Misri na Kenya
Jumanne, Septemba 10, 2019
Misri na Kenya

Maendeleo ya mahusiano kati ya Misri na Jamhuri ya Kenya


Mahusiano kati ya Misri na Kenya yalianza kabla ya Kenya kupata uhuru wake ambapo wakati wa utawala wa Rais Gamal Abdel Nasser, Misri iliunga mkono harakati za "Mao mao" za Kenya kupitia kampeni ya vyombo vya habari na kidiplomasia dhidi ya ukoloni wa Uingereza kwa Kenya. Na Misri ilianzisha Kituo cha redio kwa jina la "Sauti ya Afrika" kilichotengwa kwa raia wa Kenya ili kuwaunga mkono katika mapambano yao kwa ajili ya kupata uhuru.na kituo cha redio hiki ni cha kwanza kwa lugha ya Kiswahili kutoka nchi za Afrika ili kuunga mkono Kenya kupata uhuru wake.

• Misri ilifanya suala la "Mao mao" kuwa suala la Kiafrika na ilifanya juhudi kubwa ili kuachiliwa huru kiongozi wa Kenya Jomo Kenyatta, aliyefungwa gerezeni na ukoloni wa Uingereza katika mwaka wa 1961. Kairo ilikuwa mji Mkuu wa kwanza unawapokea na kuwasaidia wapiganaji wa Kenya wanaongozwa na Eugenja Odinga, Tom Mboya, James Jeshoro, Joseph Morupi na wengine kama wanachama wa chama cha Umoja wa Kitaifa wa Kiafrika wa Kenya (KANU) na Chama cha Umoja wa Kidemokrasia wa Kenya (KADU). Vyama hivyo viwili vilifungua ofisi huko Kairo katika kipindi hiki, na matokeo ya juhudi za kimisri katika kuunga mkono mapambano ya Kenya ili Kenya ipata uhuru wake na ilipata uhuru wake mwaka wa 1963.


Mnamo 1964, Kenya ikawa jamhuri na ilianza mahusiano ya kidiplomasia na Misiri na kufungua ubalozi wake Mkoani Kairo. Wakati wa kupitishwa kwa nyaraka za balozi wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya huko Kairo, Rais Gamal Abd El-Nasser alionesha kufurahishwa kwake kwa mapambano ya raia wa Kenya kwa ajili ya kupata uhuru kwa uongozi wa " Jomo Kenyatta" ambaye ni Rais wa kwanza kwa Kenya baada ya uhuru. Abdel Nasser alionesha kuwa tayari kwa ushirikiano na Kenya na nchi zote za Afrika ili kuimarisha nguvu ya Afrika na kukuza rasilimali zake, na hivyo kuchangia kuimarisha umoja wake

Katika mwaka wa1964, Misri ilikaribisha Mkutano wa Kilele cha Pili wa kiafrika. Pembezoni mwa vikao vya mkutano huo, Rais Nasser alionesha kuwa tayari kwa ushirikiano wa kijeshi na Kenya na Rais Kenyatta alimjibu kwa kuelezea nia yake ya kuwaondoa wanajeshi wa Uingereza katika nchi yake, kwa hivyo Misri iliunga mkono Kenya katika kujenga Jeshi la Kitaifa la Kenya.


Na katika muktadhaa huu Rais Jomo Kenyatta alisema "Tutamkumbusha Nasser kwamba misaada yake kwa Afrika imeokoa nchi nyingi za kiafrika.".
Mnamo 1967, mradi wa "Hydromet" ulianzishwa kwa kushiriki Misiri na Kenya miongoni mwa nchi tano za Bonde la Mto wa Nile na baadaye nchi zingine nne zilijiunga kwa mradi huo. Mradi huo ulilenga kufanya utafiti wa hali ya hewa na maji kwa bonde la maziwa ya Tropiki, kuweka mipango ya maendeleo ya rasilimali ya maji na kufanya utafiti wa uwiano wa maji kwa Mto wa Nile.


Kenya ilikuwa miongoni mwa nchi zilizovunja mahusiano yake ya kidiplomasia na Israel baada ya vita vya Oktoba 1973, kiasi kwamba baraza la Mawaziri la shirikisho la nchi za Afrika lilofanyika katika mwezi wa Novemba 1973,walifanya uamuzi wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Israeal , na kuiomba kuondoka maeneo yaliyo chini ya uvamizi na kuwapa wananchi wa palestina haki ya kujiamulia mambo yake.
Katika mwezi wa Novemba mwaka wa 1984 , Rais wa zamani alifanya ziara nchini Kenya ikiwa ni miongoni mwa ziara za nchi za Afrika ,na kwamba alizuru Zaire ,Somalia na Tanzania ,aidha alionesha kwamba misri itakuwa daraja muhimu baina ya nchi za kiarabu na wananchi wa Afrika kama mpatanishi ili kutatua migogoro ya bara la Afrika.
Katika mwaka wa 1998 , Misri ilijiunga na mkataba wa COMESA ambao unajumuisha nchi za Afrika 22, Kenya ikiwa ni mojawapo ya nchi zilizo tia saini masharti ya mkataba wakati ulipofanyika mkutano wa Mawaziri katika mji mkuu wa Malawi mwaka wa 1995, COMESA kwa upande wa Misri inazingatia ni muhimu sana katika nyanja ya Kijiografia na kisiasa, kwa kuwa Misri ipo katika eneo bora la kijiografia na ipo karibu na ulimwengu wa kiarabu , eneo la pembe ya Afrika , na nchi za bonde la Mto Nile , ni kama mkanda unaoizunguka Misri.

Kukua mahusiano ya pande mbili

Misri imeendeleza ushirikiano wake na Kenya katika viwango vyote, na mahusiano ya urafiki wa kidugu kati ya nchi mbili ndugu Misri na Kenya undugu huu umetokea wakati wa shida, ni katika kupambana na majanga ya asili kama ukame na mafuriko, kwa kutoa vyakula , matibabu na misaada ya kiufundi kwa watu wa Kenya.
- Katika mfumo wa ushirikiano wa kimahakama na ushauriano kuhusu mifumo ya sheria, Jaji Mkuu wa Kenya, Johnson Evens Jibshiro, alitembelea Misri kutoka 1-3 Desemba 2008 ili kufahamu juu ya kazi ya Wizara ya Sheria ya Misri na mfumo wake wa kisheria na ilifanyika idadi kadhaa ya mikutano na wenzake katika Wizara ya Sheria ya Misiri.


Mnamo tarehe 17-18 Juni 2009, Kenneth Marinde, Spika wa Bunge la Kenya, alitembelea Misri ili kuhudhuria kikao cha pili cha Kongamano la Bunge la Nchi za Bonde la Mto wa Nile.
- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Kalonzo Masyuka aliongoza ujumbe kutoka nchi yake ili kushiriki katika shughuli za mkutano wa kilele wa nchi zisizopendelea upande wowote uliofanyika mjini Sharm El-Sheikh katikati ya Julai 2009, na alikutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Misri na akielezea kuthamini kwake uhusiano wa ndani wa nchi mbili, na alisisitiza azimio la Kenya kusukuma mbele mahusiano yale, hasa kuhusu kukuza viwango vya ubadilishanaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili.

Kupitia mkutano wa nne wa Mawaziri kwa ajili ya kusaidiana kati ya China na Afrika mkutano ambao ulioitishwa na Misri katika mji wa Sharmu Sheikh katika kipindi cha kuanzia 8-9 /11/2009, na mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Moses Witangola akiongozana na wajumbe kutoka katika mji wake, Witangola alikutana pembezoni mwa mkutano wa Mawaziri na Waziri wa Mambo ya nje wa Misri pale walipofanya mazungumzo kuhusiana na matukio mengi yenye umuhimu wa pamoja hasa kusaidiana katika nyanja ya kuendeleza vyanzo vya maji nchini Kenya, na uwezo wa Misri kuisaidia Kenya kwa ajili ya kukabiliana na kupungua kwa mvua na na kurejea kuiandaa misitu yenye mvuto wa mvua.
Na katika mwezi wa mei 2010 waziri mkuu wa Kenya Laila Odinga lifanya ziara ya kuelekea nchini Misri akasisitiza kupitia mkutano wake na wausika wa kimisri kwamba Kenya "haiwezekani ikafikiria au ikaelekea katika kuyadhuru masilahi ya Misri ya kimaji".

Katika April 2011 Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Rechard Unionka alifanya ziara ya Kairo kwa ajili ya kufanya mashauriano ya kisiasa pamoja na maofisa kadhaa nchini Misri.

Mahusiano ya kisiasa

Misri inafungamana na Kenya kupitia mshipa mmoja wa uhai nao ni Mto wa Nale, na historia ndefu inayotokana na kusaidiana katika ujenzi na zinashirikiana katika malengo na mielekeo, nchi mbili hizi zinafanya kazi ya kufikia maendeleo na utulivu wa kiuchumi kwa wananchi wake zikitegemea uwezo wake mkubwa na nafasi yake ya kimiundombinu iliyo ya kipekee, kwani Misri ipo katikati ya mabara matatu ya ulimwengu wa zamani na ikipakana na bahari mbili muhimu nazo ni bahari ya Shamu na bahari ya Meditereniani na huku ikipitiwa na mfereji wa Suez, ni mapitio muhimu ya bahari kwa kiwango cha kimataifa , na ina Ustaarabu wa kale na mahusiano mazuri na nchi zote za bara la Afrika, ama Kenya inajulikana kwa mipaka yake ya Mashariki inayopakana katika bahari ya Hindi ni jambo ambalo limeifanya kuwa ni mzunguko muhimu wa muunganiko wa kibiashara kati ya Mataifa ya Kiarabu na Mataifa ya bara la Afrika tokea karne nyingi, kama ilivyojiweka nafasi yake ya kijiografia ya kipekee kwa ajili ya kusimamia nafasi yake ya uongozi katika eneo la Afrika Mashariki na nje yake.

Mahusiano ya Misri na Kenya baada ya mwaka 2014

Mahusiano kati ya Misri na Kenya tokea mwaka 2014 yalishuhudia maendeleo mazuri na ukuaji wenye kuzingatiwa katika nyanja zote, hakika Misri ilipita njia mbili katika mahusiano yake na Kenya, njia ya kwanza ni mahusiano ya pade mbili na ziara za pande mbili ambazo zinalenga kusaidiana kati yao, ama njia ya pili inahusiana na kusaidiana katika sekta ya maji kwa kuzingatia kwamba ni nchi mbili muhimu miongoni mwa mjumuiko wa nchi za Bonde la Mto Nile.
Na katika mwaka 18/2/2017 Rais Abdulfattah Al-Sisi alifanya ziara rasmi nchini Kenya ziara ambayo ni ya kwanza ya aina yake kwa Rais wa Misri tokea miaka 33, na akakutana na Rais wa Kenya.Uhuru Kinyata, pale walipofanya kikao cha mazungumzo yanayohusu pande mbili kikifuatiwa na mkutano wa pamoja ukihudhuriwa na wajumbe wa nchi mbili, na Rais Kinyata alielezea furaha ya wananchi wa Kenya kwa kutembelewa na Rais Al-Sisi, akiashiria kwamba ziara hiyo imekuja kwa ajili ya kuyavisha taji mahusiao ya kipekee ambayo yanazifunga nchi mbili na mataifa mawili yaliyo ndugu, hali ya kuwa ni mwenye kujenga nafasi ya kihistoria ambayo inasimamiwa na Misri..Katika kuunga mkono harakati za kupigania uhuru katika mataifa mbali mbali ya kiafrika, huku akitilia msisitizo kwamba ziara hiyo inaashiria kutilia umuhimu Misri mahusiano yake na mataifa ya kiafrika, na akisisitiza kurudi kwake kwa mara nyingine katika nafasi yake ya asili ya uongozi katika bara.

Kwa upande wake, Rais Al-Sisi alisisitiza lengo la Misri katika kuuendeleza uhusiano wake na Kenya katika nyanja zote, na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuhakikisha maslahi ya nchi mbili yanapatikana, na Rais Al-Sisi alitoa mualiko rasmi kwa Rais wa Kenya kuitembelea Misri kwa ajili ya kuuendeleza ushauriano na ushirikiano kati ya pande mbili.
Pande hizo mbili zilijadiliana njia za kuongeza mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi mbili, Marais hao wawili walisisitiza umuhimu wa kuzidi kusaidiana hasa kupitia uwanachama wa nchi mbili katika soko la pamoja la Mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA), na katika mfumo huu, Marais wawili walijadili njia za kuongeza kubadilishana biashara, pia walijadili matokeo ya mkutano wa kwanza wa Balaza la Biashara la Misri na Kenya ambalo lilifanyika Nairobi, na yakatimia kupitia mkutano huo makubaliano ya kuongeza kubadilishana biashara kufikia dola bilioni moja kwa muda wa miaka miwili kupitia miradi kadhaa ya pamoja katika nyanja mbalimbali.

Marais hao wawili walikubaliana kufanya mikutano ya kikao cha saba cha kamati ya pamoja chini ya uenyekiti wa mawaziri wawili wa mambo ya nje mwaka 2017, pamoja na maandalizi mazuri ili kusababisha kuunga mkono na maendeleo ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbali mbali. Marais hao wawili pia walisisitiza umuhimu wa kuamsha mikataba iliyosainiwa hapo awali kati ya pande hizo mbili, na kufanya mikataba mipya, hasa katika uwanja wa kuzuia ushuru mara mbili na kulinda uwekezaji, kwa lengo la kutoa hali ya hewa inayofaa ili kuongeza ushirikiano katika nyanja za uchumi na uwekezaji, na Rais Kenyatta alisifu misaada ya kiufundi iliyotolewa na Misri ili kusaidia na kujenga uwezo wa Wakenya katika nyanja mbali mbali, pamoja na mchango wake mzuri Katika miradi kadhaa ya maendeleo katika nyanja za afya, kilimo na umwagiliaji.
Katika suala hili, Rais Al-Sisi alisisitiza hamu ya Misri ya kuendelea kutoa msaada wa kiufundi ili kujenga uwezo na mafunzo nchini Kenya, akikaribisha ombi la upande wa Kenya; Misiri inatoa vifaa vya matibabu na madaktari katika hospitali ya kijeshi inayojengwa hivi sasa katika mji mkuu wa Nairobi, ambapo Rais aliamua kutuma ujumbe wa wataalamu ili kutembelea hospitali na kufahamu mahitaji yake haraka iwezekanavyo.

Mazungumzo hayo pia yaligusia maswala mbali mbali ya kikanda yenye masilahi ya pamoja, hasa kuhusu maendeleo ya hali nchini kusini mwa Sudan na Somalia. Marais hao wawili walisisitiza hitaji la kuendelea uratibu kati yao ili kufanya kazi kwa lengo la kufikia amani na utulivu katika eneo hilo. Rais al-Sisi alisisitiza kwamba Misri iko tayari kwa kuendelea mashauriano pamoja na upande wa Kenya ili kuimarisha utulivu na kufanikisha amani na usalama barani Afrika kwa ujumla, na uratibu katika maswala tofauti ya kikanda na ya kimataifa.

Marais wawili pia walijadili maswala kadhaa ya Umoja wa Mataifa "UN" , ambapo waliafikiana kimaoni na kukubaliana kuendelea na taratibu za mchakato wa marekebisho ya shirika la kimataifa .. Rais wa Kenya pia aliomba msaada wa Misri katika kuendelea kukaribisha Nairobi Makao Makuu ya Mashirika kadhaa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa
Mwishoni mwa ziara yake Nairobi, Rais Al-Sisi alifanya ziara kwa Kituo cha Umoja wa Mataifa barani Afrika, ambapo alisikiliza maelezo ya sehemu muhimu zaidi za Kituo hicho, ambacho kinajumuisha Makao Makuu kadhaa ya mashirika ya kimataifa kama vile Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa UN (UNEP) na Programu ya Umoja wa Makazi ya Wananchi (Habitat),pamoja na makao ya kikanda kwa mashirika kadhaa kama vile Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO).


 Ushirikiano katika uwanja wa kupambana na ugaidi


Misri inasisitiza katika vikao vyote vya kimataifa umuhimu wa kupambana na ufadhili wa ugaidi kwa ufanisi na kuzuia vyanzo vya usajili, kubeba silaha, kuunga mkono na kuwakumbatia kisiasa, pamoja na hitajio la kuunga mkono nchi za Kiafrika zinazokabiliana na ugaidi na kuzisaidia katika juhudi zake za kuuondoa, na mshikamano na waathirika waliopotelewa na watu wao na vikosi vya utekelezaji wa sheria na raia. . Na umuhimu wa kupitisha mtazamo kamili wa kukabiliana na ugaidi ambao unajumuisha kukomesha na sababu za ugaidi na itikadi kali, ikiwa ni pamoja na kupitia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Ushirikiano wa usalama kati ya Misri na Kenya katika mapambano dhidi ya ugaidi na msimamo mkali ni mojawapo ya nyanja muhimu zaidi za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kwani nchi hizo mbili zinakabiliwa na changamoto kama hizo kwa sababu ya mashambulio ya kigaidi kwenye maeneo ya kijeshi na ya kiraia kutoka makundi ya kigaidi yenye itikadi kali , mengi katika hayo ni makundi yaliyo vuka mipaka yamechochewa na itikadi kali na kutafsiri vibaya Uislamu, ambapo Kenya inateseka kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea mara kwa mara na vikundi vya watu wenye msimamo mkali.
Wakati wa mazungumzo yao mnamo Februari 2017, Rais Abdul Fattah Al-Sisi na Rais wa Kenya walisisitiza umuhimu wa kuamsha ushirikiano wa usalama kati ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia vita vya pamoja vya nchi hizo mbili dhidi ya ugaidi, na changamoto zinazokumbana nazo kutokana na tishio linaloendelea la vikundi vya kigaidi vyenye msimamo mkali, na katika muktadha huu, Rais Al-Sisi alisisitiza juu ya umuhimu wa jukumu linalofanywa na Al-Azhar katika kusambaza mafundisho sahihi ya dini la Kiislamu na kupambana na itikadi kali. Rais Al-Sisi pia alikaribisha ombi la Rais wa Kenya kuhusu kuongeza idadi ya maimamu na wahubiri wa Kenya waliopata mafunzo kutoka Al-Azhar Al-Sharif.

- Mnamo tarehe 5/6/2015, ujumbe wa ngazi ya juu wa polisi wa Kenya wakiongozwa na Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya kuhusu Mambo ya Mafunzo walitembelea Misri, na ujumbe huo ulipokelewa na (Mohammed Al – Hamzawi) Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Nchi za Bonde la Mto wa Nile. Pande hizo mbili zilijadili njia za kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kupambana na ugaidi na nyingine ni za nyanja za usalama.

Mnamo Desemba 2018, Misri ilishiriki katika Mkutano wa ngazi ya juu mjini Nairobi kuhusu Amani na Usalama barani Afrika. Balozi Osama Abdel Khalek, Balozi wa Misri nchini Ethiopia na Mwakilishi wake wa Kudumu wa Umoja wa Afrika, alitoa hotuba ya Misri wakati wa ufunguzi wa mkutano huo pamoja na Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Monica Goma na Kamishna wa Amani na Usalama wa Afrika Ismael Sharqi, na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Nairobi Hana Tita.

- Wakati wa mkutano wake na Balozi wa Misri huko Nairobi, Balozi Khalid Al-Abyad mnamo Februari 2019, Waziri wa Ulinzi wa Kenya Rachel Omano alionesha nia kubwa ya kuimarisha ushirikiano na Misri katika uwanja wa kupambana na ugaidi kama changamoto kubwa zaidi inayoikabili Kenya, akisifu -katika muktadha huu- hotuba ya Rais Al-Sisi wakati wa hafla ya kuchukua kwake Uenyekiti wa Umija wa Afrika huko Addis Ababa na ishara yake kali kwa hitajio la ushirikiano wa juhudi za kikanda ili kukomesha mizizi ya ugaidi katika bara la Afrika.

- Katika mfumo wa ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na Kenya kwa ajili ya kupambana na ugaidi, Balozi Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Mambo ya kiafrika, alisafiri kwenda mji mkuu wa Kenya Nairobi ili kushiriki katika Mkutano wa kiafrika wa kikabda wa ngazi ya juu kuhusu kupambana na ugaidi , uliofanyika jijini Nairobi mnamo 10 na 11 Julai 2019. Ushiriki wake unatoka kwa Uenyekiti wa kimisri wa sasa kwa Baraza la Amani na Usalama la Afrika.


Ubadilishanaji wa kibiashara


Thamani ya ubadilishanaji wa biashara kati ya Misri na Kenya ilitofautiana katika vipindi tofauti vya wakati,kwani baada ya Misri ilipata ongezeko kubwa la uuzaji na usafirishaji wake pamoja na Kenya kuanzia 2007 hadi 2010, thamani hii ilishuka katika miaka iliyofuata 2011 kwa sababu ya hali zilizopatikana katika uchumi wa Misri, kisha serikali ilikuwa na nia ya kuongezeka ushirikiano pamoja na Kenya tangu mwaka 2015.


- Mnamo 2007, ukubwa wa biashara kati ya nchi hizo mbili ulifikia dola milioni 320, na kiwango cha mauzo ya nje ya kimisri kwenda nchini Kenya kiliongezeka kwa 48.9% na kilifikia dola milioni 176, na kwa mara ya kwanza tangu miaka 20, na mizani ya biashara ya Misri ilikuwa katika ziada ya dola milioni 34.4.


- Mnamo mwaka 2008, thamani ya biashara ilifikia dola milioni 378.3, na takwimu za kibiashara zinaonyesha kuwa usafirishaji wa kimisri kwenda Kenya ulikuwa dola milioni 156.2, wakati bidhaa kutoka Kenya zilikuwa dola milioni 222.1 kwa ziada ya dola milioni 65.9 kwa Kenya, ongezeko hilo ambalo halijatarajiwa katika thamani ya usafirishaji wa Kenya kwenda Misri katika mwaka 2008 lilikuwa matokeo ya kuongezeka kwa kiasi na thamani ya usafirishaji wa chai kwenda Misri, ambayo iliwekwa kama waingizaji wakubwa wa chai ya Kenya.
Mwaka wa 2010 ulishuhudia kuongezeka kwa mauzo ya nje ya kimisri kwenda Kenya, kufuatia kushuka kubwa kwa kubadilishana kwa biashara ya Misri na Kenya kupitia mwaka wa 2009, na hayo katika mfumo wa kushuka kwa thamani ya ubadilishanaji wa biashara kati ya Misri na aghalabu ya nchi za ulimwengu kwa sababu ya athari ya uchumi wa Misiri kwa shida ya kifedha duniani mnamo 2008, ambapo uagizaji wa bidhaa za kimisri kwenda Kenya uliongezeka kiasi dola milioni 232,35 katika mwaka 2010 ikilinganishwa na dola milioni 120 kupitia mwaka wa 2009. Na uingizaji wa kimisri kutoka Kenya pia uliongezeka sana katika mwaka huo huo, ambapo uliongezeka kutoka dola milioni 149.3 mwishoni mwa Desemba 2009 hadi milioni 228.66 ifikapo mwisho wa 2010.


- Kiasi cha biashara kati ya Misri na Kenya kilifikia dola milioni 640 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na Dola milioni 553 kupitia mwaka 2017 kwa ongezeko la 15,7%, na uagizaji wa kimisri kwa soko la Kenya uliongezeka kwa asilimia 21.7% kufikia dila milioni 353 ikilinganishwa na dola milioni 290 kupitia mwaka wa 2017.

Uingizaji wa kimisri kutoka soko la Kenya ulirekodi ongezeko kidogo kupitia mwaka wa 2018, kwa jumla ya dola milioni 288 ikilinganishwa na dola milioni 263 kupitia mwaka wa 2017 kwa ongezeko la 9.5%. Na moja ya vitu muhimu zaidi vya usafirishaji wa kimisri ambavyo villishuhudia kuongezeka kwa usafirishaji wake katika soko la Kenya : sukari, glasi, nepi, sabuni, vyombo vya glasi na paneli zinazotumiwa kwa maandishi.
Usafirishaji muhimu zaidi wa kimisri kwenda Kenya: sukari na molasi, bidhaa za chuma, matairi ya gari na betri, bidhaa za karatasi, kemikali na sabuni za kiviwandani, nyaya na viunganisho, vifaa vya kubadilisha umeme, dawa, vifaa vya uhandisi, vifaa vya kuzuia umeme, vifaa vya nyumbani, mikeka na mazulia, mafuta ya petroli, nta ya Paraffin, viyoyozi, fanicha, PABX, Plastiki za viwandani na Rangi, kauri, zana za afya, Televisheni, Saruji,sabuni, Mbolea, unga, Chokoleti na Pipi, Juisi na Jemu.
Uingizaji muhimu zaidi wa Kimisri kutoka Kenya ni: chai, tumbaku, sisal, kemikali, mafuta, matunda na mboga safi, maua yanayokatwa, maua kavu, baadi ya vitu vya wino ya kuchapisha.
Na nchi hizo mbili zinafanya juhudi ili kuimarisha na kuongeza thamani ya ubadilishanaji wa kibiashara kati yao, na miongoni mwa huhudi hizo :


- Mnamo Julai 2019, ujumbe wa Wamisri walishiriki kwenye Maonyesho na mkutano wa kazi za mkusanyiko wa COMESA 21 na hiyo wakati wa Wiki ya Biashara ya Kenya ya Tatu katika mji mkuu wa Kenya Nairobi kutoka 17 hadi 21 Julai 2019 na ilihudhuriwa na Marais wa Kenya, Uganda, Zambia, Mauritius na Makamu wa Rais wa Shelisheli na pia wawakilishi wa nchi Wajumbe 21, pamoja na waonyeshaji zaidi ya 200 kutoka mkoa huo, na wajumbe walisisitiza kuungwa mkono kwa uongozi wa kisiasa wa nchi hizo mbili kwa juhudi za kuongeza ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Misri na Kenya ndani ya mfumo wa COMESA na kuunga mkono jitihada zinazolenga kuungana vikundi vitatu vya Kiafrika COMESA, SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki.


- Mnamo Mei 2015, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Misri iliandaa maonyesho ya kwanza ya usafirishaji wa kimisri kwenda bara la Afrika Egypt export expo » katika mji mkuu Nairobi mbele ya mabalozi kadhaa wa nchi za Kiarabu, Rais wa Chama cha Kenya ya Biashara, na Katibu wa Chini wa Wizara ya Biashara ya Kenya, na Maonyesho hayo yalifunguliwa na Balozi wa Misiri nchini Kenya Mahmoud Talaat , ambapo alisisitiza umuhimu wa ziara kadhaa za wafanyabiashara wamisri kwani soko la Kenya lina washindani wengi waliopo tangu nyakati za zamani, ambazo zinahitaji kurudiwa mara kwa mara ili watumiaji wa Kenya wanaweza kujua bidhaa za kimisri, na alitoa wito kwa wawekezaji wa Kenya watembelee viwanda vya Misri na maeneo ya uwekezaji, na pia alissitiza haja ya ushirikiano zaidi ili kuboresha mizani ya kibiashara katika usafirishaji na uagizaji bidhaa kwa faida ya nchi hizo mbili, akionyesha kutafuta ili kuvutia waingizaji wamisri katika soko la Kenya, akibainisha kuwa shida ya usafirishaji ni shida maarufu zaidi zinazokabili usafirishaji wa bidhaa za nje kwenda Kenya.