Algeria
Alhamisi, Januari 03, 2019
Algeria

Al-Jumhurīyah al-Jazā’irīyah ad-Dīmuqrāṭīyah ash-Sha’bīyah

Kaulimbiu ya taifa: Kiarabuمن الشعب و للشعب:
;Mapinduzi ya watu kwa ajili ya watu")

Wimbo wa taifa: Kassaman (qasaman bin-nāzilāt il-māḥiqāt)
(Arabic: Twayamini kwa radi inayoharibu)
Lokeshen ya Algeria
Mji mkuu Algiers [1]
36°42′ N 3°13′ E
Mji mkubwa nchini Algiers
Lugha rasmi Kiarabu, Kiberber
Serikali Demokrasia Jamhuri
Rais Abdelaziz Bouteflika

Waziri Mkuu Abdelmalek Sellal
Uhuru Tarehe kutoka Ufaransa
5 Julai 1962 [2]

Eneo 2,381,741 km² (10th)
- Jumla
- Maji (%) kidogo sana
Idadi ya watu

- 2015 kadirio
- Msongamano wa watu
39,500,000 [1] (ya 35)
{{{population_density}}}/km² (ya 208)
Fedha Dinari ya Algeria (DZD)
Saa za eneo
- Kiangazi (DST) CET (UTC+1)
CET (UTC(hawajali))
Intaneti TLD .dz
Kodi ya simu +213
-

Algeria (pia: Aljeria ; kwa Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir; kwa Kiberber: Dzayer, au kwa jina
rasmi Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria" ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi.
Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger,
Libya na Tunisia.

Ramani ya Algeria
Algeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa
la Sahara.

Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa
lugha ya Kiarabu.

Yaliyomo
1 Jiografia
2 Hali ya hewa
3 Historia
3.1 Historia ya kale
3.2 Uvamizi wa Waarabu
3.3 Ukoloni wa Wafaransa
4 Wilaya za Aljeria
5 Miji
6 Watu

Jiografia
Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa, Sahara iko upande wa kusini. Asilimia 20 za eneo la Algeria
upande wa kaskazini ni makao kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya ni pwani ya Mediteranea
na milima ya Atlas.

Atlas inapanda hadi kimo cha mita 2,308 juu ya UB.

Sahara inaanza kusini kwa Atlas na kanda yenye nyasi chache, halafu inafuata eneo la matuta
ya mchanga pasipo mimea yote. Kusini kwake tena ni nyanda za juu ambazo ni hasa maeneo
ya miamba mitupu.

Kusini kabisa kuna milima ya Ahaggar inayopanda hadi mita 2,918.

Mito ya kudumu iko kaskazini tu, sehemu za pwani. Mabonde ya mito ya ndani ni makavu,
isipokuwa baada ya mvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa.

Hali ya hewa

Kanda la kaskazini lina hali ya hewa inayoathiriwa na Bahari ya Mediteranea. Huko halijoto
kwenye mwezi Agosti ni 25 °C na 12 °C wakati wa Januari.

Kwenye sehemu za juu kuna baridi na hata barafu kwenye majira ya Januari lakini joto ni kali
zaidi wakati wa Julai/Agosti.

Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C
katika siku moja. Wakati wa joto halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka
chini ya °C kwenye saa za usiku.

Mvua ni haba mno: kuna miaka mfululizo bila tone hata moja. Katika milima ya Ahaggar kuna
usimbishaji kidogo kutokana na ukungu, kwa hiyo miti kadhaa na mimea mingine iko.

Historia
Makala kuu: Historia ya Algeria
Historia ya kale
Historia inayojulikana ilianza na Waberber ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi
asilia.

Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye
pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwa Karthago uliopanua utawala wake
hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini).

Kumbe Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.

Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma, hivyo
wakapata uhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala
eneo la Algeria moja kwa moja.

Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia
zililimwa huko.

Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wa Algeria na Dola la Roma
lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu katikati ya karne ya 7.

Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha
milki yao kwa muda wa karne moja.

Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7
uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.

Uvamizi wa Waarabu
Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya
Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada ya uhamisho wa serikali
ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski, Waumawiya walikaza jitihada huko Afrika ya
kaskazini.

Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu
ulikuwa kitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Algeria ya leo walirudishwa na Waberber
Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika
ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Algeria na Moroko) zilikuwa chini ya
utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu
wakasaidiana na Waarabu.

Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa
lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.

Ukoloni wa Wafaransa
Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na
utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya miaka 1830 na 1962.

.