Misri na Namibia
Jumapili, Machi 17, 2019
 Misri na Namibia

Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza ambazo zilianzisha mahusiano ya kidiplomasia na Namibia baada ya uhuru katika mwaka 1990. Aprili 2008, Namibia ilimtuma balozi wake wa kwanza huko Kairo na Mashariki ya Kati baada ya kuanzisha uwakilishi wake wa kwanza wa kidiplomasia huko Mashariki ya Kati Mjini Kairo, mwaka 2007. Misri pia ilikuwa na jukumu kubwa katika kuunga mkono harakati za Uhuru wa Namibia (SWAPO) wakati wa mapambano yake dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ili kupata uhuru, pamoja na msaada wa Misri kwa Namibia katika vikao vya kimataifa, hasa katika Umoja wa Mataifa. Misri ilifanya jukumu kuu katika suala hili kupitia Baraza la Umoja wa Mataifa la Namibia. Misri pia imetoa misaada ya fedha na maadili kwa Namibia, ikiwa ni pamoja na kufunza kundi la kijeshi la kwanza la Namibia wakati wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi kwa mwaliko wa Rais aliyefariki dunia Gamal Abdel Nasser. Kairo ilifungua kituo cha kwanza kilichofunguliwa nje ya Namibia kwa harakati za Swabo.

Mahusiano ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili yanajulikana kwa nguvu na ustadi, na kufikia ushiriki wa Misri katika sherehe za uhuru wa Namibia mwaka 1990, kwani Misri ni kiongozi wa tassisi za Umoja wa Kiafrika na Misri inasisitiza kuendelea kuiunga mkono Namibia kisiasa na kiuchumi baada ya kupata uhuru.

Na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi alipokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa Rais wa Namibia wakati huo Hifikepunye  Pohamba tarehe 19 Juni, 2014 kwa kutawala kwake Misri.

Ziara za pamoja:

Rais wa Namibia Hage Geingob alishiriki katika Mkutano wa tatu wa kiafrika Mjini Sharm El Sheikh, Juni 2015.

Ziara ya ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Namibia Bwana Atoni Nyuma ulitembelea Kairo kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 2 Novemba 2010, na katika ziara hii Mawaziri wa Mambo ya Nje, biashara, viwanda, kilimo na elimu walikutana.

Ziara ya ujumbe ulioongozwa na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje ili kushiriki katika Mkutano wa kilele cha kutoegemea kwa upande wowote Mjini Sharm El Sheikh, Juni 2009.

Ziara ya ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje ili kushiriki katika Mkutano wa China-Afrika Mjini Sharm El Sheikh, Novemba 2009.

Ziara ya ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Biashara na Viwanda Dokta Hage Geingob ili kushiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Biashara wa Afrika, katika kipindi cha 27 Oktoba hadi 29 Oktoba 2009 Mjini Kairo.

Ziara ya ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Elimu wa Namibia Mwezi wa Februari, 2008 ili kujadili njia za kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya elimu, na kunufaika na uzoefu wa Miisri katika nyanja ya kujifunza na kufunza kwa Chuo Kikuu.

Ziara ya ujumbe kwa Misri Oktoba 2008 ulioongozwa na Waziri wa Afya Daktari: Rechard Kamwoi, ili kujadili njia za kuendelea na kukuza mahusiano ya ushirikiano katika nyanja ya afya kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Spika wa wa Bunge la Namibia Dokta Thio bin Gorirab _ ambaye ni Mwenyekiti  wa Umoja wa Bungeza kimataifa_ aliyetembelea Misri Desemba 2008 ili kuchunguza ukweli wa matukio ya Ghaza.

Ziara ya Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya kiafrika na mambo ya Umoja wa Afrika na Naibu wa msaidizi wa mambo ya Mashariki na Kusini mwa  Afrika, Aprili 2009 Mjini Walfish Bai na yalisainiwa makubaliano mawili katika nyanja za elimu na madini. Pamoja na kujadili maudhui kadhaa za kibiashara na kisiasa.

ziara ya ujumbe ulioongozwa na Katibu wa Mfuko wa Misri wa ushirikiano wa kiufundi na Afrikaalitembelea Namibia tarehe 2 na 3 Machi 2009, na ujumbe huu ulikutana na Waziri wa kilimo na Waziri wa Afya.

Ziara ya ujumbe ili kushiriki katika Mkutano wa kumi na tisa wa Wakuu wa vifaa vya kimataifa vinavyohusika na utekelezaji wa sheria za madawa ya kulevya (Honelia) uliofanyika Mjini Bondhouk tarehe 12 hadi 16 Oktoba, 2009.