Misri na Sudan Kusini
Jumapili, Februari 24, 2019
 Misri na Sudan Kusini

  • Kairo imeitambua Jamhuri ya Sudan Kusini rasmi tarehe 9 Julai 2011.
  • Misri imetuma kikosi kikubwa zaidi katika vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini Sudan ya kusini, ili kusaidia hali ya utulivu wa nchi.
  • Misri inaisaidia Sudani Kusini katika nyanja za elimu, afya, miradi ya huduma na miundombinu, na ushirikiano wa pamoja katika nyanja zote.
  • Waraka wa maelewano juu ya ushirikiano wa kilimo ili kuanzisha shamba sanifu la pamoja katika eneo la hekta 200.
  • Misri imeanzisha maabara kuu ili kupima ubora wa maji huko Juba na ina vifaa vya kisasa , zana zinazohitajika ili kupunguza vyanzo vya maji machafu katika majimbo yote ya Sudan ya kusini.
  • Misri imetekeleza miradi kadhaa ya maendeleo katika maeneo ya pekee ya Sudan ya kusini ili kutoa maji safi ya kunywa kwa njia ya kuchimba na kuwezesha visima 30 vya maji chini ya ardhi. Na kuanzishwa kwa vituo 6 vya kunywa kwa kutegemea juu ya visima vya maji chini ya ardhi mjini Juba na utekelezaji wa kituo kikubwa cha kuinua katika mji wa Wau, pamoja na Ukarabati wa vituo vya kupima viwango na mifereji ya maji kwenye mito mikuu Sudan ya Kusini.
  • kusainiwa itifaki ya ushirikiano kati ya Misri na Sudan ya kusini ili kuanzisha eneo kubwa zaidi la kimisri la viwanda katika mji Mkuu (Juba) katika eneo la kilomita za mraba 116 ili kuchangia kuongeza idadi ya mauzo ya nje ya Misri na kutoa nafasi za ajira kwa vijana.
  • Kuanzishwa tawi la Chuo Kikuu cha Alexandria kusini, pamoja na kutoa masomo ya kulipiwa ya kila mwaka kwa wanafunzi wa Sudan Kusini katika vyuo vikuu vya Misri.