MISRI na ANGOLA
Jumanne, Septemba 24, 2019
MISRI na ANGOLA

                                                             Misri na Angola

Mahusiano kati ya Misri na Angola yanarejea kwenye miaka ya sitini katika karne iliyopita, ambapo wananchi wa Angola walikuwa wakishiriki katika mapambano kwa ajili ya uhuru  na yalifika kiwango cha juu mwaka 1979 wakati wa ufunguzi wa Ubalozi wa Angola nchini Misri.

                                                               Ziara za pamoja

Tarehe 15/8/2018 bwana  Joao Baptista Borges  Waziri wa Nishati  na Maji wa Angola pamoja na  ujumbe wake walifanya ziara  nchini  Misri na Dkt.Muhamad Shaker  Waziri  wa  Umeme na Nishati mbadala aliwapokea , pande zote mbili walijadili njia za kuimarisha na kukuza mahusiano kati ya nchi mbili katika nyanja  za umeme na Nishati mbadala.

Januari 2018 Rais abdul Alfatah Sisi  alimpokea Rais wa Angola  " João Manuel Gonçalves Lourenço"   katika makao yake  Addis Ababa pembezoni mwa kushiriki kwake katika Mkutano wa Afrika, Rais wa Angola João Manuel Gonçalves Lourenço  alisisitiza juu ya dhamira ya Misri ya kuendeleza ushirikiano  na Angola katika uwanja wa kujenga uwezo kupitia programu za mafunzo zinazotolewa na shirika la ushirikiano la Misri ili kufanikisha maendeleo katika nyanja tofauti, Rais wa angola ameonesha  juhudi zinazotolewa na nchi yake katika kuboresha miundombio baada ya miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopita, akionesha nia yake ya kufaidika kutokana  na  uzoefu wa Misri katika uwanja huu.  Rais wa Misri alionesha  kuwa Misri ipo tayari kushirikiana na Angola katika suala hili na kutoa uzoefu wake.

Ziara ya mwenyekiti  wa baraza la michezo la Kitaifa kwenda Angola mara mbili mwezi wa Januari 2010 ili kuhudhuria shughuli za ufunguzi na hitimisho   la michuano ya mataifa ya Afrika  ya soka "Angola 2010 kwa mwaliko wa mwenzake wa Angola Mwandumba.  

 Mawaziri na maafisa kadhaa wa Angola walitembelea Misri wakati wa 2009 na 2010 ili kuhudhria mikutano kadhaa na sherehe za kimataifa,ili kukuza na kuimarisha  mahusiano kati ya nchi hizo mbili, na miongoni mwa ziara muhimu zaidi zilizotajwa ni ziara ya Waziri Mkuu wa Angola (Antonio Paolo kasuma  (Spika  wa bunge la sasa ) na Waziri wa Mambo ya nje (Asuncao  Dos ingush ) kuhudhuria mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote  uliofanyika  julai 2009 katika mji wa Sharm El Sheikh.

 

Ziara ya Waziri wa Mipango wa Angola  Ana Diaz Loranso akiwa na ujumbe wa Angola ambao ulijumuisha Mawaziri kadhaa  ili kushiriki  katika Mkutano wa China-Africa, uliofanyika Sharm El-Sheikh kutoka tarehe 6 hadi 9 Novemba 2009.

Ziara ya Waziri wa Vijana na Michezo wa Angola mjini kairo katika mwezi wa februari 2010 kuitikia wito wa mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Kitaifa kuhudhuria Mechi ya timu ya Angola ya mpira wa mikono wakati wa michuano ya  Mataifa ya Afrika ya mpira wa mikono mjini kairo.

 

                                                           Mahusiano ya kiuchumi

 

Misri na Angola  zina nia ya  kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati yao, na kufaidika na mahusiano ya kisiasa bora kati ya nchi hizo  mbili , na kuzitafsiri kwa miradi halisi ya biashara, viwanda na uwekezaji  inayoonekana , ambayo inahudumia  uchumi wa misri  na Angola , Misri  inaunga mkono uwekezaji  wa Wamisri barani Afrika na kinyume chake na inafanya  kazi  ya kuendeleza  na kuboresha masuala ya bara kupitia mawasiliano mazuri na ya kindugu, , na  kukuza  maendeleo ya  uchumi  barani Afrika.

. Angola ina nia ya  kuongezeka ushirikiano na Misri katika sekta ya mafuta, ambapo Angola ina uzoefo mkubwa  na inaweza kushirikiana na Misri kupitia uzoefo wake katika tawi hili la shughuli  kutoka sekta ambayo inaiweka Angola  katika mstari wa mbele  wa uzalishaji mafuta  yasiyosafishwa (barani Afrika, ushirikiano katika sekta hii inachangia  kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza  maendeleo  endelevu kati  ya nchi hizo mbili.

Angola ilishiriki katika maonesho ya Afrika ya biashara ya Ushirikiano Desemba 2018 ikiwa na  waoneshaji 24 na wafanyabiashara 60.  Ushiriki mzuri wa Angola uliashiria  mwanzo wa awamu mpya ya uhusiano wa uchumi  mzuri  pamoja na Misri .

Kampuni tano za Misri zilishiriki kwa mara ya kwanza katika  maonesho ya Luanda ya Kimataifa Julai 2009,  ambapo kampuni hizo zilionesha mifano ya bidhaa zao, kampuni muhimu zaidi ilikuwa  kampuni ya Saruji ya Qena, ,Samani za El Qasr na nyingine za vifaa vya  plastiki za majengo.

Kiasi cha ubadilishanaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili ni kama Mikataba michache ya biashara  inayoendeshwa  kwa njia  isiyo ya  mpangilio, na inafanywa na kikundi cha makampuni ya Kimisri kama El Sewedy Cables, iliyotuma ujumbe kutoka kampuni hiyo kwenda Luanda  Julai 2009 kujadili fursa za usafirishaji wa bidhaa za kampuni hiyo nchini Angola na baadhi ya kampuni zingine za viwanda na biashara katika nyanja kadhaa.   

Pia kuna bidhaa nyingi za chakula za Misri (vyakula na vinywaji) katika soko la Angola ambazo huingizwa kupitia wafanyabiashara  wa Lebanon waliopo  Angola au moja kwa moja kupitia baadhi ya kampuni za Misri ambazo zinajaribu kupenya  kwenye soko la Angola lenye mustakbali bora.