Mahusiano ya Misri na Aljeria
Jumamosi, Aprili 13, 2019
Mahusiano ya  Misri  na  Aljeria

*Historia 

Mahusiano  ya Misri na Aljeria  yanaongozwa na urithi wa kihistoria wa kusaidia na kuunga mkono  kwa  kubadilishana. Wakati ambapo Misri iliisaidia Aljeria katika mapinduzi yake matukufu kwa ajili ya kuumaliza ukoloni wa kifaransa katika mwaka 1954. Na Misri ilikabiliwa na uadui wa pande tatu ( ufaransa,Israel, na uingereza ) mwaka 1956 kutokana na kusaidia na kuunga mkono kwa misri  kwa  mapinduzi ya Aljeria. VilieVile raia wa Aljeria hawatasahau kamwe  misaada ya misri iliyoendelea baada ya uvamizi mpaka raia wa Aljeria wapate uhuru. Uhuru huu  uliwagharimu thamani kubwa ya roho za wanae zaidi inapindukia shahidi milioni. Raia wa misri kwa upande wake hawatasahau kamwe kwamba Aljeria, raia wake na raisi Hawari Bumdin waliisaidia kwa ngazi za kisiasa na kifedha  baada ya janga la mwaka 76. Kusaidia huku kuliendelea baada ya kifo cha raisi Abdal Nasar mpaka kutokea kwa vita vya mwaka 1973 ambapo vikosi vya Aljeria vilishiriki katika vita hivi . Ambapo Aljeria ilikuwa nchi ya pili kwa kusaidia  vita vya mwaka 1973. Na ilishiriki katika upande wa Misri kwa silaha ya 8ya mnyororo wa mitambao kwa ushiriki wa wanajeshi 2115 na mistari 128 ya maafisa wa jeshi  na maafisa 192 wa Aljeria. Aljeria iliipa Misri vifaru 96 na makombora 33 na makombora 12 ya ardhini na makombora 16 dhidi ya ndege pamoja na zaidi ya ndege mpya aina ya mig 21 na mig 17 na sokhawi 7. Misri na Aljeria zina maslahi mengi ya pamoja kwa mikondo mbali mbali ya kisiasa na ya kiusalama na ya kiuchumi na ya kiutamaduni. Ambapo mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi mbili yalishuhudia uboreshaji mkubwa baada ya mapinduzi ya 30 Juni  kwa fadhila ya kushirikiana  kwa Misri na Aljeria katika mtazamo mmoja wa kisiasa na mlingo wa mitazamo  katika maswala ya eneo. Aljeria inazingatiwa kuwa ni nchi ya kwanza ambayo raisi, Abdal  Fatah EL-Sisi aliizuru tangu aingie madarakani kwa kuchaguliwa katika mwezi  wa  Juni 2014. Jambo ambalo lilipelekea kutokea kwa uboreshaji mkubwa wa mahusiano ya nchi mbili.  

*Mahusiano  ya  kisiasa

Misri na Aljeria zinafanana katika mambo mengi ambayo  yanapindukia  urithi ambao haukanushiki bali inafikia kuusimamia mustakabali  ambapo  mwelekeo wa nchi mbili  unakuwa  wa  ushirikiano ndani yake. Jaribio  la Aljeria  katika kupiga vita ugaidi linazingatiwa kuwa ni  jaribio la kipekee na la aina mbali mbali. VileVile suala la Libya  linahitaji juhudi za nchi mbili. Mahusiano  ya kisiasa yaliyo imara  baina ya nchi mbili  yanatoa urithi wa kipekee kwa ajili ya  kuimarisha  mahusiano katika Nyanja mbali mbali  na khasa katika muktadha wa hali ya mambo  yanayokabiliwa na mataifa ya kiarabu ukiongezea na  mabadiliko yanayashuhudiwa na  mataifa ya kiafrika.

 

Kuna  mlandano kamili wa mitazamo ya nchi mbili  unaohusiana na suala la Libya kuhusu umuhimu wa utulivu wa kiusalama nchini Libya na kulijenga taifa la Libya na kuyakidhi mahitaji ya raia wa Libya pamoja na kuzijenga taasisi zake zinazotoa mchango muhimu wa kulisimamisha  taifa.

Katika muktadha wa mashauriano ya kudumu nchi mbili zinatilia umuhimu  wa kuimarisha  mahusiano  ya  pande mbili na utaratibu wa pamoja kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ambazo taifa linakumbana nazo pamoja na kufautilia maswala yote ya mataifa ya kiarabu na mabadiliko yanayotokea katika pande mbili za kiarabu na kiafrika  ambayo yakitangulizwa na suala la Palestina na hali ya kiusalama katika nchi za Iraki, Siria na Yamin ukiongezea na  kuuhakikisha utulivu wa kisiasa katika mataifa ya kiarabu na ya kiislamu na ya kiafrika. VileVile nchi mbili zinatilia umuhimu mkubwa wa kupiga vita makundi ya kiugaidi katika kipindi muhimu cha historia ya eneo ukiongezea na uratibu wa pamoja  unaohusiana na maswala ya kiafrika na ya kiarabu na ya kiafrika.

*Mahusiano  ya  kiuchumi

Nchi  hizi mbili zina mahusiano ya kiuchumi yaliyo imara sana  hayaishii katika kiwango cha ubadilishano wa kibiashara  bali yanajumuisha pia  uwekezaji wa pamoja baina ya nchi mbili. VileVile kuna safari zinazoandaliwa na wafanyabiashara ili kutambua  mazingira na uwezekano ili kuyasimamisha mashirika ya pamoja. Baadhi ya wamisri wanakuja nchini Aljeria ili kuwezeka na kinyume chake ni sahihi.  

Misri inazingatiwa kuwa ni mmoja wa wawekezaji wa kiarabu walio muhimu sana nchini Aljeria. Kiwango cha vitega uchumi vya misri nchini Aljeria kinakadiriwa kwa dola za kimarekani bilioni 3,6. Na kiwango cha ubadilishano wa kibiashara baina ya nchi mbili kinafikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni. Ama kuhusu kiwango cha vitega uchumi vya Aljeria nchini misri hakipindukii dola za kimarekani milioni 90. 

Nchini Aljeria kuna mashirika 32 ya kimisri yanayafanya kazi katika Nyanja za mawasiliano, ujenzi, shughuli za umma, viwanda, huduma na kilimo. Mashirika haya yana ushiriki mzuri na mkubwa pamoja na mashirika ya Aljeria.   

Kuna jukumu kubwa ambalo baraza la wafanyabiashara wa misri na wa Aljeria  limebebeshwa ili kufungua masoko na kutekeleza miradi ya pamoja katika Nyanja zote. Ambapo mashirikiano baina ya nchi mbili katika uwanja wa nishati yanazingatiwa kuwa ni miongoni mwa vipaumbile vikuu mnamo kipindi kijacho. Aljeria ilikuwa imeahidi kuongeza kiwango cha bidhaa zake za majiko ya gesi  inazozisafirisha  kwa misri kwa asilimia 50 ili kufikia tani milioni 1,5 kila mwaka.  VileVile nchi mbili zinakuwa na shime kuimarisha mashirikiano na kuongeza harakati za ubadilishano wa kiutalii na khasa pamoja na ongezeko kubwa lililosajiliwa kwa idadi ya watalii wa Aljeria waliokuja nchini misri katika mwaka 2018. Ambapo idadi hii ilifikia hadi watalii elfu 43 wa Aljeria. Aidhaa kumetimia kuendesha safari 11 za anga kila mwaka baina ya nchi mbili. Mji wa Sharm EL-Shekh unazingatiwa kuwa ni kusudio linalopendewa na watalii wa Aljeria.

VileVile yanafanyika maandalizi ili kufanyika tume ya pamoja baina ya nchi mbili ili kuhakikisha mhamo wa kiaina wa ushirikiano baina ya nchi mbili katika robo ya kwanza ya mwaka 2019.  Umoja wa vyumba vya kibiashara vya kimisri unataka kuharakisha ili kuanzisha njia ya majini ya moja kwa moja inayounganisjsha kati ya Misri na Aljeria kwa lengo la kupunguza gharama za kupakia na kuongeza bidhaa zinazoagizwa kutoka Aljeria  kupitia mhimili wa mfereji wa Suweiz. Mhimili huu unazingatiwa kuwa ni kituo cha uchukuzi kwa ajili ya mataifa ya kiarabu, Afrika mashariki  na Asia . Pia inapendekezwa kujiunga Aljeria katika makubaliano ya "AGHADIR" ya kiuchumi pamoja na Tunisia, Moroko na Aurdun kwa lengo la kuuhakikisha ushirikiano kamili wa viwanda na kuongeza bidhaa za nje katika masoko mapya . 

Mahusiano ya kiuchumi baina ya Misri na Aljeria  yameongeza kwa kiwango kikubwa tokea mwaka 2014 baada ya kufanyika kongamano la saba la kamati kuu ya pamoja ya misri ya Aljeria chini ya uangalizi wa waziri wakuu  wa nchi mbili, BW. Ibrahim Mihlab na Abdal Maelk Salal. Katika kongamano hili yametia saini makubaliano 17 baina ya nchi mbili yanajumuisha sekta mbali mbali.

Bidhaa zinazoagizwa kutoka Misri zinajumuisha :"aluminiamu, chuma na chuma cha pua, nyaya za bodi, simenti  na aina zake, vilivyosindikiwa katika vinywaji,  madawa, kiyoyozi, viwembe na mashine za kunyolea, mbegu za kutia nguvu na mboga mboga, vifaa vya kuzalishia majiko ya gesi, mashine za kufulia, majokofu na spea za magari, mifereji na mabomba ya shaba, injini za umeme, vifaa na taa za kuangazia zilizotengenezwa,bidhaa zinazotengenezwa kwa karatasi, bidhaa zinazotengenezwa kwa plastiki, zana na vitabu vya shule na vya vyuo vikuu, machapisho,magazeti  na  majarida  . Ama kuhusu bidhaa zinazoagizwa kutoka Aljeria zinaishia katika bidhaa zinazotengenezwa kwa petrol.

*Mahusiano  ya  kiutamaduni  na ya kihabari 

Kuna ubadilishano wa kiutamaduni kwa kiwango cha juu na imara baina ya Misri na Aljeria. Ubadilishano huu unapatikana kwa uhudhuriaji  wa kipekee wa nchi mbili katika matukio na shughuli za pamoja au shughuli zinazoandaliwa na nchi nyingine. Na  miongoni mwa ushiriki ulio muhuhimu sana katika nyakati za hivi karibuni ni ushiriki wa Misri kama vile, shamrashamra za constantinal "Mji mkuu wa utamaduni wa kiarabu " na  uhudhuriaji wa Misri kama mgeni wa heshima katika banda la kimataifa la vitabu na uhudhuriaji wa Aljeria kama mgeni wa heshima katika banda la kimataifa la vitabu mjini Kairo katika mwezi wa Febuari 2018 pamoja na ushiriki wa kimisri wa kudumu katika matamsha yote ya kiutamaduni yanayofanyika nchini Aljeria kama vile,  tamsha la Waharan la sinema ya kiarabu. Ambapo  kunatimia kuwatoza tuzo baadhi ya wasanii wa kimisri kwa sura ya kudumu katika makongamano ya tamsha.

Ni vyema kuashiria kwamba raisi wa Aljeria, BW.Abdal-Azizi Abu Tikila alimtoza tuzo msanii mkubwa wa kimisri, Mahmoud Fawzi  ambaye ni mtia sauti wa wimbo wa taifa wa Aljeria " KASAM" kwa kumpa zawadi ya nishani ya taifa na kuliandika jina lake katika nishani hiyo  kwa wananchi kuutambua mchango wa msanii huyo nguli aliyetoa kwa ajili ya Aljeria sauti nzuri yenye nguvu ya wimbo wa taifa ulimwenguni kote.

VileVile Aljeria inaitazama Misri kama kituo cha usambazaji wa kiutamaduni na wa kifasihi na wa kiustaarabu kwa muda wa karni kadhaa na mpaka sasa. Ambapo  Misri  ilichangia kwa kiwango kikubwa katika mambo yaliyohakikishwa  na  ustaarabu wa kiislamu. Aidhaa mnamo zama ya kisasa Misri ilikuwa ni mwanzo wa maendeleo ya kiarabu pamoja na chanzo cha usasa. Na hayo kwa fadhila ya vyombo  vyake  vya  habari, wasomi wake, wasanii wake na wataalamu wake. Na kupitia kwake ilianza zama ya kuthakafisha  kwa kiarabu kwa kiislamu. Vyuo vikuu vyake vikubwa vilikuwa ni tembeleo la wanafunzi kutoka pande mbali mbali duniani. Hakuna mtu ye yote anazikana fadhila zake juu ya utamaduni wa kiarabu. Aidhaa pataoneshwa maigizo ya kimisri katika runinga za Aljeria. Na nchi mbili zinakuwa na shime  kuchangamsha  vyombo vyote vya kiutamaduni na vya habari na khasa  kuanzisha moja ya aina za mashirikiano baina ya runinga maalumu za Misri za Aljeria ili kujenga picha ya hali halisi katika nchi mbili.

*Mahusiano  ya  kidini

VileVile  ushirikiano baina ya nchi mbili unafikia ili kuyajumuisha maswala ya kidini. Nao ni uwanja ulio muhimu kwa ajili ya pande mbili. Ambapo Aljeria inashiriki katika shughuli zote za  kidini zinazoandaliwa na Azhar Shariif na ofisi ya fatwa pamoja na wizara ya mambo ya wakfu. Aidhaa Misri inahudhuria shughuli za kidini nchini Aljeria. Nchi mbili zina maslahi ya pamoja yanahusiana na kuinua maadili ya usamehevu wa kidini na ukati ambao uislamu umejengeka kwao na kupiga vita msimamo mkali pamoja na kufanya upya mazumgumzo ya kidini.