Misri na Ghana
Jumapili, Machi 24, 2019
Misri na Ghana

 

Kwanza: Utangulizi

     Misri na Ghana wana mahusiano ya kihistoria yaliyo thabiti tangu miaka ya hamsini karne iliyopita wakati wa uhuru wa Ghana kutoka kwa Uingereza mwaka 1957.  Ambapo Misri iliipa umuhimu zaidi Ghana, hasa tangu wakati wa zama za Rais Nkrumah  na msimamo wa Misri ambao umemsaidia wakati huo. Ni muhimu kutambua kwamba Rais wa kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah, ambaye aliongoza nchi yake kuelekea uhuru, alioa mwanamke Misri, Fatheya Nkrumah. Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza zilizo na mahusiano mazuri ya kidiplomasia na Ghana. Nkrumah alikuwa rafiki wa karibu wa Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser.                                                                                         

     Baadhi ya watu wanafikiri kuwa mahusiano ya Misri na Ghana yanarejea miaka ya hamsini  ya karne iliyopita. Mwanzo wa harakati za ukombozi katika bara, lakini ukweli ni kuwa yalianza kabla ya hapo, tangu nyuma ya karne za Kati wakati kulikuwa na falme za Afrika kama vile Ufalme wa Ghana, ambao alisilimu na ulihusisha mahusiano ya kibiashara na kitamaduni na nchi za Kiislamu zikiongozwa na Misri, wananchi wa Ghana wanamahusiano  na Misri zaidi tangu kiongozi wao Kwame Nkrumah, Rais wa kwanza wa Ghana baada ya uhuru, aliamua kuoa  Mchumba wa Nile "Fathiya" kama walivyokuwa wakimwita "fatia" kwa maana mwanamke mzuri, wananchi wa Ghana walimshangaa  na kusema kuwa Nkrumah alikwenda Misri na amelirudi na Mchumba wa Nile, ingawa miaka mingi imepita tangukufariki Fathia na mume wake Nkrumah, lakini wananchi wa Ghana bado wanamkumbuka  na wanasimulia juu ya "Fatheya",na kama alivyoipenda Ghana, wananchi pia walionesha hisia za upendo wao, na Fathiya alizoea kusaidia masikini na kutunza watoto yatima, jambo ambalo ilimfanya yeye kuwa karibu na mioyo ya wananchi wa Ghana, hawakumsahau Fathia kuwa alikuwa Mmisri, baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1967, alichangia kwa mapambo yake kupitia  benki ya kairo ili kusaidia mapambano ya  vita

Gamal Nkrumah, mtoto wa kwanza wa kiongozi Kwame Nkrumah, anakumbuka kwamba wakati wa mapinduzi  Alfajiri mama yake alihitaji msaada kutoka  Abd Al-Nasir, na alimhakikishia na  alituma ndege ya binafsi mjini Akra ili kutuleta kairo na tuliishi katika jumba la Tahra kwa miezi mitatu mpaka kukamilika kwa nyumba yetu sehemu ya Maadi. Jamal, ambaye aliitwa kwa jina la kiongozi Abdel Nasser, alieleza kwamba Nasser alikuwa rafiki wa baba yake, na bila yeye, Familia ya Fatheya isingekubali juu ya ndoa hii, na Nasser alimwambia  bibi yangu, "Unaogopa nini?, Binti yake ataolewa na Kiongozi  mkubwa wa Afrika, Nitafungua Ubalozi wa Misri nchini Ghana pamoja na safari ya ndege ya moja kwa moja na unaweza kumtembelea binti yako wakati wowote" na Jamal inaendelea, mama yangu alisafiri Ghana na bibi yangu alitutembelea hata baada ya baba yangu kufariki mwaka 1972, mama yangu alijali kutuunganisha na nchi ya baba yetu na tulirudi nchini Ghana na ndugu zangu wanaishi huko . Nilimaliza masomo yangu nchini London na ninaishi nchini  Misri.                                                          

Mahusiano ya Misri na Ghana yanajulikana kwa kina cha historia na kuheshimiana wakati wa msaada wa Misri katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Misri hutoa misaada mingi na kozi  nyingi kwa Wakuu wa Ghana katika nyanja za afya, usalama, vyombo vya habari na utalii, ambayo yamekuwa na athari kubwa katika kuendeleza uwezo wa kiufundi wa Wakuu wa Ghana katika nyanja mbalimbali, Ambazo zimenufaisha jamii ya Ghana wakati wa majaribio yake katika maendeleo kwa ujumla.                                                                                         

Uhusiano wa Kiuchumi na Maendeleo kati ya nchi hizo mbili:              

Waziri wawili walikutana tarehe 5/12/2017 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari " Yasser Al-kadhi"  na Waziri wa Mawasiliano wa Ghana "Yursula Awasu Afukul"  na kusaini mkataba wa maelewano ili kuimarisha  njia za ushirikiano wa nchi mbili katika mawasiliano na teknolojia ya habari, na kuendeleza na kusaidia fursa za mafunzo, kupanga sera, utafiti, uvumbuzi na ujasiriamali ambao unafikia maslaha  katika sekta ya umma na binafsi, na muda wa kufanya kazi katika mkataba ni miaka miwili ambao unajumuisha  Nyanja za ushirikiano kati ya Wizara mbili katika kupanga na kujenga  maeneo ya kiteknolojia nchini Ghana, uhamisho wa ujuzi wa Misri kwa upande wa Ghana katika uwanja wa matumizi  ya Teknolojia na serikali, miundombinu na vituo vya habari, usalama wa habari, uvumbuzi na ujasiriamali, na kuhifadhi urithi wa utamaduni na wa asili wa Ghana.                                            

Mahusiano kati ya Misri na Ghana yanaendeleza hasa katika Nyanja za kiuchumi na maendeleo, nchi hizo mbili zinajaribu kupata faida kutokanana na uwezo, ujuzi na uwezekano wa kila nchi kusukuma mchakato wa maendeleo katika  nchi zao, uwepo wa kiuchumi wa Misri katika Ghana ulianza karibu miaka 30 iliyopita, wakati mfanyabiashara wa Misri, Medhat Khalil, alianzisha kampuni kubwa ya aluminium nchini Ghana, na sasa kampuni hii ni muhimu zaidi katika uwanja huu katika Afrika Magharibi na imekuwa maarufu. Kampuni ya Nasr kwa kuagiza na kuuza imefanya  katika uwanja wa kuuza nje kakao na mbao za Ghana tangu miaka ya hamsini ya karne iliyopita. Licha ya uwepo wa kampuni za mawasiliano ya misri "Alkan", "AG Bro" na kampuni ya "The Arab Contractors" ambayo inajenga miradi mikubwa juu ya ziwa la "Fulta" nchini Ghana, na kampuni ya "United Engineers" ambayo inafanya kazi ya ujenzi katika mji Mkuu "Akra".                                                         

Ziara muhimu na ushirikiano kati ya Misri na Ghana:                             

Jumatatu, Septemba 18, 2017, Rais Abdelfattah Sisi alikutana na Rais wa Ghana Nana Akufo Addo pembeni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York,  Rais alielezea umuhimu wa kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote na kufanya kazi ili kuongeza madiliko  ya kibiashara ikiwa ni pamoja na kunafikia  kiwango cha mahusiano ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili, ambayo alidokeza  uwekezaji wa Misri katika sekta nyingi nchini Ghana. Kwa upande wake, Rais wa Ghana alionesha fahari ya nchi yake katika uhusiano wake wa kihistoria na Misri, akisisitiza nia yake ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote, licha ya kuongeza uwekezaji wa Misri huko, na  alitoa shukrani zake kuhusu  msaada wa kiufundi wa Misri kwa wananchi  wa Ghana katika nyanja za kujenga uwezo, akielezea nia ya nchi yake kufaidika kutokana na uzoefu wa Misri katika uwanja wa usalama na kupambana na ugaidi.                                

Tarehe 11/5/2017, Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shoukri alitembelea Ghana, ambayo Rais wa Ghana Nana Akufo Addo alimpokea,  Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuimarisha mahusiano ya nchi zote katika nyanja zote. Shoukri alimpa Rais wa Ghana ujumbe kutoka na Rais Al-Sisi ambao unajumuisha heshima na fari juu ya Misri kuendeleza mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili na njia za kuyaendeleza katika nyanja zote, pamoja na kumwalika Rais wa Ghana kutembelea Misri haraka  iwezekanavyo.                                                                                      

Tarehe 9/1/2017, Mjumbe wa Rais wa Ghana, James Victor Djebbou, na wajumbe ambaye waliandamana naye kutembelea Misri, Rais Abdel Fattah Al-Sisi alikutana nao. Pande hizo mbili zilijadili masuala ya Mkutano wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa mnamo Januari 2017, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa Tume ya Umoja wa Mataifa.                

Tarehe 7/1/2017, Mhandisi/ Ibrahim Mahlb, msaidizi wa Rais kwa miradi wa taifa, alitembelea Ghana, kuwakilisha Misri katika sherehe ya Rais mpya "Nana Akufo Addo",  Rais waGhana aliwapokea  na pande hizo mbili zilijadili masuala ya kikanda yenye maslahi kati yao na njia za kuimarisha ushirikiano na uratibu kati ya nchi mbili katika vikao vya kikanda na kimataifa.                                                                              

 

Tarehe 11/7/2016, wajumbe wa ngazi ya juu kutoka "Gesi Misri" iliyoongozwa na M. Mohamed Ebrahim, Mkurugenzi wa Mtendaji wa kampuni hiyo walitembelea Ghana, ambapo alitembelea mashamba na vituo vya uzalishaji na kusukuma gesi asilia ili kuona miundombinu ya sekta ya gesi asili nchini Ghana, Wajumbe walihudhuria mikutano mingi na Rais na maafisa wa kampuni hiyo "Gesi ya Ghana" na Tume ya mafuta ya Ghana, pande mbili zilikubaliana kubadilishana ziara  na kuendelea kujadili wakati ujao ili kupanga kuhusu ushirikiano na nyanja zote,  viashiria vya awali vinathibitisha uwepo wa fursa nakuahidi ushirikiano kutokana na ujuzi wa muda mrefu wa kampuni ya misri,  upande wa Ghana ulionesha nia ya kufikia ushirikiano wa kazi  na washiriki waaminifu na wenye uzoefu, kuimarisha  jitihada zake katika maendeleo ya sekta hii muhimu, ambayo ni moja ya nguzo za ukuaji wa uchumi nchini.                                                                                      

Ziara ya Waziri wa Uwekezaji kwa Ghana Februari 2010 kushiriki katika mkutano wa Uwekezaji wa Afrika na Misr iri iliomba serikali za nchi za Kiafrika kuchanganya uchumi na kuunga mkono uwekezaji na kuimarisha sheria za udhibiti zinazopanga sekta ya fedha ili kuunda kazi mpya na kukuza ukuaji na maendeleo zaidi katika Afrika                       

Ziara ya balozi msaidizi na Waziri wa Mambo ya Afrika na mambo ya Umoja wa Afrika alikwenda Ghana mnamo Oktoba 2010.                    

Ziara ya Waziri wa Uwekezaji kwa  Accra  kutoka 8 hadi 10 Februari 2010 ilikuwa kwa ajili kushiriki katika Baraza la Uwekezaji la Kiafrika.

Ziara ya Mheshimiwa John Evans Atta Mills, Rais wa Jamhuri ya Ghana, alikwenda Misri kushiriki katika Mkutano wa NAM kipindi cha  15-16 Julai 2009 huko Sharm El Sheikh.                                                        

Ziara ya John Mahama, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Ghana, kwenda Misri kushiriki katika Mkutano wa Maziri wa Nne wa Baraza la China-Afrika kipindi cha 8 hadi 9 Novemba 2009                                          

Ziara ya Rais wa zamani wa Ghana John Kufuor alikuja kushiriki Mkutano wa Umoja wa Afrika kutoka Juni 30 hadi 1 Julai 2008 huko Sharm El Sheikh.                                                                                 

Ziara ya Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa kwa  Accra wakati wa 2-4 Septemba 2008 ili kushiriki katika mkutano wa juu ya ngazi ya kiuchumi  ili kuthibitisha misaada ya kigeni.                                                          

Ziara ya Rais wa zamani Mubarak kwa Accra kushiriki katika Mkutano wa Umoja wa Afrika mnamo 1 Julai 2007                                             

 Ziara ya Rais wa zamani John Kufuor kwa Cairo tarehe 27-29 Mei 200

Ziara ya Rais wa zamani  Mubarak kwenda Ghana mwezi Julai 2007, wakati ambapo alishiriki katika Mkutano wa tisa wa Mkutano wa Umoja wa Afrika, ambao ulikuwa pamoja  na sherehe za uhuru wa Ghana tangu miaka 50.                                                                                             

Ziara ya Rais wa Ghana, John Kufuor, kwenda  Misri  mwezi Mei 2007. Mazungumzo yao  yalishughulika na masuala kadhaa, muhimu zaidi ni kupanua na kuimarisha mahusiano kati ya nchi ya Misri na Ghana katika nyanja mbalimbali, walichangia maoni kuhusu masuala ya uwanja wa Afrika, hasa maendeleo katika Pembe ya Afrika, Darfur na Somalia, na njia za kazi ya kiafrika.