Misri na Guinea ya Ikweta
Jumapili, Januari 06, 2019
Misri na Guinea ya Ikweta

Mahusiano ya pamoja

1-Tarehe 8/11/2017 Waziri Mkuu wa Guine ya Ikweta Fransisko Paskal
Obama Alifanya ziara Nchini Misri ili kushiriki katika kongamano la vijana
la Kimataifa, na katika ziara hiyo pembezoni mwa kongamano hilo alikutana
pamoja na Waziri Mkuu wa Misri Dk. Shirif Esmail, pande zote mbili
zilifanya majadiliano na kutafuta kumarisha ushirikiano wa pamoja kati ya
pande zote mbili.

2- Tarehe 13 /8/2017 Waziri wa Mambo ya nje wa Guinea ya Ikweta
Makali Kamara alifanya ziara nchini Misri na alipokelewa na Waziri wa
Mambo ya nje ya Misri Bw. Sameh Shokry, pande zote mbili walitafuta njia
za kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya nchi mbili, pia
walishauriana kuhusu utaratibu kati ya nchi mbili katika masuala ya
kimataifa .

3-Tarehe 20 /7/2015 Ujumbe wa Misri ulishiriki katika kongamano la
Kimataifa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa ya " EBOLA" ujumbe huu
uliongozwa na Waziri Mkuu aliyepita Mhandisi Dk. " Ibrahim Mehleb"
Ambaye Alikutana na Raisi wa" Guinea ya Ikweta" pembezoni mwa
kongamano hilo .

4- Tarehe13/3/2015 katika mfumo wa ushirikiano na Jamhuri ya Guinea ya
Ikweta nchini Misri kulifanyika kongamano la kuimarisha na kuboresha
uchumi wa Misri "Naibu Rais wa Jamhuri ya Guinea ya Ikweta "Ijinathyu
Milaam alihudhuria na alikutana na Rais wa Misri "Abd Alftaah Alsisi"
pembezoni mwa kongamano.

5-Tarehe 10 /12/2014 Rais wa Jamhuri ya Guinea Ya Ikweta Ubyang Njema

Alifanya ziara nchini Misri ambapo Alikutana na Rais Abd Alfatah Alsisi,
na walitafuta kwa pamoja fursa za uzalishaji na kutafuta njia za ushirikiano
wa pamoja hasa katika Nyanja za makazi, ujenzi na utengenezaji barabara
zaidi na kuangalia upya suala la mikataba na pia kuongezeza mikataba
mipya ili kuimarisha ushirikiano baina ya nchi mbili katika Nyanja zote.

6-Tarehe 8/5/2014 Waziri Mkuu wa Misri Mhandisi Dk." Ibrahim Mehleb"
Alifanya ziara nchini Guinea ya Ikweta ambapo alikamilisha makubaliano
na kutia saini mikataba ya ushirikiano katika upande wa Afya, Misri
itaanzisha kutokana na mkataba huu Chuo cha matibabu nchini Guine ya
Ikweta katika eneo lenye ukubwa wa kilomita 2000.

USHIRIKIANO KATIKA NYANJA ZOTE

Tareha 9/5/2014 Misri na Guinea ya Ikweta zimetia saini mikataba minne ya
ushirikiano ili kuimarisha mahusiano katika Nyanja mbalimbali za Kiu
chumi. kama ifuatayo:
1-katika Nyanja ya makazi
2-katika Nyanja ya Afya
3- katika Nyanja ya kilimo
4-kaika Nyanja ya petroli na madini