Misri na Ethiopia
Jumanne, 19 Februari 2019
Misri na Ethiopia

Vipengele viwili vimeunda mahusiano kati ya Misri na Ethiopia na uhusiano kati ya wananchi wa nchi mbili.. Vipengele hivi viwili ni historia na jiografia.
Kwa kihistoria, ushirikiano na mawasiliano kati ya wananchi wa nchi mbili unarejea  tangu kale. Kila moja ina wananchi wenye ustaarabu wa kina..Kisha mwelekeo wa kidini uliimarisha mahusiano haya ambapo Kanisa la Ethiopia limeunganishwa na Kanisa la Misri la Wakopti tangu karne ya nne baada ya kuzaliwa Nabii Isa. Baada ya hayo, Waislamu huko Misri na ulimwengu wote wa Kiislamu wamehifadhi nafasi ya watu wa Ethiopia katika kulinda Uislamu mwanzoni , ambapo Mfalme wa Abyssinia aliwakaribisha wahamiaji  Waislamu  wa kwanza.

Na katika zama za kisasa, nchi hizo mbili zimekuwa na nafasi kubwa katika uongozi wa shughuli za pamoja za kiafrika. Sio jambo la kubahatisha kwamba  Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) limeshiriki katika mapambano kwa nguvu pamoja na Misri , na Makao Makuu yake ni mjini Addis Ababa.

Na kwa upande wa jiografia, nchi hizo mbili zimeunganishwa na dhamana yenye nguvu zaidi.. Mto wa Nile ni chanzo cha maji, maisha na ustaarabu nchini Misri.. Sehemu kubwa ya maji yake hutoka kwenye uwanda wa Ethiopia kupitia Nile ya Buluu.

Katika miaka minne iliyopita, kumekuwa na mawasiliano makubwa ya kidiplomasia kupitia ziara za urais, kwani Addis Ababa ulikuwa mji mkuu wa Kiafrika ambao ulitembelewa zaidi na Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Kuhusu suala la bwawa la maendeleo la Ethiopia , misingi ya kushughulika nayo iliwekwa kupitia azimio la kanuni kati ya Misri, Ethiopia na Sudan mwaka 2015. Uratibu wa kidiplomasia kati ya nchi hizi tatu unaendelea kupitia mikutano ya Kilele na kisha kamati yenye majumbe tisa, ambayo inajumuisha mawaziri wa kigeni na umwagiliaji na viongozi wa Huduma za upelelezi katika nchi tatu.

Kubadilisha biashara kati ya nchi hizo mbili imeongezeka hadi dola bilioni moja mwaka 2017. Na aidha uwekezaji wa Misri nchini Ethiopia umeongezeka hasa katika uwanja wa mitandao ya umeme na maji.

Ziara za Rais El-Sisi nchini Ethiopia kutoka Juni 2014 na mpaka Februari 2019

Ethiopia imechukua nafasi ya kwanza kwa ziara ya Rais El-Sisi kwa nchi za Afrika zisizo za Kiarabu kwa ziara (5) zimefanyika kati ya ziara za nchi mbili, au kwa kushiriki katika mikutano ya mara kwa mara ya Kilele cha Umoja wa Afrika .. Kwa kuendelea katika kipindi cha miaka minne ya kipindi cha kwanza cha urais kuanzia Januari 2015 ili  Kushiriki katika Kilele cha nne cha Umoja wa Kiafrika na hivi karibuni katika Januari 2018 ili kushiriki katika Kilele cha 32 cha Umoja wa Kiafrika .
Mfululizo wake ni kama ifuatavyo :

Ziara ya kwanza tarehe 29/30 Januari 2015 kama Rais wa ujumbe wa Misri unaoshiriki katika shughuli za Kilele cha 24 cha Kiafrika na kilichoendelea kwa siku mbili chini ya anuani "2015: mwaka wa Uwezeshaji wa Wanawake na Maendeleo kuelekea Ajenda ya Afrika 2063

Ziara ya pili tarehe 23/24 Machi 2015 kama ziara ya nchi mbili zimekuja baada ya ziara ya Sudan na kusainiwa kwa Mkataba juu ya Azimio la kanuni za bwawa la Maendeleo  huko Khartoum mwezi Machi 2015

Ziara ya tatu iliyofanyika tarehe 30 Januari 2016 ili kuongoza ujumbe wa Misri kwenye shughuli za Kilele cha 26 cha Kiafrika huko Addis Ababa.

Ziara ya nne tarehe 30/31 Januari 2017 ili kuongoza ujumbe wa Misri katika kazi za "Kilele cha28 cha Kiafrika" mjini Addis Ababa .. na katika wakati huo El-Sisi aliiongoza Kamati ya Marais wa Afrika inayoshughulikia Mabadiliko ya Hali ya Hewa. .

Ziara ya tano tarehe 27/29 Januari 2018 ili kuongoza ujumbe wa Misri katika "Kilele cha 30 cha Kiafrika" huko Addis Ababa, ambapo El-Sisi alikuwa kiongozi wa Kilele cha Baraza la Usalama na Amani ya Kiafrika.