
Historia
Misri na DJibouti zina mahusiano imara ya kihistoria na ya kimkakati,wakati ambapo Misri inazingatiwa kuwa ni moja ya nchi za kwanza ambazo zilifanya mahusiano ya kidiplomasia pamoja na kufungua ubalozi wake nchini DJibouti baada ya kupata uhuru katika mwaka 1977, Misri pia ilifanya haraka kwa ajili ya kuyakaribisha makubaliano ya kisiasa yaliyosainiwa kati ya serikali pamoja na umoja wa vyama vya upinzani nchini DJibouti kwa ajili ya kumaliza mgogoro wa kisiasa, kwa upande mwingine Djibouti imeiunga mkono Misri katika vikao vya Kimataifa, ambayo hivi karibuni ilikuwa kupiga kura dhidi ya azimio la baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika kwa kusimamisha ushiriki wa Misri katika shughuli za umoja wa Afrika baada ya mapinduzi ya Juni 30. Na jambo ambalo linayaimarisha mahusiano imara kati ya pande mbili ni eneo la kimkakati la Jibouti katika lango kuu la Bahari ya Shamu karibu na Ghuba ya Adeni na mlango wa Bab El-Mandab kusini mwa lango la Mfereji wa Suez. Na unaozingatiwa kuwa ni moja ya mihimili mikuu ya usalama wa taifa la Misri pia Djibouti inazingatiwa kuwa ni mlango muhimu wa eneo la pembe ya Afrika na Afrika mashariki kwani ina miundombinu pamoja na bandari ya kisasa.
Mahusiano ya kisiasa
Ziara iliyo muhimu ya Rais wa Djibouti, Mhe. Esmail Omar Gila nchini Misri katika mwezi wa Desemba mwaka 2016 imeonesha mahusiano imara kati ya nchi mbili, ambapo amefanya mazungumzo ya kina ya pande mbili pamoja na Rais Abdal Fatah El-Sisi ambayo yameshughulikia njia za kuimarisha pande mbalimbali za mahusiano ya pande mbili kutokana na ushiriki wa Mawaziri wahusika kutoka pande mbili. Kama walivyojadiliana baadhi ya maswala ya pamoja ya Kikanda na Kimataifa, kama walivyozungumzia pia hali ya mambo katika eneo la pembe ya kiafrika na Yemen na hali ya usalama na amani barani Afrika na changamoto ambazo Afrika inakabiliana nazo kutokana na migogoro kadhaa barani Afrika pamoja na ongezeko la tishio la ugaidi. Vile vile Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Djibouti Mahamoud Ali Yussuf alitembelea Misri tarehe 8 ya mwezi wa Novemba mwaka 2017, na katika ziara yake hiyo amekutana na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Misri Sameh Shukri, ambapo walifanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya pande mbili kati ya nchi mbili na maswala ya eneo la pembe ya Afrika na kuanzisha utaratibu wa mashauriano ya kisiasa ya mara kwa mara kati ya nchi mbili kwa upande wa Mawaziri wa Mambo ya Kigeni.
Mahusiano ya kiuchumi
Licha ya kuwepo kwa mahusiano imara kati ya Misri na Djibouti isipokuwa kiwango cha kubadilishana biashara kati ya nchi mbili hakivuki dola za kimarekani milioni 30 kila mwaka hazioneshi nguvu za mahusiano imara kati ya nchi mbili, licha ya ziara ya Rais wa Djibouti nchini Misri katika Desemba mwaka 2016 iliyoshuhudia utilianaji saini mikataba kadhaa na hati za mashirikiano muhimu katika nyanja mbalimbali ambazo zilijumuisha :
Hati ya makubaliano ya kusafirisha na kuagiza na kuvuka mifugo na nyama , na hati ya makubaliano ya uwanja wa elimu ya kiufundi, na hati ya makubaliano ya mashirikiano ya uwanja wa ushiriki wa maonesho na masoko ya kimataifa ,na hati ya makubaliano ya uwanja wa mashirikiano ya kibiashara na mikataba ya mashirikiano ya kiuchumi na ya kiufundi kati ya nchi mbili, na hati ya makubaliano ya uwanja wa afya na madawa pamoja na hati ya makubaliano kati ya mamlaka ya Mfereji wa Suez na Mamlaka ya Bandari za Djibouti. Pia Nchi mbili zina makubaliano ya mashirikiano ya pamoja, na hati za makubaliano katika Nyanja mbalimbali. Na idadi yake inakadiriwa kwa mikataba na hati za makubaliano 33, Pia tume ya pamoja ya mashirikiano ya kiuchumi na ya kiufundi ya nchi mbili imefanya vikao kadhaa, kupatikana wawekezaji wa kimisri nchini Djibouti kutoka Makampuni mawili ya Umoja wa Wahandisi na ambao kwa sasa wanafanya miradi mbalimbali katika uwanja wa ujenzi na Jumuiya ya Shoura ambayo imeweza kuanzisha benki ya Misri nchini Djibouti.
Mahusiano ya kiutamaduni
AL- Azhar Sharif na Vyuo Vikuu vya Misri vinatoa mchango muhimu katika kuimarisha mahusiano ya kiutamaduni kati ya nchi mbili, Na hayo ni kutokana na mapokezi ya Misri kwa nafasi za masomo za Djibouti, pia Misri inatoa fursa kadhaa za kutoa mafunzo kwa ajili ya wenye vipaji wa Djibouti katika nyanja mbalimbali, na hayo yanatimia kutokana na programu ya kutoa mafunzo inayotolewa na Shirika la Misri kwa ushirikiano wa maendeleo. Idadi ya wajumbe wa AL- Azhar Sharif kwa sasa inakadiriwa wajumbe 12 ukiongezea na nafasi za masomo zinazotolewa na AL- Azhar kwa ajili ya wanafunzi wa Djibouti, na ambayo idadi yake inakadiriwa nafasi15 kila mwaka na idadi ya wataalamu wa mfuko wa Misri wa ushirikiano wa kiufundi pamoja na Afrika nchini Djibouti inakadiriwa wataalamu 12 katika nyanja kadhaa. Na wizara ya elimu ya juu imekubali ombi la Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Djibouti kwakuongeza la idadi ya nafasi za Vyuo Vikuu na masomo ya Juu maalumu kwa Djibouti hadi kufikia nafasi15 ukiongezea na nafasi10 za masomo ya juu ili kufaika katika mwaka wa masomo, 2016 /2017.
Mahusiano ya Kijeshi
Hakika Misri inatoa mafunzo ya kiufundi na masomo ya kijeshi ndani ya vyuo vyake vya kijeshi kwa makanda wa kijeshi wa Djibouti katika nyanja mbalimbali. Ukiongezea na misaada ya Misri kwa DJibouti katika uwanja wa kupiga vita ugaidi na msimamo mkali kutokana na kuziboresha mbinu zinazotumika kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya mashirikiano ya kijeshi na ya usalama pamoja na kulinda eneo la bahari ya Shamu kutokana na vitisho vya ugaidi pamoja na uharamia wa kimataifa.