Misri na Afrika Kusini
Jumapili, Machi 10, 2019
Misri na Afrika Kusini

     Misri ilipambana na ukoloni tangu miaka mingi iliyopita na baada ya kupata uhuru wake ilikuwa na msimamo wa wazi katika kuunga mkono harakati za uhuru barani Afrika kwa ajili ya kupata uhuru. Misri ilijiunga na mpango wa kimataifa dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.  Na baada ya kuondoa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na kuanzisha serikali ya kwanza ya umoja wa kitaifa nchini Afrika Kusini katika mwaka 1994, Misri  ilianzisha mahusiano ya kidiplomasia na Afrika Kusini kwa haraka na kushirikiana naye katika nyanja zote. Misri ilidhihirisha umuhimu mkubwa wa kuimarisha mahusiano na Afrika Kusini na kuratibu pamoja na nchi hiyo ili kuunga mkono bara la Afrika kwani nchi hoyo na Misri zinazingatia ni nchi mbili kubwa zaidi barani Afrika ambazo zina nafasi ya pekee kaskazini na kusini mwa bara. Pia zina ukubwa na uwezo wa kushiriki kwenye majukumu muhimu katika viwango vya kikanda na kimataifa.

Mahusiano ya kisiasa

    Mahusiano ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili yanashuhudia maendeleo ya wazi katika kipindi cha kisasa, ambapo marais wa nchi hizo mbili walifanyika mikutano kadhaa, wa kwanza ni pembezoni mwa Mkutano wa ngazi ya juu wa kikao cha 70 cha Jumuia kuu wa Umoja wa Mataifa New York, mwezi wa Septemba 2014, na kisha ziara ya Rais wa zamani Jacob Zuma kwenda mjini Cairo kwa kuitikia mwaliko wa Rais" Abdel Fattah El Sisi " katika mwezi wa Aprili 2015, ambayo ndiyo ziara ya kwanza ya Rais wa Afrika Kusini tangu mapinduzi ya Januari 2011, na ziara ya mwisho ya rais wa Afrika Kusini mjini Cairo ilikuwa katika mwezi wa Oktoba 2010, na marais wawili hawa walikutana mjini Moscow mwezi Mei 2015 pembezoni mwa sherehe za nchi kwa kumbukumbu ya miaka 70 kuhusu kushindia Nazism katika Vita vya Dunia vya Pili.

    Waziri Mkuu mstaafu Muhandisi: Ibrahim Mihleb alishiriki katika kikao cha kawaida cha 25 cha Mkutano wa Afrika huko Johannesburg Juni 2015. Na pia Waziri Mkuu wa zamani Sherif Ismail alishiriki katika Mkutano wa China na Afrika huko Johannesburg Desemba 2015. Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Sahar Nasr pia alishiriki katika Mkutano wa Kiuchumi wa Dunia kwa Afrika Juni 2015, kwa niaba ya Waziri Mkuu.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini  mara kadhaa, na hayo yamekuja pembezoni mwa kikao cha 70 cha Jumuia Kuu ya Umoja wa Mataifa Septemba 2014, na pia katika Mkutano wa "kurejesha ujenzi wa Gaza" huko Cairo tarehe 12 Oktoba 2015. Wakati wa ziara ya Rais wa zamani Jacob Zuma kwa Cairo Aprili 2015, na pembezoni mwa shughuli za Mkutano wa kilele cha Umoja wa Afrika huko Johannesburg katika mwezi wa Juni 2015, na pia pembezoni mwa shughuli za Mkutano wa kilele wa jukwaa la China na Afrika huko Johannesburg Desemba 2015.

     Pretoria ilielezea matumaini yake ya kuendelea kikao cha tisa cha Kamati ya Pamoja kati ya nchi mbili mwaka 2015, ambapo imepangwa  Cairo kuwa mwenyeji, ambapo kikao cha nane cha Kamati ya Pamoja kilifanyika chini ya uwakilishi wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo mbili huko Pretoria mnamo Machi 2010. Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ilifanya mkutano wa uratibu kati ya ubalozi na wawakilishi wa taasisi za serikali zinazohusika ili kujua maendeleo ya hivi karibuni ya kupanga kamati ya pamoja, na upande wa Afrika Kusini ulielezea matumaini yake na kupokea tarehe zilizopendekezwa ili kufanya Kamati ya Pamoja wakati wa 2016, kwa kuzingatia kikao kijacho cha Kamati ya pamoja ya kibiashara wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka wa 2016.

    Miaka ya 2014 na 2015 ilishuhudia ziara ya wajumbe kadhaa wa Misri kwenda Afrika Kusini, wakiongozwa na waziri wa zamani wa utafiti wa Sayansi na Pretoria mnamo Februari 2015, pamoja na ziara ya ujumbe wa serikali kutoka Kituo cha Uzalishaji Safi na kutoka Umoja wa Viwanda vya Misri mjini Pretoria Desemba 2015, licha ya ziara ya ujumbe wa Misri kutoka Tume Kuu ya Uchaguzi, Wizara ya Haki, baraza la nchi na Asasi za kiraia mjini Pretoria mwaka 2014, pamoja na ziara nyingine, hivi karibuni ziara ya ujumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa ya Misri kwa Tume ya Uchaguzi ya kujitegemea ya Afrika Kusini Septemba 2018.