Mahusiano ya Misri na Libya
Jumatano, Mei 01, 2019
Mahusiano ya Misri na Libya

Historia kwa ufupi

Libya inatiliwa shime kubwa na Misri. Wakati ambapo usalama wao wa kitaifa haugawanyiki ukiongezea na mahusiano ya kihistoria, mipaka ya pamoja na makabila ya misri ya Libya  yaliyoenea katika nchi mbili.Kuna wamisri wenye asili ya Libya na mamia ya maelfu ya wamisri  wanafanyakazi nchini Libya. Na  katika wigo wa mahusiano ya ujirani na kuoleana pamoja na maslahi ya juu ya nchi. Misri inashughulikia sana hali ya mambo nchini Libya.

 

Mahusiano ya misri ya Libya yana mizizi ya kihistoria na ya kijiografia.Wakati ambapo familia ya 23 ya wafalme wa Libya "AL-Mashwasha" imeitawala misri ya juu katika kipindi kutoka mwaka 734 B.C hadi mwaka 880B.C. Na imeanzishwa  makaazi kadhaa ya kiyunani katika nchi mbili kama vile, mji wa kurini  nchini Libya na mji wa Alexandria nchini misri.

 

VileVile wabatalima wamezitawala misri na mashariki mwa Libya "Birkah" na baadaye misri na birkah zikawa  majimbo ya taifa la kiothmani.Mnamo zama ya  Amr bin AL-Khatab  majeshi ya kiislamu  chini ya uongozi wa Amru bin Aasiy  yaliifungua misri. Na kutoka misri  ulianza ufunguzi wa kiislamu kwa  kaskazini mwa Afrika. Mwanzo ulianza kwa  maeneo  yanayokaribiana na misri  kutoka  magharibi  ikawa birkah kisha Tripoli mnamo zama ya utawala wa kiislamu.Kwa ujumla Tripoli ilikuwa huru na misri mara nyingine na khasa katika zama ya utawala wa AL-Aghalba katika kipindi kutoka  mwaka 800 B.K hadi mwaka 909 B.K. Ilhali mara nyingi nchi mbili  zilikuwa zikiungana  chini ya  mfumo mmoja wa idara na khasa katika zama ya  ukhalifa wa ukoo wa Fatuma katika kipindi kutoka  mwaka 909 B.K hadi mwaka 1171 B.K. Aidhaa nchi mbili  zikawa majimbo ya taifa la kiothmani mwaka 1517.

 

Misri ilikuwa nchi ya kwanza ilishirikiana rasmi na Libya baada ya kupata uhuru  mwanzoni mwa miaka ya hamsini ya karne ya ishirini.Mahuasiano baina ya nchi mbili  yamevipitia vipindi mbali mbali  .Na  mapinduzi ya Libya mwanzoni mwake  yaliathiriwa na mapinduzi  ya Julai.Aidhaa raisi wa zamani wa Libya kanali "AL-Kazafi" alifanya bidii ya kuungana na misri na hayo kwa kutia saini mkataba wa Tripoli mwezi wa Disembe mwaka 1969 ambao unakusanya unaoitwa "Mrengo wa kitaifa wa kiarabu".Na baadaye siria ilijiunga na  kumetangazwa umoja wa jamhuri za kiarabu baina ya misri, Libya na siria tarehe 17 Aprili mwaka 1971.Libya iliisaidia misri katika vita vya mwaka 73 wakati ambapo ilitia saini  mkataba  wa  ndege , aina ya "mirage"  pamoja na  ufaransa  na kutoa pasipoti kwa  marubani wa kimisri kwa ajili ya kutoa mafunzo nchini ufaransa. Wakati misri ilipokumbana na tatizo la manunuzi ya vifaru, aina ya  "T62", Libya  ilivinunua na kutuma makundi mawili ya ndege moja wapo likiongozwa na wamisri na jingine likiongozwa na walibya.

 

Mahusiano yamekipitia kipindi cha hali tete katika kipindi cha utawala wa raisi aliyekufa Anur AL-Sadat mpaka mahusoiano baina ya misri na Libya  yalirudi mwaka 1989  wakati wa kufanyika mkutano wa kilele wa kiarabu nchini  moroko na kufuta vibali  vya kuingia kwa wananchi  wa nchi mbili  pamoja na kutia saini  mikataba  10  inashughulikia mikondo mbali mbali  ya mashirikiano baina ya nchi mbili  mwaka 1991.

 

Kuanzia  kuzuka  kwa mgogoro wa Lokabi mzingiro wa kimarekani ambao umekuwa  wa kimataifa kwa uamuzi wa umoja wa mataifa mwaka 1992.Misri ilihangaikia kusaidia na kuunga mkono Libya kwa kuizingatia kuwa ni  msaidizi wake  katika mawasiliano yake pamoja na  ulimwengu wa kigeni.Aidhaa misri  ilishughulikia sana hali ya mambo nchini Libya katika zama baada ya AL-Kazafi "baada ya mapinduzi ya 17 Febuari 2011".Wakati ambapo misri iliiandaa mikutano kadhaa iliyowakusanya wanasiasa na wakilishi wa Libya  kwa ajili ya  walibya  wenyewe kujitatulia mizozo  mbali na  ushiriki wa misri katika makongamano ya kimataifa  yanayohusiana na  Libya  kwa ngazi za kikanda  au za kimataifa. Na la mwisho  lilikuwa ni kongamano la Bilmiru kusini mwa Italia katika   mnamo 12:13 Novemba  mwaka 2018 ambalo raisi  Abdal Fatah EL-Sisi  alilishiriki  ukiongezea na   kongamano la 12 la mawaziri  la  jumuiya ya mataifa  yaliyo  jirani na Libya mjini khartum  tarehe 29 Novemba 2018 na alilishiriki  waziri wa mambo ya kigeni wa kimisri.

 

Mahusiano ya kisiasa

 

Kwa hakika mzozo wa Libya unazingatiwa kuwa ni moja ya vipaumbile vya kisiasa vya kigeni vya misri sasa hivi .Ambapo nchi mbili  zina maslahi  ya kiusalama  na kiuchumi  ukiongezea na mahusiano  ya kijamii  na khasa kwa kuwa Libya inazingatiwa kuwa ni  mlango wa magharibi  wa misri.Kiasi kwamba mipaka  inayosambaa sambaa  baina ya nchi mbili  katika urefu wa  mstari wa mipaka kutoka  kaskazini  kwenye bahari  ya kati mpaka kusini  ambako  kuna mipaka na sudani kwa  urefu wa takriban  kilomita 1200.

 

Misri  haiweki akiba  yoyote ya juhudui  katika kuwasaidia walibya katika nchi yao kupita na kuelekea katika eneo  la amani na kupita kipindi hicho  kigumu  cha historia yao  na iliwakusanya  wagomvi  wa Libya  mjini  kairo katika  jaribio la kutaka  kurejesha mfungamano baina ya  yao  na kukusanya juhudi zao  pamoja na misri na mataifa yote yanayopenda amani na  Libya.

Misri daima inasisitiza kufuata suluhisho  kwa njia ya kisiasa kama njia pekee ya kuumaliza  mzozo na kuhakikisha uelewano  na pande mbali mbali  za raia  wa Libya  kukata  kuingkilia kati  kwa kigeni  , kufuata  suluhisho kwa njia ya kijeshi  ili kuumaliza  mzozo, udharura wa kulinda  mfumo na muungano wa taifa  la Libya na taasisi zake za  kitaifa na kushughulikia utatuzi  uwe  mbali na  tatuzi zilizopendekezwa na  mataifa ya kigeni.VileVile  misri  inasisitiza  umuhimu wa kuafikiana  walibya kuhusu  kuunga mkono  juhudi  zilizofanywa na kutekeleza  mkataba wa sakhriat, maamuzi ya baraza la amani yenye kuhusiana na mambo haya  , kupiga kura ya mani  juu ya katiba mpya na kufanyika uchaguzi wa kidemokrasia ya amani  kwa ajili ya  kuyahakikisha  mambo haya (mkataba wa sakhriat nao ni mkataba  umesainiwa mjini sakhriat nchini moroko  mwaka 2015 chini ya ulezi  wa umoja wa mataifa  ).

 

Mwaka 2014  jumuiya ya nchi jirani  na libya ziliasisiwa  kutokana na  uanachama  wa Aljeria ,misri,Libya,Tunisia,sudani,chadi na Nigeria  na zimeundwa wakati wa kufanyika  mkutano wa kilele wa kiafrika nchini  Gini ya Ikweta. Nchi jirani  na Libya na khasa  nchi jirani za moja kwa moja  kama vile,misri, Aljeria na Tunisia  zinafanya kazi  kwa lengo la kutoa  kusaidia na kuunga mkono  kwa kisiasa  na kiusalaa kwa  ajili ya Libya  kupitia kufanya kazi kwa vikundi ili kushirikiana  na Libya kwa mujibu wa chombo cha pamoja  cha nchi  jirani  kutokana na uratibu na kushirikiana na  katibu mkuu wa jumuiya  ya mataifa  ya kiarabu na  mwenyekiti wa  kamesheni  ya  umoja wa kiafrika kwa ajili ya kuujenga  muono  wa pamoja na ramani ya njia  kwa mujibu wa  utashi  wa walibya  na  vipaumbile vyao  vitaoneshwa kwa nchi jirani ili  ziyapitishe.

 

Mahusiano ya kiuchumi

 

Nchi mbili  zinafanya kazi  juu ya  kuyatekeleza  makubaliano  ya biashara ya pamoja  baina yao  yaliyosainiwa mwaka 1990 ukiongezea na  makubaliano  yaliyosainiwa pembezoni mwa  makubaliano hayo yanayohusiana na usafiri na abiria.Kiasi kwamba makubaliano  Hayo  yakawa  katika haja ya kurekebishwa na kubadilishwa ili kuendana na maendeleo na mabadiliko yaliyojitokeza  katika vyombo vya uchumi wa kimataifa kwa ujumla na uchumi wa nchi mbili hasa hasa.

 

Hakika  kuongezeka kwa mashirikiano ya kiuchumi  baina ya misri na Libya  kunakabiliwa na vikwazo mbali mbali  vinavyozingatiwa kuwa ni  sababu kuu ya  kuporomoka   hivi sasa   kunakoshuhudiwa na  makadirio ya  mashirikiano na  harakati ya biashara  baina ya nchi mbili  katika  miaka ya mwisho.Wakati ambapo  kiwango  cha ubadilishano wa kibiashara  kilipungua  kutoka dola za kimarekani bilioni 2,5 mwaka 2010 hadi kilifikia kiasi cha dola za kimarekani  bilioni 500 mwaka 2018.Ilhali kiwango cha vitega uchumi  vya Libya katika soko la misri  kinakidiriwa kwa dola za kimarekani bilioni 10 katika Nyanja za petroli,utalii,ujenzi na soko la fedha.

 

Kuna fursa nzuri kwa mashirika ya ujenzi  ya misri ili  kushiriki katika miradi ya  kujenga upya  pamoja na  kuwepo kwa  marekebisho kadhaa ya kiuchumi  yaliyofanywa na serikali ya Libya  kwa ajili ya  kuboresha  mazingira ya  wafanyakazi  na kuvutia  vitega uchumi vya kigeni  na miongoni mwayo kuingilia kati kwa  benki  kuu ya Libya ili  kuiacha huru  bei ya paundi ya Libya  kwa kuiga  lililofanywa na n misri  katika uwanja huu. Na  marekebisho hayo yatakuwa na  mchango muhimu sana  katika  kuboresha ufanisi  wa uchumi wa Libya na  kuichangamsha  harakati ya ubadilishano wa kibiashara  na  vitega uchumi pamoja na mataifa mbali mbali ulimwenguni kote.Na miongoni mwa mataifa muhimu zaidi ni misri katika eneo la kiarabu.

 

VileVile kuanzisha  chumba cha biashara cha misri na Libya  kunazingatiwa kuwa ni  hatua kwa ajili ya  kuimarisha  mashirikiano  ya kibiashara na ushirikiano kamili wa kiuchumi  baina ya misri na Libya na kutosheleza  uhuru wa kusafirisha abiria , rasilimali, bidhaa, huduma, kuondosha vikwazo pamoja na  kusaidia na kuunga mkono mashirika ili kurahisisha  harakati ya bidhaa.

 

Aidhaa nchi zinahangaikia kwa ajili ya kutekeleza miradi ya pamoja na khasa katika Nyanja za usafiri, uchukuzi, barabara, bandari, miundo mbinu na umeme  kutegemea juu ya  uzoefu wa misri katika mpango wa sasa  wa umeme wa miradi mikubwa na ushiriki wa miradi ya viwanda ambayo misri  ina uzoefu na teknolojia  inayoongoza kama vile, utengenezaji wa vifaa vya ujenzi, bidhaa za petroil na vyakula.

 

VileVile  masoko ya Libya yatawavutia wafanyakazi wa misri kupitia kujenga upya katika kipindi kijacho na khasa kwamba kiwango chake  kilikuwa kinafikia wafanyakazi milioni 2 na kilipungua na kipo kati ya asilimia  35% na 40% baada ya mapinduzi. Aidhaa kuwepo kwa fursa kubwa ili kuongeza ubadilishano wa kibiashara baina ya nchi mbili mnamo kipindi kijacho. Kiasi kwamba  kiwango cha ubadilishano huo kilipungua kwa asilimia 25% Ikilinganishwa na  kiwango chake kabla ya mapinduzi.

 

 

Hivi sasa Libya inazipokea aina mbali mbali za bidhaa zinazoagizwa kutoka misri kama vile, kauri, rangi za kupakaa, vifaa mbali mbali vya ujenzi, semanti, vyakula na kilimo . Eneo la mashariki nchini Libya linajumuisha asilimia 70% ya bidhaa zinazoagizwa kutoka misri. Hakika kurejesha utulivu wa kiusalama nchini Libya kutarejea katika biashara baina ya nchi mbili na ongezeko la ushirikiano mzuri baina yao.

 

Mahusiano ya kiutamaduni

 

Misri  na Libya zilitia saini protokoli ya kiutamaduni tarehe 28 Januari 2013 inayolazimisha kuunda tume  inajumuisha  wanafikira wakuu, wasomi  na wasanii nchini misri  na Libya, kushiriki katika maonesho ya vitabu ya kikanda na ya kimataifa, kushiriki katika uwanja wa haki miiliki na orodha za kisanaa, sanaa za uchongaji vinyago na maigizo, sinema ,majumba ya maigizo, kubadilishana timu za muziki za kimaumbile,sanaa za kienyeji katika matamsha pamoja na kufanyika  wiki za kiutamaduni baina ya nchi mbili.