Mahusiano ya Misri na Togo
Jumatano, Aprili 10, 2019
Mahusiano  ya Misri na Togo

*Historia  kwa ufupi

Mahusiano  ya  kidiplomasia  baina  ya Misri na Togo yalianza  moja kwa moja  baada ya Togo imepata  uhuru  mwaka 1960.  Ambapo  ubalozi  wa kimisri  umekuwepo  nchini  Togo  tangu nchi hiyo ipate uhuru ila(isipokuwa )Togo haina ubalozi nchini Misri. Na mwishoni  mwa  mwaka 2004 Togo  imemteua  balozi wake wa  Libya  kwa  ajili ya kuliwakilisha  taifa lake nchini Misri uwikilishi usio wa kudumu . Na serikali  ya  kimisri  imekubali  hivyo. Nchi mbili hizi  zina  mahusiano imara kwa upande wa kisiasa. Kiasi kwamba  nchi mbili hizo zinashirikiana katika  mitazamo  inayohusiana na maswala ya kikanda na ya kimataifa ukiongezea na Togo  haishiriki  katika siasa zo zote zinazosababisha madhara kwa maslahi ya kimisri. Kama pia Togo  huunga mkono nafasi zinazogombewa na Misri  katika  mahafali (sherehe)  na mashirika ya kikanda na  ya kimataifa.

*Ziara za Pamoja

*mnamo  10-4-2016  raisi wa Togo, Bw. Fur Ganasingaby amezuru  Misri  pamoja na amempokea raisi EL-Sisi, Ambapo wamefanya mazungumzo kwa ajili ya kujadili njia za kuimarisha mahusiano ya pande mbili katika Nyanja mbali mbali  kwa ajili ya kuhakikisha maslahi ya nchi mbili na ya raia wawaili ukiongezea na kuzungumzia maswala ya kiafrika na ya kimataifa ya pamoja na njia za kuimarisha mashirikiano kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii pamoja na kupiga vita ugaidi na umaskini barani Afrika.

Mnamo  4-3-2016 ziara ya makamu wa raisi wa  kimisri wa miradi ya kimikakati na ya kikanda  ,BW, Ibrahim Mihlab  nchini Togo akikubali  mwaliko wa  raisi wa Togo  , BW. Fur Ganasingaby  . Mihlab  amekabidhi barua ya raisi EL-Sisi kwa mwenzake wa Togo, Pande mbili zimefanya mazungumzo kwa ajili ya kujadili  njia za kuimarisha mashirikiano ya pamoja katika Nyanja kadhaa kama vile, usafiri wa baharini, usafiri wa anga,afya,kilimo,nguvu za nishati,makaazi pamja na utalii.

mnamo 12-2-2016 waziri mkuu wa Togo, BW.Komi Sialum Klasu ametembelea Misri kwa ajili ya kushiriki katika shughuli za kongamano la kiafrika mwaka 2016 mjini Sharm ELshekh, Ambapo amemkutana na raisi EL-Sisi na  wamezungumzia njia za kuimarisha mashirikiano ya pande mbili.

Ziara ya Waziri wa mambo ya kigeni wa Togo wa zamani , BW.Koffi Essaw, mshauri wa kisiasa wa raisi Fur  mjini Sharm EL-shekh kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa mawaziri wa maandalizi  kwa ajili ya mkutano wa kilele wa nchi zenye harakati za kutopendelea katika kipindi kutoka 13 Julai hadi 14 Julai mwaka 2009.

 Ziara ya waziri wa utalii wa Togo mjini Kairo katika mwezi wa Machi ya mwaka 2009,Ambapo amemkutana na waziri wa utalii wa kimisri na wametia saini hati ya makubaliano ya mashirikiano ya kiutalii baina ya nchi mbili.

Ziara ya waziri wa nishati na migodi wa Togo mjini Kairo kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa tatu wa kongamano la mawaziri wa nishati wa kiafrika katika  kipindi kutoka 31 Mei ya mwaka 2010 hadi 2Juni ya mwaka 2010.

 Ziara ya mshauri wa kisiasa  wa raisi katika 21-2-2005 kwa ajili ya kuyamaliza mapingo ya kisiasa nchini Togo baada ya kifo cha raisi Iadyama.

Ziara ya  msaidizi wa waziri wa mambo ya kigeni wa maswala ya kiafrika na ya umoja wa kiafrika katika kipindi kutoka 2Novemba  hadi 4 Novemba ya mwaka 2007, Na katika ziara yake amewakutana na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya kigeni wa Togo pamoja na waziri wa afya.

Ziara ya raisi Fur nchini Misri katika mwezi wa Julai ya mwaka 2008 kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa kilele wa umoja wa kiafrika mjini Sharm EL-Shekh.

 Ziara ya balozi ambaye ni msaidizi wa waziri wa mambo ya kigeni wa maswala ya kiafrika na ya umoja wa kiafrika nchini Togo katika kipindi kutoka 21 Oktoba hadi 23 Oktoba ya mwaka 2010,Katika ziara yake hiyo amewakutana na waziri mkuu wa Togo na mkuu wa mahakama ya kikatiba na naibu wa kwanza wa  spika wa bunge ukiongezea na mawaziri wa usalama na wa kiutalii na wa afya, Na katika ziara hii kumefanyika kikao cha mazungumzo ya pande mbili katika wizara ya mambo ya kigeni ya Togo na kikao hiki kimezungumzia njia za kuimarisha mahusiano kati ya nchi mbili pamoja na mitazamo ya nchi mbili kuhusu hali ya mambo katika eneo la Afrika magharibi.

 

*Mahusiano ya kiuchumi

Tarehe 19 ya mwezi wa Febuari ya mwaka 2017 waziri wa anga  , BW. Shariif Fathy na waziri wa usafiri wa Togo, BW. Gunufaham wameshuhudia kutia saini kwa hati mbili za makubaliano baina ya Misri na Togo katika Nyanja za kutoa mafunzo na ubora na usalama  wa anga pamoja na amani.kKatika 10-4-2016 raisi Abdal Fatah EL-Sisi na raisi wa Togo, BW. fFur Ganasingabi wameshuhudia kutia saini protokoli na mipango mine ya mashirikiano ya pamoja.Protokoli hii imezungumzia  eneo baina ya nchi mbili pamoja na mashirikiano katika sekta za ujenzi na makaazi.Na kwa upande wa misri imetiliwa saini na waziri wa mambo ya kigeni,BW. Sameh Shukri  na kwa upande wa Togo imetiliwa saini na waziri wa makaazi na mipango mijini, BW. Kabu Sisanu. Kama pia pande mbili  zimetia saini mipango minne ya utekelezaji ya mashirikiano nayo ni :*

*Mpango wa utekelezaji wa mashirikiano katika uwanja wa michezo kati ya wizara ya vijana na michezo ya Misri na wizara ya habari na utamaduni na vijana na michezo ya Togo kwa upande wa Misri umetiliwa saini na waziri wa vijana na michezo, BW. Khaled Abdal Aziz na kwa upande wa Togo umetiliwa saini na waziri wa habari na utamaduni na vijana na michezo. * Mpango wa utekelezaji wa mashirikiano katika uwanja wa utamaduni kati ya wizara ya utamaduni ya Misri na wizara ya habari na utanmaduni na vijana na michezo ya Togo kwa upande wa Misri umetiliwa saini na waziri wa utamaduni, BW. Halmi EL-Namnam na kwa upande wa Togo umetiliwa saini na waziri wa habari na utamaduni na vijana na michezo. *Mpango wa utekelezaji wa mashirikiano katika uwanja wa habari kati ya mamlaka ya maelezo na wakala wa Togo wa kiutamaduni kwa upande wa Misri umetiliwa saini na mkuu wa mamlaka ya maelezo, balozi, BW. Salah Abdal Sadk na kwa upande wa Togo umetiliwa saini na waziri wa habari na utanmaduni na vijana na michezo. *Mpango wa utekelezaji wa mashirikiano katika uwanja wa idhaa na televisheni kati ya umoja wa idhaa na televisheni wa Misri na wizara ya habari na utamaduni na vijana na michezo ya Togo, kwa upande wa Misri umetiliwa saini na mkuu wa umoja wa idhaa na televisheni, BW. Asam EL—Amir na kwa upande wa Togo umetiliwa saini na waziri wa habari na utamaduni na vijana na michezo. Shirika la EL-Nasr la uagizaji na usafirishaji linafanya kazi kama upande wa tatu. Ambapo linasafirisha mazao ya msingi ya kilimo ya Togo kama vile, kahawa na kakao kwa Ulaya. 

 

*Tume ya pamoja

Tume ya pamoja imeanzishwa baina ya nchi mbili katika mwezi wa Febuari ya mwaka 1988. Na imefanya kikao cha kwanza katika mwezi wa Febuari ya mwaka 1988 mjini Kairo. Aidhaa imefanya kikao cha pili katika mwezi wa Januari ya mwaka 1991 mjini Lumi.

 

*Wigo wa kufungamana baina ya nchi mbili 

*Mkataba kwa ajili ya kufanyika tume ya pamoja baina ya nchi mbili.

* Mkataba kwa ajili ya mashirikiano ya kiutamaduni umetiliwa saini katika 17-3-1964 ukiongezea na kumetimia kutia saini protokoli ya utekelezaji kuhusu miaka mitatu, mwaka 1991 na mwaka 1992 pamoja na mwaka 1993.  * Mkataba kwa ajili ya mashirikianao ya kibiashara umetiliwa saini katika 17-3-1964.  * Mkataba kwa ajili ya mashirikiano ya kiuchumi nay a kiufundi umetiliwa saini katika 27-1-1981.  *Protokoli  kwa ajili ya mashirikiano ya kijeshi umetiliwa saini katika 18-4-1981.     * Mkataba kwa ajili ya mashirikiano ya kiufundi umetiliwa saini  pamoja na sanduku la kimisri la mashirikiano ya kiufundi  na  bara la Afrika katika 6-2-1988. * Mkataba kwa ajili ya usafiri wa baharini umetiliwa saini katika 5-2-1988. * Hati ya makubaliano katika uwanja wa mashirikiano ya kiutalii.

 

*Mahusiano  ya kiutamaduni na ya kiufundi baina ya nchi mbili

Wajumbe 10 wa Azhar Shariif wapo Togo wanafanya kazi katika uwanja wa ulinganiaji wa kiislamu na kufundisha lugha ya kiarabu na quran katika shule za kiislamu katika kanda mbali mbali nchini Togo. Aidhaa Azhar Shariif  inatosheleza nafasi kadhaa za masomo za kila mwaka kwa wanafunzi wa Togo  kwa ajili ya kusoma katika vyuo vya AzharShariif. Vile Vile hutolewa mwito Azhar Shariif kwa ajili ya kushiriki katika kozi zinazoandaliwa na wakala wa kimisri wa mashirikiano kwa aili ya maendeleo katika Nyanja mbali mbali kama vile, polisi ,kilimo,mahakama,afya,uaguzi,habari na diplomasia  ukiongezea na kuwasaidia ndugu wa Togo kutokana na kutoa misaada na zana za kimatibabu na za kiafya na za uchukuzi.