Misri na Tanzania
Jumapili, Januari 06, 2019
 Misri na Tanzania

Utangulizi

Misri na Tanzania zina ushirikiano mzuri, na hasa kwa kuzizingatia kuwa
Tanzania ni moja ya nchi za bonde la Mto Nile, pia kuna ushirikiano mzuri,
ambapo ziko kamati kuu zenye ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ambapo
kwa kawaida hukutana ili kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.
Ziara za pamoja
1- Tarehe 13/12/2018 Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa ujenzi na
maendeleo ya makazi Dk. Mostafa Madbuli Alifanya ziara nchini Tanzania
kwa ajili ya kushiriki katika sherehe ya kutia saini mkataba wa kuanzisha
mradi wa kuzalisha umeme wa bwawa la Mto"RUFIJI" mradi huo
unafanywa kwa ushirikiano wa makampuni mawili ya ukandarasi, Kampuni
ya kwanza ni "Arab Contractors" na Kampuni ya pili ni "ElSewedy Electric
zote kutoka Misri, kwa gharama za dola za Kimarekani bilioni 9,2 Rais wa
Tanzania Dk.John Maghufuli alimkaribisha Waziri Mkuu wa Misri.
2- Tarehe 4/11/2018 Ujumbe kutoka umoja wa viwanda vya Misri
ukiongozwa na Dk. Sharif Algibali" Rais wa tume ya ushirikiano ya kiafrika
ndani ya Umoja wa Afrika, na kwa kuwashirikisha wanachama thalathini
kutoka mashirika 24 ya Kimisri kutoka pande zote za kiuchumi walifanya
ziara nchini Tanzania kwa lengo la kukuza viwanda vya Kimisri ndani ya
soko la Tanzania.
3-Tarehe 8/1/2018 Agustin Mahiga Waziri wa Mambo ya nje nchini
Tanzania akiongozana na ujumbe mkubwa kati yao ni Waziri wa nchi ofisi
ya Rais wa Zanzibar mheshimiwa Isaa Haji Osii walifanya ziara nchi Misri
na kupokewa na Waziri wa mambo ya nje wa Misri Bwana Sameh shokry.
4- Tarehe 14/8 /2018 Rais wa Misri " Abd Alftaah Alsisi" Alifanya ziara
nchini Tanzania inazingatiwa kama ni ziara ya kwanza kwa Marais wa Misri
tangu mwaka 1968. Rais wa Tanzania D.k John Maghufuli alimpokea
mwenzake wa Misri, na pande zote mbili zilizungumzia masuala
mbalimbali ya Kimataifa .

MIKATABA
Mei 1999 Misri,Tanzania na shirika la " Alfaw" Zilitia saini Mkataba ili
kutekeleza Programu Binafsi kwa " usalama wa chakula " katika mfumo
kuimarisha siasa za "usalama wa chakula " zilizotajwa kama ni Malengo ya
kungamano la mkutano wa Kimataifa wa chakula uliofanyika Jijini
"ROMA" mwaka 1996.
Ushirikiano katika upande wa Ulinzi na Afya
Tarehe 17 /8 /2016 ujumbe uliundwa na Madaktari saba kutoka Chuo Kikuu
cha "Alexandaria" walifanya ziara nchini " Tanzania " na Kisiwa cha "
Zanzibar " katika mfumo wa mkataba uliosainiwa kati ya Chuo Kikuu cha
"Alexandarea " na Chuo Kikuu cha " Mahumbili" kwa lengo la kuimarisha
ushirikiano wa afya na Sayansi kati ya vyuo vikuu hivi viwili ili kufanya"
Upasuaji" kwa watoto.
Ziara hii ilizingatiwa kuwa ni ya tatu katika miaka mitatu mfufulizo kwa
ujumbe wa madaktari kutoka Chuo Kikuu cha" Alexandarea".
Misaada ya kibinadamu
Tarehe 8/12 /2016 Misri ilipeleka misaada kwa waathirika wa tetemeko la
ardhi lililotokea katika eneo la "Kagera" kaskazini mwa Tanzania misaada
hii ilifikia tani 4.5 ikijumuishwa na idadi kubwa ya vifaa vya matibabu na
huduma ya kwanza, misaada hii ilikuwa na thamani ya zaidi dola za
kimarekani 70,000 , uongozi wa Tanzania ulipokea misaada ya kimisri
kupitia ofisi ya Waziri Mkuu wa Tanzania