Misri
Jumanne, 1 Januari 2019
Misri

 

Mahali na eneo

Mahali pa kifalaki:

Jamuhuri ya Kiarabu ya Misri iko kati ya mistari mbili ya latitudo 22 ° na 32 ° Kaskazini mwa Ikweta, na kati ya mistari miwili ya longitudo 24 ° na 37 ° Mashariki mwa mstari wa Greenwich.

 

Mipaka ya kijiografia:

Misri iko  Kaskazini Mashariki mwa bara la Afrika .. inapakana Kaskazini na Bahari ya Mediterania kwa pwani yenye urefu wa kilomita 995, na inapakana Mashariki na Bahari ya Shamu kwa pwani inayofikia urefu wa kilomita 1941, na inapakana Kaskazini Mashariki na Palestina na Israeli kwa urefu wa kilomita 265, na inapakana Magharibi na Libya  kwa urefu wa kilomita 1115. Na inapakana Kusini na Sudani kwa urefu wa kilomita 1280.

 

Eneo: eneo la Jamhuri ya Kiarabu ya Misri linafikia takriban kilomita za mraba 1.002.000  na eneo linalokaliwa ni 78990 km2, kwa asilimia 7.8 kwa eneo lote.

 

Hali ya hewa:

Hali ya hewa ya Misri inaathiriwa na sababu kadhaa, na sababu muhimu zaidi ni eneo, umbo la ardhi (au mandhari ya ardhi), mashinikizo madogo ya hewa na maeneo ya mkusanyo wa maji, sababu hizo zote zilisaidia kuigawanya Misri katika majimbo kadhaa ya hali ya hewa, ambapo Misri iko katika eneo kavu la kitropiki isipokuwa kingo za Kaskazini zinazoingia kwenye eneo lenye hali nzuri ya hewa ambalo lina hali ya hewa sawa na jimbo la Bahari ya Mediterania lenye sifa ya joto na ukame katika miezi ya majira ya joto na kwa wastani wakati wa majira ya baridi, na mvua mdogo.

Hali ya hewa ya Misri inaweza kugawanywa katika misimu miwili: msimu wa joto kavu ambayo ni kati ya miezi ya Mei na Oktoba, na msimu wa baridi wenye mvua ndogo ambao ni kati ya Novemba na Aprili.

 

Hali ya joto:

Kiwango cha chini cha joto kinafika nyuzi joto  9 hadi 11 katika mwezi wa Januari, na kiwango cha juu cha joto ni nyuzi  joto 20 hadi 24.

Kama ilivyo katika miezi ya Julai na Agosti, kiwango cha chini  cha joto ni kati ya nyuzi joto 21 hadi 25 na kiwango cha juu ni  nyuzi joto 37 hadi 42.

 

Lugha:

Lugha rasmi ya nchi ni lugha ya Kiarabu, pamoja na Kiingereza na Kifaransa katika maeneo ya kibiashara.

 

Idadi ya watu:

Idadi ya watu ilifikia watu milioni 104.2, Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2017.

 

Sarafu:

Poundi ya Misri.

 

Sikukuu ya kitaifa:

Julai 23 kila mwaka, ambayo ni inaambatana na kumbukumbu ya mapinduzi ya Julai 23, 1952.

 

Pendera ya Misri:

Pendera ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri inaundwa na mistatili mitatu kwa mlalo, mstatili wa juu wenye rangi nyekundu, wa katikati wenye rangi nyeupe na wa chini wenye rangi nyeusina katikati ya pendera kuna Tai mwenye rangi ya dhahabu.

Mji mkuu:

Kairo ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na unazingatiwa ni mji mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu na barani Afrika kwa  idadi ya watu. Mji wa Kairo ulijengwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, Kairo kuu ni makao makuu ya serikali nchini Misri, na alama zake za kale mashuhuri zaidi ni, Peramidi, Mnara wa Kairo, Ngome ya Salah el-Din, Msikiti wa Al-Azhar, Msikiti wa Sultan Hassan, Ngome ya Babeli, Makumbusho ya Kiislamu, Makumbusho ya Kikoptiki .. na mengine.

 

Miji muhimu zaidi:

Kairo, Giza, Alexandria, Port Said, Luxor, Aswan, Sueiz, Hurghada, Sharm El-Sheikh, Marsa Matrouh na Marsa Alam.

Uchumi wa Misri ni moja ya uchumi unaotekelezeka zaidi katika Mashariki ya Kati na Afrika. Uchumi huu unategemea misingi tofauti kama kilimo, viwanda, utalii na huduma kwa kiasi kinacholingana.  Sekta ya kilimo ni moja ya vyanzo muhimu zaidi vya mapato ya kitaifa, ambapo Misri na ustaarabu wake unaambatana na kilimo, na eneo la kilimo linafikia ekari  milioni 10, na watu wanaofanya kazi katika sekta hii wanafikia takriban asilimia 30 ya jumla wa wafanyakazi. Na sekta hii inachangia asilimia 8.14 ya pato la kitaifa. Mauzo ya nje ya kilimo huchangia asilimia 20 takriban ya jumla ya mauzo ya bidhaa.

Wamisri wa kale walijua kazi nyingi za viwanda kama vile uchimabji wa madini kama shaba, dhahabu na fedha na namna ya kuzitengeneza. Pia walijua utengenezaji wa mashine, vifaa vya kilimo na kijeshi na utengenezaji wa meli, na kazi hizi ziliendelea kuendelezwa kulingana na kila zama. Mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa, Muhammad Ali alianzisha sera kubwa ya viwanda, kwa hivyo alianzisha viwanda vipya, alijali  zaidi viwanda vya nguo na vya kijeshi, na alianzisha viwanda vya kutengeneza meli.

Misri imejulikana katika historia yake kama muelekeo wa watalii tangu "Herodotus" alipotembelea katika historia ya kale, na kushangazwa kwake na  tofauti kubwa iliyopo kati ya nchi yake na Misri, Misri imebaki hivyo wakati wote wa historia yake ya kale na ya kisasa, hata hivyo ugunduzi wa athari za Mafarao umeongeza maridadi yake pamoja na athari zake za kipekee za kidini na kistaarabu, na vilevile eneo lake la kijiografia katikati ya ulimwengu, hali yake nzuri ya hewa katika majira ya joto na ya baridi, pwani zake, kwa hivyo Misri imekuwa ikijulikana kwa aina zake za wazi katika bidhaa zake za utalii.

Licha ya aina nyingi za Utalii na umilki wa Misri kwa mambo mengi , Utalii wa kitamaduni ni aina inayowavuta watalii sana kutokana na kile ambacho Misri inamiliki kwani ina theluthi ya makumbusho yanayojulikana katika ulimwengu wote.

Pamoja na Utalii wa kitamaduni na akiolojia, aina mpya za uatalii zimetokea kama Utalii wa burudani, Utalii wa pwani, Utalii wa kidini, Utalii wa matibabu, Utalii wa mazingira, Utalii wa michezo, Utalii wa safari, Utalii wa jangwani na utalii wa mashua, pamoja na utalii wa matamasha, makongamano na maonesho.