Misri na Eritrea
Jumanne, Februari 26, 2019
Misri na Eritrea


Utangulizi:

Misri ina mahusiano ya kihistoria na Eritrea. Misri ilikuwa na jukumu kubwa katika kuunga mkono mapinduzi ya Eritrea hadi kupata uhuru wa kitaifa wa Eritrea mwaka 1993. Na katika kipindi cha mapambano ya silaha, Misri ilibaki na mahusiano mazuri na vikundi vya mapinduzi ya Eritrea. Baada ya Eritrea kupata uhuru wake, Misri ilishiriki katika kupongeza  Azimio la Uhuru na kuweka  misingi imara kwa ajili ya maendeleo ya  baadaye na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote.

Mahusiano ya kisiasa

Misri ilikuwa na umuhimu kwenye suala la Eritrea miaka ya arubaini, karne iliyopita, na hayo yalifanya kuanzisha makao ya kupata uhuru wa Eritrea mjini Kairo,  Julai 1960. Baada ya  Eritrea kupata uhuru wake kutoka Ethiopia, Misri ilikaribisha kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia  kati ya nchi hizo mbili ili kuwa kama kituo halali kati ya Kairo na Asmara. Udiplomasia wa Misri ulikuwa na jukumu kubwa wakati wa vita vya mipaka vilivyo endelea kwa miaka miwili kati ya Eritrea na Ethiopia (1998-2000), ambapo Misri ilifanya juhudi ili kuhakikisha  amani kati ya pande hizo mbili. Tangu uhuru wa Eritrea, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ametembelea Misri mara 16,

hivi karibuni ulikuwa mkutano wake nchini Misri na Rais Abdel Fattah El Sisi Novemba 2016. Pande hizo mbili zilijadili njia za kuimarisha mahusiano  kati ya nchi hizo mbili katika Nyanja za kisiasa na kiuchumi,pamoja na  maendeleo  ya hali katika Pembe ya Afrika Na njia za kupambana  ugaidi na uhalifu.


Ziara za pamoja

Nchi hizo mbili zina zinatembelea ili kujadili mahusiano kati ya nchi hizo mbili  na maswala muhimu ya ushirikiano wa  pamoja, na  hasa ziara:
                                                
Septemba 13, 2018, Waziri wa Mambo ya Nje Sameh shoukri alizuru Asmara ili kufikisha ujumbe wa mdomo kutoka kwa Rais Abdel Fattah El Sisi kwa Rais wa Eritrea Isaias Afwerki, kwa lengo la kutoa ushawishi mpya kwa mahusiano maalumu na ya karibu kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote. Pia kujadili maswala kadhaa ya kikanda yenye umuhimu wa pamoja.

Januari 9, 2018, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki alitembelea Kairo, ambapo alikutana na Rais Abdel Fattah Al Sisi ili kujadili maendeleo ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili, na maendeleo mapya ya hali katika nchi za Bonde la Mto wa Nile na eneo la Pembe ya Afrika na maendeleo ya maswala ya pamoja ya kikanda na kimataifa.                                             

Mai 6, 2017, Waziri wa Mambo ya Nje ya Eritrea Othman Salih na Mshauri wa Rais wa Eritrea  Bwana: Yemeni Jabr Ab walizuru Misri, Walikaribishwa na Bwana: Sameh Shukri Waziri wa Mambo ya Nje. Walijadili njia za kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali na kufuatilia mipango ya ushirikiano iliyopo, kulingana na mahusiano mazuri ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili.

 Machi 19, 2017, ujumbe wa Eritrea wa kiwango cha juu unaojumuisha Waziri wa Mambo ya Nje Othman Salih na washauri wa kisiasa na kiuchumi wa Rais wa Eritrea, kwa kufuatana na, Yamaniy Jabr Ab na Hagos Jabr hweet, walitembelea Misri, waliokaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shukri. Pande mbili zilijadiliana ushirikiano wa nchi mbili na masuala ya kikanda yenye wasiwasi wa pamoja, hasa usalama wa kanda ya Bahari ya Shamu  na maendeleo ya hali katika Yemen, Somalia na Sudani kusini, pamoja na uratibu kati ya nchi hizo mbili katika vikao vya kimataifa, pamoja na msimamo  wa Eritrea juu ya vikwazo vilivyowekwa kwa Baraza la Usalama.                                                                                    

 


Novemba 29, 2016, Rais wa Misri Abdel fattah El Sisi alimkaribisha Rais wa Eritrea Bwana: Isaias Afwerki  Mjini kairo, ambapo walijadili njia za kuendeleza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili na maendeleo ya hali barani Afrika na eneo la pembe ya Afrika                                                                       

Mai 7,2015, waziri wa mambo ya nje Bwana: Sameh Shoukri alizuru Eritrea, ambapo alikutana na waziri wa mambo ya Nje ya Eritrea Bwana: Othman Saleh na Mshauri wa hali ya kisiasa wa rais Aforky Bwana: Yemani Gabr Ap. Na katika mkutano huu walizungumzia pande zote za mahusiano kati ya nchi ndugu hizo mbili na njia za kuongeza maendeleo ya mahusiano haya, licha ya kuzungumzia maswalaa muhimu kadhaa ya kikanda, hasa mgogoro wa Yeman na usalama wa eneo la bahari ya Shamu na ushirikiano wa pamoja katika nyanja ya kupambana na ugaidi na hali katika pembe ya kiafrika na maendeleo ya hali katika eneo la Mashariki ya Kati.
                                                                                      
Septemba 9,2014, Rais wa Eritrea Asiass Aforky alizuru Misri akiongoza ujume uliojumuisha Bwana: Othman Saleh waziri wa mambo ya Nje,  Bwana: Yemani Gabr mshauri wa Rais wa Eritrea, balozi wa Eritrea mjini Kairo na Bwana  Hassan katibu wa taarifa ya Rais wa Eritrea, ambapo walizungumzia maendeleo ya hali barani Afrika hasa inayohusiana na kupambana na  ugaidi, msimamo  mkali na uharamia, ambapo maoni ya Marais hawa wawili EL Sisi na Isaias Afwerki walikubaliana juu ya kuimarisha ushirikiano na utaratibu kati ya nchi za Afrika ili kuhakikisha amani, usalama na utulivu barani Afrika.