Misri Na Somali
Jumatatu, Aprili 15, 2019
Misri Na Somali

 

Historia :

Mahusiano kati Misri na Somali ni yenye nguvu na uimara ,basi ni mahusiano ya kihistoria tangu enzi ya Mafarao hasa wakati ambapo mfalme wa kike Hatshepsut,ambaye ni Firauni wa tano wa familia kumi na nane,alituma ujumbe za biashara kwa nchi ya "Punt", Somalia sasa, ili kuleta bidhaa za eneo lile, hasa harufu za kunukia, vile vile katika enzi ya kisasa Misri ilikuwa nchi ya kwanza ya kutambuliwa uhuru wa Somalia mwaka 1960 ,bado inatajwa kwa tathmini zote jina la shahidi wa kimisri Kamal Eldin Salah ambaye ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, aliyelipa maisha yake mwaka 1957 kama thamani kwa juhudi  zake za  kupata uhuru wa Somalia  na kuhifadhi umoja wake.

 Somalia ni moja ya nchi muhimu zaidi za Pembe ya Afrika, ambayo ina mchango mkubwa katika kudhibiti(kutawala) Mlango wa Bab el-Mandeb, ambao ni mlango wa kusini kwa Bahari ya Shamu na Suez ,jambo lililosababisha kuongezeka kwa umuhimu wake wa kiuchumi ,kijiografia na kisiasa kwa Misri. Misri imeunga mkono Somalia katika kipindi kilichofuatilia uhuru katika nyanja mbalimbali, hasa katika uwanja wa elimu ambapo zilikuwepo shule na walimu wa kimisri mjini Mogadishu, kama vile ujumbe za Al-Azhar na walimu wanaoifuata walichangia kueneza (kusambaza) elimu na mafundisho ya Uislamu wa kweli.

Mahusiano ya kisiasa:

 Tangu kuzuka kwa mgogoro wa Somalia mwaka 1991,Misri ilishughulikia kupata ufumbuzi na kuyamaliza mapigano kati ya ndugu wa Somalia, na katika mazingira ya juhudi za Misri  zinazoendelea ili kupata ufumbuzi kwa tatizo la ( mgogoro wa ) Somalia , kairo iliandaa mkutano wa upatanisho wa kitaifa wa kisomalia mwaka 1997 uliojumaisha zaidi ya viongozi wa makundi ya kisomalia wakati huo. Misri pia  huwa na nia ya kushiriki katika mikutano yote ya kimataifa na mikutano inayohusu  mgogoro wa Somalia miongoni mwayo Mkutano wa Al-Khartoum mwaka 2006, na Mkutano wa Djibouti mwaka 2008, ambao ulisababisha  mwishoni kuja kwa Rais wa zamani "Sharif Sheikh Ahmed,"kama rais wa Somalia.

Misri pia ni mwanachama hai  (chanya )katika kundi la uchumi la kimataifa linalohusisha na tatizo  la Somalia na huwa na nia (inazigatia )kushiriki katika mikutano yote yanayofanyikwa na kundi , Misri imezidi hatua yake ya kimataifa katika miaka ya karibuni kutafutia kuungwa mkono kwa swala la Somalia na kuhamasisha vikosi vya kimataifa kuchangia  kujenga upya kwa taasisi za kitaifa za  Somalia kutokana na umuhimu mkubwa wa  Somalia na mchango wake katika kuimarisha usalama wa taifa la Misri, Misri imeshiriki  kwa ujumbe unaoongozwa na Mhandisi Ismail Sharif ambaye ni Waziri Mkuu, katika Mkutano wa London juu ya Somalia kutoka 10 hadi 11 Mei 2017 kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Somalia na serikali ya Uingereza ili kutafuta kuimarisha utulivu na Usalama nchini Somalia.

Vile vile, Misri ni mwanachama wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano linalohusisha na kupambana  na Uharamia katika pwani ya Somalia ambako ilikuwa urais wa kundi la kazi la nne linalofuatilia  kundi la Mawasiliano ambalo linahusisha na kuunga juhudi za kidiplomasia na kusambaza uelewe kuhusu  uharamia, Misri imepokea mkutano wa pili wa kundi la mawasiliano  katika March 2017. Katika 20 / 8/2017 Mohamed Abdullahi Mohamed Frmajo  ambaye ni Rais wa Somalia alizuru  Misri na Rais Abdel Fattah sisi amabapo alijadili pamja naye njia za kuimarisha mahusiano ya kati . Na kutoa msaada wa kukiri (kuhakikisha) maendeleo na utulivu nchini Somalia ,kama vile kuunga mkono katika nyanja za  elimu  ,mafunzo na huduma za afya katika mfumo wa sanduku la Misri kwa Ushirikiano wa kiufundi na Afrika, pamoja na kuyajadili masuala kadhaa ya kikanda, kiafrika na ushirikiano wa kupambana  na ugaidi .

Mahusian kiuchumi .

Mahusiano ya kiuchumi kati ya Misri na Somalia yameshuhudia ongezeko la kasi katika miaka ya karibuni, yakiambatana na kuwepo kwa nia nguvu ya kisiasa ili kuiweka mipango ya siku zijazo na kufungua milango mipya kwa ajili ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali .Na kiwango cha biashara kati ya Misri na Somalia kilifikia  dola milioni 88 mnamo mwaka 2017 ikilinganishwa na  dola milioni  54 mwaka 2016. Mauzo ya nje ya Misri kwa Somalia ni bidhaa za chakula na vifaa vya ujenzi na madawa , wakati (ilhali) Misri inagiza wanyama kutoka somali. Katika Agosti 2016 ,Balozi wa Misri nchini Somalia alifungua mkutano wa wafanyabiashara wa Misri na wa Somalia kwa kichwa ( moyoni mwa Misri ).

Miradi ya niashati na maji huzingatiwa moja ya nyanja ambazo zinaweza kushuhudia maendeleo makubwa kati ya nchi mbili, hasa katika miradi inayohusisha na seli za nishati ya jua na mitandao yake , kwani hali ya hewa ya nchi mbili ni sawa (sambamba) , pia sekta ya benki pamoja na uwanja wa kilimo na mifugo ni moja ya sekta za mutakbali zinazoweka kuzi zingatiwa kama njia ya kuamsha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

 Mnamo miaka miwili ya 2015 na 2016,Misri na Somalia zilitia saini mikataba ya  ufahamu katika nyanja mbalimbali  kama vile afya, elimu, vikwazo, kilimo, mifugo ,uvuvi na biashara.katika Aprili 19 2016 Somalia na Misri,zilitia saini mkataba wa ufahamu katika uwanja wa ushirikiano wa kiuchumi unaokusanya kuanzisha kamati ya biashara ya pamoja chini ya uenyekiti wa mawaziri wa biashara na wahusika wakubwa katika nchi hizo mbili ili kurahisisha zoezi (harakati)la biashara na kuondoa vikwazo vyote  ikiwa ni pamoja viongozi waandamizi katika uwanja wa biashara, kujadili kuwezesha harakati ya biashara na kuondoa vikwazo vyote na kujadili serikali mahitajio ya kiserikali katika miundombinu, usafiri wa bahari, afya, kilimo, ufugaji na uvuvi.

Katika 2018/03/18, Ubalozi wa Misri ilitoa shehena ya msaada wa matibabu iliyokadiriwa  kwa juu ya tani  2 ya dawa inayotolewa na Wekala ya Ushirikiano wa kimisri kwa ajili ya maendeleo inayofuata wizara ya mambo ya nje  kwa Dr Abdullah Hashi,ambaye ni Naibu wa Kwanza wa Wizara ya Afya ya Somalia. Katika 2017/05/17 chini ya maelekezo ya Rais Abdel Fattah Sisi Misri iliendelea juhudi zake za kusaidia ndugu wao nchini Somalia walioathirika na wimbi la ukavu na zilizotokea  maeneo mbalimbali kutoka Somalia, ambako ilipeleka misaada mipya ya vyakula, dawa, na vifaa vya matibabu.

 

Mahusisno ya kiutamaduni.

Mnamo Oktoba 2014, Rais Abdelfattah Al-Sisi alikubali kuogngeza idadi ya ujumbe zilizotolewa kwa wanafunzi wa Somalia katika vyuo vikuu vya Misri hadi ujumbe  wa kimasomo 200 kwa kila mwaka, pamoja na kuamiliana na wanafunzi wa Somali wanaosoma  katika vyuo vikuu vya Misri kama wanafunzi wa Misri katika mfumo wa Kuunga mkono kwa mahusiano pamoja na nchi jirani  Somalia, hasa katika nyanja za kisanaa ambapo Misri ina ujuzi bora .Upande wa Somalia sasa unapata ujumbe wa masomo 50 ya kila mwaka kwa mujibu wa  mpango wa kitamaduni kati ya nchi hizo mbili, pamoja na ujumbe 40 nyingine kwa Ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na Ubalozi wa Somalia katika Cairo.

Misri ina mchango muhimu hadi sasa ​​katika usambazaji wa utamaduni na elimu katika nchi jirani ya Somalia kwa kutuma walimu wa Wizara ya Elimu ili kufundisha  katika shule za Somalia au walimu wa Al-Azhar Al-Sharif,vile vile wajuzi wa Misri wa Ushirikiano wa kisanaa na Afrika wanaosambaza elimu katika taasisi za elimu ya juu, pia Al-Azhar inatoa idadi ya ujumbeza kimasomo za kila mwaka kwa ajili ya wanafunzi kutoka Jamhuri ya Somalia ili wasome katika Chuo kikuu cha Al Azhar au vyuo vya Alazhar.

 Mahusiano ya kijeshi

ubalozi wa Misri mjini Mogadishu ilitangaza tarehe Novemba14, 2014 kufikia kwa msaada wa kijeshi wa Misri kwa Mogadishu, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kijeshi na vya kilogistia , katika mfumo wa mpango wa Misri mwenye muda mrefu  ili  kuziunga mkono taasisi za usalama nchini Somalia, pia Misri imeshatoa misaada ya kijeshi  katika mwezi wa Februari 2016 kama :magari ya kivita na vyombo vya ofisi kwa jeshi la Somalia, na katika July 2016 Misri imetoa vifaa kamili kwa kundi la vikosi hasa vya jeshi vya Somalia na kompyuta. Misri pia alishuhudia katika kipindi kilichopita ziara za idadi ya mawaziri na wanajeshi wa Somali , ambapo nchi mbili zimetiwa saini mkataba wa ufahamu wa ushirikiano wa pamoja na ushirikiano katika nyanja kadhaa za kijeshi, jinsi inavyounga mkono nyanja zote za kupambana na ugaidi.