa…  na wafadhili wa kimataifa.

2 -  Wahusika waafrika na wa kimataifa  1200  wakati wa "Kongamano la Afrika katika mwaka wa 2016".

Kongamano la Afrika la 2016 liliwakusanya washiriki zaidi ya 1,200 kutoka nchi 45, na kongamano lilishuhudia kufanyika  zaidi ya mikutano 300 ,  na makubaliano  7 ya uelewa yalisainiwa kati ya serikali za kiafrika na sekta binafsi katika nyanja za nishati, miundombinu, huduma za afya na usimamizi wa takataka. Na kongamano lilipendekeza umuhimu wa kujenga mazingira sahihi kwa wawekezaji ili bara linaweza kucheza nafasi yake kama mchezaji wa kisiasa na kiuchumi mkubwa katika ngazi ya kimataifa.

 1. "Kongamano la Afrika la 2017" … ajenda ya maendeleo kabambe kwa bara la Afrika

Kongamano lilijaribu kugundua fursa za uwekezaji katika miradi inayowezekana  kufadhiliwa, na  Mkutano wa 2017 ulionesha siku ya makampuni yaliyojitokeza na kuongoza wajasiriamali,waliopata mazungumzo kamili kwa ajiliya ya kazi za  kibiashara na  maonesho katika suala hili, ili kuvutia fedha na ushirikiano kwa baadhi ya miradi ya ubunifu zaidi kutoka Kairo hadi Cape Town.

Na kongamano lilihitimisha kwa  mapendekezo kadhaa, hususan: kuanzishwa miradi ya pamoja hasa katika uwanja wa miundombinu, utekelezaji wa mipango ya kuchochea ujasiriamali, na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja zote za shughuli za kiuchumi kama kipengele cha ufanisi katika mchakato wa maendeleo barani Afrika.

4 -  Kongamano la Afrika mwaka wa 2018 ..  Ujasiriamali na Uwezeshaji wa Wanawake wa afrika

- Kongamano la "Afrika 2018" lilijadili katika toleo lake la tatu, taratibu za kupata ushindani wa haki, ulinzi wa uwekezaji wa ndani  kupitia  COMESA, mwenendo mpya kwa fursa za kiuchumi, mabadiliko ya tarakimu, na  ujasiriamali.

- Kipindi cha 2018 kiliweka  Siku ya wajasiriamali vijana, ili kujadili kuchochea wajasiriamali na kuimarisha makampuni machanga katika bara na kufikia kimataifa, na kongamano lilishuhudia pia kufanyika kwa Mkutano wa "Kuwawezesha Wanawake Waafrika" ili  kujadili njia za ushiriki wake katika  kuunda mipango ya kiuchumi na kisiasa  kwa bara na kuunda mustakbali wake.

 

- Mapendekezo makuu ya Kongamano la 2018 yalikuwa :  kuanzishwa kwa mfuko wa dhamana ya hatari za uwekezaji barani  Afrika, majadiliano pamoja na taasisi za kimataifa ili kusaidia miundombinu kwa ajili ya kuunganisha nchi za bara  ,  na kupanua shughuli  za biashara, na  kuanzisha  mfuko ili kuwekeza katika miundombinu ya habari na ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na nchi za Aafrika katika nyanja za utawala Kupambana na ufisadi, na kuzindua awamu ya pili ya mkakati wa kitaifa ili Kupambana na ufisadi 2019-2022 kama sehemu ya ukumbusho wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ufisadi.

Sita : Rais  El-Sisi .. Na kutetea  nafasi ya Afrika kuhusu  mabadiliko ya hali ya hewa:

Katika kipindi cha 2015-2016, Misri imetilia umuhimu mamboya mabadiliko ya hali ya hewa barani  Afrika,  kwa mujibu wa Rais Sisi alichukuliwa kama mratibu wa tume ya marais wa nchi na serikali za Afrika zinayohusiana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa CAHOSCC  hadi  mwisho wa mwaka wa 2016,  kwa kushirikiana na urais  wa Misri kwa mkutano wa mawaziri  wa mazingira  Afrika AMCEN  kwa muda wa miaka miwili  2014-2016.

Katika hali hii, Misri ilijaribu kuimarisha masuala yafuatayo yanayohusiana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika bara la Afrika:

- Ushiriki wa Misri katika majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa, kupitia  jukumu lake la kuwakilisha bara la Afrika na kuratibu nafasi zake, na kuonesha mpango muhimu wa bara la Afrika kuhusu  kuhamasisha msaada wa kimataifa kwa shughuli za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.

- kuzungumza kuhusu juhudi zinazofanywa na bara la Afrika ili kukuza matumizi ya nishati mbadala katika nchi za bara, kulingana na hatua za kimataifa ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, na mipango ya kufikia maendeleo endelevu.

 • Kusisitiza juu ya umuhimu wa utekelezaji kwa nchi za wafadhili na zinazoonesha majukumu yao yaliyotolewa katika  mkataba wa Paris, hasa ugawaji wa dola bilioni 10 kwa ajili ya utoaji fedha  kwa mpango wa nishati mbadala barani Afrika.