Misri na Chad
Jumatatu, Februari 25, 2019
Misri na Chad

Utangulizi

Mahusiano kati ya Misri na TChad yanajulikana kwa ubora katika ngazi rasmi na ya  Kitaifa, ambapo TChad imejitahidi kuhifadhi na kudumisha uhusiano na Misri kwa sababu ya mchango wa Misri katika  uwanja wa Afrika tangu Misri ilipopata uhuru wake mwaka 1952.

        Mahusiano kati ya Misri na Tchad ni ya muda mrefu kwa kuizingatia kama ni nchi muhimu kwa usalama wa taifa la Misri na imepakana pamoja na Sudan na Libya, Historia ya TChad inarejea kwenye Enzi ya Ufalme, ambapo utawala wa kwanza wa kiarabu na Kiislamu ulianzishwa nchini TChad katika karne ya pili na ya nane Hijra.  Jina lake lilikuwa Mamlaka ya  (Kanimu) kaskzini Mashariki mwa Ziwa la TChad, kisha ilipanua ushawishi wake katika karne ya tatu Hijra hadi eneo lote la Sudan ya kati, mpaka ilipoanguka chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia 1920 mpaka kupata uhuru wake mwaka 1960.

Ziara za Pamoja

Ziara ya Rais Abdel Fattah Alsisi nchini Tchad, Agosti 2017.

Mhandisi Sharif Ismail, Msaidizi wa Rais wa Jamhuri kwa miradi ya kitaifa na ya kimkakati kama ni Mjumbe maalumu wa Rais wa Jamhuri tarehe 16/10/2018, alitembelea TChad, na alipokelewa na Ashta Saleh Damani, Katibu wa Nchi kwa Mambo ya Nje  na ushirikiano wa  Afrika na Kimataifa nchini TChad. Ismail pia alikutana na Waziri wa Mafuta wa TChad.

Rais wa TChad, Idriss Deby, alitembelea Misri mwezi Desemba 2014, Ziara hii imeshuhudiwa kutia saini rasimu yamaelewano  kuhusu ushirikiano katika Nyanja za kilimo na afya.

Waziri Mkuu wa zamani alitembelea TChad mwezi Aprili 2014, Ziara hii Imeshuhudia kutia saini mkataba katika shamba la kilimo.

 

kubadilishana biashara

Mafuta ya petroli: Pande mbili zilikubaliana kuratibu ziara ya kazi kwa wataalamu wa Misri ili kutathmini mahitaji upande wa TChad na kuandaa kozi za mafunzo ili kukuza uwezo wa rasilimali za watu wa TChad wanaofanya kazi katika sekta ya Mafuta ya petroli.

 

  • Utalii "Pande mbili Ziliamua kuharakisha katika utafiti wa mradi kwa ajili ya Ushirikiano katika uwanja wa utalii uliotolewa na TChad.

Biashara: Upande wa Misri ulimpa mshirika wake TChad rasimu ya mkataba wa maelewano juu ya ushiriki wa nchi hizo mbili katika maonesho na masoko ya kimataifa.

Mkandarasi wa Kiarabu: Kampuni ya Mkandarasi wa kiarabu ina nafasi  kubwa nchini TChad.

 

Mahusiano ya kitamaduni na elimu

 

TChad Inazigatiwa kama ni nchi kubwa zaidi ya Afrika kwa upande wa  idadi ya wajumbe wa Al-Azhar Sharif (wajumbe 40), ni msimamizi wa elimu, Pia Al-Azhar Sharif inatoa nafasi za elimu katika ngazi ya sekondari na Chuo Kikuu, Pia TChad inapata idadi ya nafasi kadhaa katika uwanja wa elimu ya juu.

Maprofesa watatu kutoka Vyuo VIkuu vya Misri walichaguliwa kufanya kazi nchini TChad ili kusaidia taasisi za elimu na hii ni kutokana na  ombi la Wizara ya Elimu ya Juu ya TChad.

 

Kutoka: Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri