
Mahusiano ya kisiasa :
Mahusiano ya kisiasa kati ya Misri na Sudan yanaonesha historia ya pamoja, na zina vipimo vya kikanda na kimataifa kwa sababu ya Jiografia ya kisiasa ya nchi hizo mbili, Pia zina masuala mbalimbali ya pamoja na ya kikanda ambayo yanahitaji uratibu wa mara kwa mara kati ya nchi hizo mbili, kama vile suala la maji ya Nile na ushirikiano kati ya nchi za Bonde la mto Nile kwa ajili ya maslahi ya pamoja, na faili la usalama na utulivu katika Bonde la Bahari ya nyekundu na pembe ya Afrika, halafu faili la uratibu kuhusu masuala ya Afrika, iwe kupitia Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa na ya kikanda au kwa njia ya kushughulika na masuala yenye athari kama vile kupambana na ugaidi na wenye msimamo mkali na mengineyo.
Mahusiano ya Misri na Sudan yanashuhudia ufanisi mkubwa kipindi cha hivi karibuni, na mwishoni ni mikutano ya kipindi cha pili cha Kamati ya rais Misri na Sudan ya pamoja iliyofanyika mjini Khartoum Oktoba 2018 chini ya uongozi wa Marais wawili Sisi na Bashir, ambayo ilikuja kama kuimarisha ushirikiano na ukamilifu kati ya nchi hizo mbili, na kusisitiza juu ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili na idara ya kisiasa ili kufikia maslahi ya wananchi wa nchi mbili za Bonde la Nile, na kuangalia mahusiano haya kwa upeo mpana na Nyanja pana za ushirikiano wa kukuza na wenye manufaa, na kuthibitisha uaminifu unaoongezeka kati ya nchi hizo mbili.
Misri imekaribisha jitihada za Sudan ili kufikia amani na utulivu kusini mwa Sudan, na ilionesha msaada wake kwa juhudi hizi na nia yake ya kutoa njia mbalimbali katika kutekeleza makubaliano ya amani iliyosainiwa Khartoum.. Na Maraisi wawili pia wanasisitiza juu ya kuendeleza mazungumzo kati ya nchi hizo mbili juu ya masuala ya kikanda na vikao vya kimataifa, Hasa kwa kuwa Misri inachukua uongozi wa Umoja wa Afrika mwaka 2019, na nia ya kuendelea na uratibu mkubwa kati yao kwa njia ambayo inachangia kufikia maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili, Zaidi ya kuimarisha ushirikiano katika ngazi mbalimbali na kukuza juhudi za ushirikiano kati ya nchi za kanda na bara la Afrika na kufikia maendeleo yenye faida kwa ajili ya wananchi wake.
Mahusiano ya Misri na Sudan yanashuhudia mafanikio makubwa wakati wa kipindi cha Rais Abdel-Fattah al-Sisi, ambaye anajitahidi pamoja na Rais wa Sudan Omar al-Bashir ili kuendeleza mahusiano na kuyaimarisha ili kufikia hatua ya ukamilifu wa kimkakati kati ya nchi mbili katika nyanja mbalimbali, Mwelekeo huu unaonekana katika hati ya mkakati iliyosainiwa na maraisi wawili El-Sisi na Al-Bashir Oktoba 2016, na kuwepo kwa utaratibu wazi katika mikutano ya pande nne, ambayo inajumuisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zote mbili na wakuu wawili wa kituo cha upelelezi ili kuweka mambo vizuri kwa namna ambayo haitaruhusu watu wa nje kujaribu kutumia hali hiyo kwa ajili ya faida yao yenyewe dhidi ya maslahi ya wananchi wa nchi hizo mbili na historia yao ya pamoja.
Ziara za pamoja kati ya nchi hizo mbili:
Katika kipindi cha miaka mitano (2014-2019), zaidi ya mikutano 25 ya kilele imefanyika kati ya Maraisi wawili wa nchi hizo mbili, na idadi hii haijawahi kupatikana kati ya nchi na nchi nyingine yoyote, zifuatazo ni ziara muhimu zaidi juu ya ngazi ya Urais:
Ziara za pamoja:
Tarehe 27/1/2019, Rais Omar al-Bashir alitembelea Kairo, ambapo alikutana na Rais Abdel Fattah al-Sisi. Ziara hiyo ilikuja ili kusisitiza juu ya nia ya viongozi wawili kuhusu kuimarisha mahusiano kati ya nchi mbili ndugu, pamoja na mashauriano ya pamoja kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa yenye umuhimu wa pamoja.
Tarehe 6/11/2018, Rais Abdel Fattah al-Sisi alikutana na Rais wa Sudan Omar al-Bashir huko Sharm el-Sheikh ili kuhudhuria hitimisho la Kongamano la Kimataifa la Vijana..
Tarehe 25/10/2018, Rais Abdul Fattah Al-Sisi alifanya ziara rasmi mjini Khartoum, na Mkutano wa Kilele ulifanyika kati ya Marais wawili kujadili njia za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote na kuyafanya kama mfano wa ushirikiano na ukamilifu katika ulimwengu wa Kiarabu na wa Kiafrika, pamoja na kuzingatia juu ya kuanzishwa kwa miradi mikubwa katika nyanja za uunganishaji wa umeme, chuma na njia zingine za usafiri, pamoja na upande wa usalama wa chakula, miundombinu, sekta ya biashara, uwekezaji, utamaduni, elimu na mengine.
Tarehe 19/7/2018, Rais Abdul Fattah Al-Sisi alitembelea Sudan, ambapo pande mbili zilijadili njia za kuimarisha mahusiano kati ya nchi mbili katika viwango vyote vya kisiasa, kiuchumi, usalama na utamaduni, na masuala yote yenye maslahi ya pamoja.
Tarehe 18/3/2018, Rais Omar al-Bashir alitembelea Misri, ambapo alipokewa na Rais Abdel Fattah al-Sisi. Pande mbili zilijadili njia za kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja zote, kwa njia ambayo itachangia kufikia maslahi ya wananchi wa nchi hizo mbili ndugu, Maraisi wawili pia walishuhudia sherehe ya familia ya kimisri katika uwanja wa kimataifa wa Kairo.
Tarehe 10/10/2016, Rais Abdelfattah El-Sisi alifanya ziara nchini Sudan ili kushiriki katika kikao cha mwisho cha Majadiliano ya kitaifa ya Sudan, kupitia kikao hicho, Rais El-Sisi alifanya mkutano mfupi na Maraisi wa Sudan, Mauritania, Chad na Uganda, wakati wa mkutano wa mwisho wa majadiliano ya kitaifa nchini Sudan.
Tarehe 5/10/2016, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alifanya ziara nchini Misri, ili kuongoza ujumbe wa nchi yake katika shughuli za Kamati ya juu ya Pamoja kati ya Misri na Sudan, wakati wa ziara hiyo, Rais Abdel Fattah al-Sisi alimpa Nishani ya "nyota ya heshima", Kwa kutambua ushiriki wake katika vitengo vya kijeshi vya Sudan, ambavyo vilisaidia katika uwanja wa kupigana katika vita vya Oktoba 1973. Hii ilikuja wakati wa ushiriki wa Rais "Sisi" na "Bashir" katika onesho la kijeshi lililofanyika kwenye makao makuu ya Jeshi la Pili huko Tall Al-Kabiir mjini Ismailia kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa vita vya Oktoba.
Tarehe 21/2/2016, Rais wa Sudan Omar Al-Bashir alitembelea Misri ili kushiriki katika shughuli za kongamano la Afrika 2016 mjini Sharm El-Sheikh, ambapo alikutana na Rais Abdel Fattah Al-Sisi wakati wa kongamano hilo. Pande mbili zilijadili njia za kukuza ushirikiano, hasa katika nyanja za uchumi, biashara na uwekezaji.
Tarehe 2/6/2015, Rais Abdel Fattah al-Sisi alitembelea Sudan ili kushiriki katika sherehe ya kuchukua Rais Omar al-Bashir urasi wa nchi ya Sudan kwa kipindi kipya. Marais wawili walifanya mkutano ambapo Sisi alisisitiza maandalizi kamili ya Misri ili kutoa msaada wowote kwa Sudan ili kufikia maendeleo na utulivu zaidi, pia pande hizo mbili zimejadiliana kuhusu hali zote katika uwanja wa Kiarabu na Kiafrika.
Tarehe 27/3/2015, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alitembelea Misri ili kuhudhuria Makutano wa Kilele cha 26 cha huko Sharm el-Sheikh na alipokewa na Rais Abdel-Fattah al-Sisi.
Tarehe 23/3/2015, Rais Abdel Fattah al-Sisi alitembelea Sudan ili kushiriki katika Mkutano wa kilele cha pande tatu za Misri, Sudan na Ethiopia ambacho kiliitishwa na Sudan na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hela Miriam DiSalleen alihudhiria kilele hicho , na Marais wawili "Sisi" na "Bashir" walijadili njia za kuendeleza mahusiano kati ya nchi hizo mbili, na hali mpya zote za Mashariki ya Kati, na masuala yenye umuhimu wa pamoja.
Tarehe 13/3/2015, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alitembelea Misri ili kuhudhuria mkutano wa kuunga mkono na kuendeleza uchumi wa Misri huko Sharm El-Sheikh na alipokewa na Rais Abdel Fattah al-Sisi wakati wa mkutano huo.
Tarehe 18/10/2014 , Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, alitembelea Misri na Rais Abdel Fattah al-Sisi alimpokea, na Mkutano huo ulishuhudia maelezo ya pande kadhaa za mahusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa katika kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kuongezeka kwa kubadilishana biashara, hasa wakati wa ufunguzi wa bandari ya Qastal / Ashqit "kati ya nchi hizo mbili, na kujadili uwezekano wa kuanzisha eneo la biashara huru kati yao.
Tarehe 27/6/2014, Rais Abdel Fattah al-Sisi alitembelea Khartoum ili kumjulia hali Rais wa Sudan Omar al-Bashir, juu ya mafanikio ya upasuaji alioufanya na walijadili masuala ya maslahi ya pamoja katika viwango vya kikanda na kimataifa, hasa hali nchini Libya, Syria, Iraq na Sudan Kusini, na kubadilishana maoni kati ya pande mbili kuhusu masuala hayo.
Mahusiano ya kiuchumi:
Sera ya Misri inashughulikia kuendeleza mahusiano ya pamoja ya kiuchumi na kufanya kiwango cha ubora katika nyanja mbalimbali, kwani Sudan ni nchi pekee ambayo ina ofisi ndogo ya ubalozi mjini Aswan, ambayo inaonesha ukuaji wa kiasi cha ubadilishanaji wa biashara. Jukumu la ubalozi huo sio tu kuimarisha mahusiano ya biashara na ya kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, lakini pia linajumuisha mahusiano katika nyanja mbalimbali.
Mahusiano ya biashara ya Misri na Sudan wameshuhudia ukuaji wa ajabu katika miaka ya hivi karibuni, hasa kutokana na uanachama wa nchi hizo mbili katika eneo la Biashara huru kubwa la Kiarabu na COMESA, Misri na Sudan wanajitahidi ili kuimarisha mahusiano ya kibiashara kwa kuanzisha miradi ya pamoja ya kiuchumi katika sekta zote, viwanda,Kilimo, umeme, maji, utajiri wa wanyama, wafanyakazi wenye mafunzo ya kiufundi), ambayo zinafaidika nchi hizo mbili, na kwa kweli huchangia marekebisho ya mahusiano ya baadaye kati ya Sudan na Misri, ambayo inaoneshwa vyema juu ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi hizo mbili.
Misri na Sudan zina vipengele vingi vya kiuchumi ambavyo vinaruhusu kufikia viwango kadhaa vya biashara ya ndani, kwani Misri inaagiza nyama, ufuta, unga wa ngano na malighafi kutoka Sudan. Na Sudani inaagiza mashine za chakula, vifaa vya ujenzi, nguo na madawa kutoka Misri. Sudan pia ina vifaa vya madini muhimu sana ambavyo nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana kwa kuzitumia katika viwanda.
Kiasi cha uwekezaji wa Misri katika soko la Sudan kinakadiriwa kwa bilioni 10 na dola milioni 100 kulingana na takwimu za 2017. Uwekezaji uligawanywa kwa miradi 229, miongoni mwao 122 ambayo ilikuwa miradi ya viwanda kwa uwekezaji wa dola bilioni 1.372 katika saruji, plastiki, marumaru, madawa, vipodozi, samani, chuma na viwanda vya chakula, na miradi 90 ya huduma na kiasi cha uwekezaji wake ni dola bilioni 8.629 kama benki, umwagiliaji, huduma za umeme, maabara ya uchambuzi, vituo vya matibabu na teknolojia ya habari na mawasiliano, pamoja na miradi 17 ya kilimo na kiasi cha uwekezaji wake ni dola milioni 89 katika sekta za mazao na uzalishaji wa mifugo, kuku na uvuvi.
Kuna makampuni 315 ya Sudan nchini Misri, ambayo uwekezaji wake unasambazwa kati ya sekta za viwanda, biashara, kilimo, fedha, ujenzi, utalii na sekta za mawasiliano. Sekta za viwanda zinawakilishwa na makampuni 73 na uwekezaji wa unakadiriwa na dola milioni 50.4. Ama Shughuli za fedha ni nafasi ya pili na makampuni yake ni 7 na uwekezaji wake unakadiriwa dola miloni 21.3.
Kuna umuhimu mkubwa kwa kuvutia uwekezaji wa Misri kwa Sudan katika sekta ya kilimo, kwa ajili ya kulima maeneo makubwa ya ngano ili kujaza pengo nchini Sudan na Misri, pamoja na kupatikana fursa za uzalishaji wa pamba ili kukidhi mahitaji ya viwanda vya Misri.
Kuna nyanja za uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji wa sukari, ili Sudani kufikia kujitegemea katika sekta hii, kwani Sudan ina ardhi kubwa na maji mengi. Uzalishaji wa mafuta pia ni kipaumbele katika nyanja ya uzalishaji na viwanda vya kilimo kwa njia ya upanuzi katika kulima mazao ya mafuta ili kujaza pengo katika nchi hizo mbili.
Fursa zipo kwa makampuni ya Misri katika uwanja wa ujenzi., kwani kuna miradi ya kuanzisha njia za kuunganisha Sudan na Eritrea, ambao utekelezaji wake kwa sehemu kubwa ni wa makampuni ya ujenzi ya Misri.
Moja miongoni mwa miradi muhimu zaidi ya pamoja kati ya nchi mbili ni ujenzi wa barabara ya pwani kati ya Misri na Sudan yenye urefu wa kilomita 280.
- Mradi wa barabara ya Qustal na Wadi Halfa yenye urefu wa kilomita 34 ndani ya ardhi za Misri, na kilomita 27 ndani ya ardhi za Sudan.
- Barabara ya Aswan / Wadi Halfa / Dongla.
- Mradi wa unganishaji wa umeme kati ya Misri na Sudan, kwani Misri inatoa kwa Sudan megawati 300 katika hatua yake ya kwanza, na kuongeza megawati 600 kwa hatua ya baadaye, kufikia megawati 3,000.
Kubadilishana biashara:
Kiasi cha kubadilishana biashara kati ya nchi hizo mbili ni dola bilioni moja, kulingana na takwimu za mwaka 2017 na manufaa yanamili kwa Misri kutokana na ongezeko la mauzo ya viwanda vya chakula, vifaa vya ujenzi na nguo, wakati ambapo Misri huagiza kutoka Sudan kwa wanyama hai, ufuta na bidhaa nyingine .. Mauzo ya nje ya Misri kwa Sudan yamefikia hadi dola milioni 550 mwaka wa 2017, aidha Kiasi cha mauzo ya petroli ya Misri kupitia mwaka wa 2017 kilifikia dola milioni 40, na kiasi cha uagizaji wa Misri kutoka Sudan kiliongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, kwani kilifikia dola milioni 450 katika mwaka wa 2017.
Mahusiano ya utamaduni na vyombo vya habari :
Mahusiano ya utamaduni kati ya nchi mbili yameshuhudia nafasi kubwa ya Vyuo Vikuu kwa ajili ya kukuza mahusiano haya, kwa njia ya kubadilishana ziara kati ya maprofesa wa Vyuo Vikuu vya Misri na Sudan kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubadilishana utafiti kati ya Vyuo Vikuu katika nchi hizo mbili, na kuwaruhusu wanafunzi hodari wa VyuoVikuu kufanya ziara kwa Vyuo vya nchi nyingine , na kutoa msaada wa masomo ya Uzamili.
Mahusiano ya vyombo vya habari kati ya nchi hizo mbili yameshuhudia maendeleo mengi, kwani yamesisitiza juu ya ushirikiano wao katika mahusiano kati ya nchi hizi mbili.
Nchi hizi zina idadi kadhaa ya protokoli, itifaki, na mipango ya utekelezaji katika kazi za vyombo vya habari vya pamoja, na miongoni mwake ni :
Tarehe 2/12/2018: Mkataba wa kufanyika mkutano wa pamoja kwa wasomi wa Sudan na wa Misri na vyombo vya habari chini ya jina la "mkutano wa umoja wa Nile." Pia zilikubaliana kuwezesha kazi ya waandishi wa habari katika nchi hizo mbili na uratibu kamili wa vyombo vya habari kati ya nchi hizo mbili katika masuala yote. kijamii
Nchi mbili zimesaini mkataba tarehe Machi, 2011 kwa ajili ya ushirikiano katika sekta ya vyombo vya habari kati ya taasisi kuu na baraza la vyombo vya habari vya nje kwa Jamhuri ya Sudan.
Mkataba katika nyanja ya ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya Serikali ya Jamhuri ya Sudan na Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri (Julai 19, 2003) Ilikuwa kama sisitizo juu ya uhusiano wa ndugu kati ya nchi hizo mbili na kufuatilia utekelezaji wa mkataba wa uelewano uliosainiwa tarehe 8 Julai 2001 na mpango wa utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi hizo mbili.