Misri Na Visiwa vya Komoro
Jumatatu, Machi 25, 2019
Misri Na Visiwa vya Komoro

Historia

Misri na Komoro zina mahusiano bora katika nyanja zote kwa mtazamo wa uanachama wa nchi hizo mbili katika Umoja wa Afrika , Umoja wa  nchi za Kiarabu na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu, licha ya mahusiano ya kiutamaduni na kielimu  ambayo yanafanya wanafunzi wengi wa Komoro tangu makumi ya miaka wanakwenda Misri ili kusoma katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar au katika vyuo vikuu vya Misri.       

  Kama Misri ilivyo weka umuhimu wakutoa msaada  wa kiufundi kwa viongozi wa Komoro katika nyanja mbalimbali kupitia Shirika la Misri la Ushirikiano kwa ajili ya maendeleo lililo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje.. Komoro inaendelea kuiunga mkono  Misri  kisiasa katika vikao vyote,ni sawa viwe  vya kiafrika, Kiarabu au kimataifa.                                

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Misri na Jamhuri ya Komoro yanarejea  tangu 1976, wakati uamuzi wa Misri ulipotolewa  Julai 26 ili kubadilishana uwakilishi wa kidiplomasia. Hata hivyo, mahusiano yaliongezeka baada ya mwanzo wa milenia mpya, Nchi hizo mbili zilifanya kazi ili kuimarisha mahusiano ya pamoja, hasa katika ngazi ya kiuchumi, baada ya kujiunga na COMESA, ambayo ni moja ya nguzo za Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika, pamoja na ushiriki wao katika mashirika ya kimataifa mbalimbali kama Umoja wa Afrika, Shirika la Mkutano wa Kiislamu na Umoja wa nchi za Kiarabu,pamoja na jitihada zao  za kubadilishana na kuongeza ushirikiano katika nyanja zote tisa.               

Mahusiano ya Kisiasa

Maono ya nchi hizo mbili yanakwenda sambamba katika maswala mbalimbali na masuala ya kanda na bara la Afrika, ziara za pamoja kati ya viongozi wa nchi mbili zinaonesha shauku ya kuendeleza na kuimarisha mahusiano katika nyanja zote.                                           

Mahusiano ya Kijeshi

Misri ilishiriki na idadi ya watazamaji wa kijeshi (watazamaji watatu) kama mchango kutoka Misri katika juhudi za kufikia amani.                  

Chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa katika Visiwa vya Komoro kuanzia mwaka wa 1997-1999