Angola
Alhamisi, Januari 03, 2019
Angola

Angola ni nchi kubwa iliyopo upande wa kusini wa bara la Afrika ikipakana na Namibia, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo, na Zambia. Upande wa magharibi kuna pwani ndefu ya Bahari
Atlantiki. Mkoa wa Kabinda umetenganika na sehemu nyingine za nchi na unapakana na
Jamhuri ya Kongo pia.

Angola ni nchi tajiri kwa mafuta na madini: almasi ndiyo muhimu zaidi. Lakini nchi ni maskini
kutokana na vita vya miaka 29; kwanza vita vya kupigania uhuru dhidi ya Ureno iliyofuatwa na
vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 2002.

Nchi yenyewe hasa ni ya kidemokrasia na inajulikana kama Jamhuri ya Angola (kwa Kireno:
República de Angola, kwa matamshi ya IPA: /ʁɛ.'pu.βli.kɐ dɨ ɐ̃.'ɣɔ.lɐ/; kwa lugha za wenyeji:
Repubilika ya Ngola).

Yaliyomo
1 Asili na historia ya jina 'Angola'
2 Jiografia
3 Maeneo ya Angola
4 Historia
4.1 Dola la Kongo
4.2 Dola la Lunda
4.3 Dola la Kasanje
5 Siasa
6 Watu
7 Tazama pia
8 Tanbihi

9 Viungo vya nje
9.1 Serikali
9.2 Habari
9.3 Maoni
9.4 Radio na Muziki
9.5 Maelekezo
9.6 Utalii
9.7 Mambo mengine
Asili na historia ya jina 'Angola'
Jina Angola linatokana na neno la lugha ya Kibantu "N’gola", ambalo lilikuwa jina la kiongozi wa
ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili.

Jiografia
Makala kuu: Jiografia ya Angola
Maeneo ya Angola
Ramani ya Angola na Mikoa iliohesabiwa
Makala kuu: Mikoa ya Angola
,
Makala kuu: Manispaa za Angola
Angola imegawiwa katika mikoa 18 (províncias) na manispaa 162 (municípios).
Mikoa ni:

1 Bengo
2 Benguela
3 Bié
4 Kabinda
5 Cuando Cubango

6 Cuanza Norte
7 Cuanza Sul
8 Cunene
9 Huambo
10 Huila
11 Luanda
12 Lunda Norte
13 Lunda Sul
14 Malanje
15 Moxico
16 Namibe
17 Uige
18 Zaire
Historia
Makala kuu: Historia ya Angola
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK kutoka kaskazini walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo
na uhunzi.

Kuanzia karne ya 14, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, kwa mfano Dola la Kongo,
Dola la Lunda na Dola la Kasanje.

Dola la Kongo
Dola la Kongo lilikuwa ufalme ulioenea ndani ya nchi za leo za Angola, Kongo (Kinshasa) na
Kongo (Brazzaville).
Ulianzishwa katika karne ya 14 ikadumu hadi karne ya 17.
Mtawala wake alikuwa na cheo cha "Mwene Kongo" au "Manikongo" wa kabila la Bakongo.

Ufalme huo umejulikana zaidi kihistoria kwa sababu ya mawasiliano yake ya kimataifa. Katika
karne ya 15 meli za Wareno zilifika mwambaoni mwake.
Wakati wa kukutana na Wareno Ufalme wa Kongo labda ulikuwa na eneo la km² 300,000
ukaunganisha robo ya magharibi ya Kongo (Kinshasa) pamoja na sehemu za Angola na Kongo
(Brazzaville).

Manikongo mbalimbali walijenga uhusiano na Ureno na Kongo ilikuwa taifa la kushikamana na
Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kile taarifa mbalimbali ziliandikwa
zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo.
Manikongo alikaa katika mji wa M'banza-Kongo.
Baada ya wafalme kuwa Wakristo Wakatoliki na kujengwa kwa kanisa kuu, jina la "São
Salvador do Congo" (kwa Kireno: "Mwokozi Mtakatifu wa Kongo") lilikuwa kawaida kwa mji
mkuu wa milki.
Ufalme ukawa na majimbo, wilaya na vijiji. Majimbo yalikuwa saba ya Mpemba, Nsundi,
Mpangu, Mbata, Mbamba na Soyo.
Kwa mikataba ya baadaye falme za Kakongo, Loango na Ngoy likatokea shirikisho ya sehemu
nne.

Dola la Lunda
Dola la Lunda lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1600 hadi 1850 hivi kandoni kwa mto
Kasai, mpakani kwa nchi za kisasa za Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Dola la Kasanje
Dola la Kasanje lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1620 hadi 1910 hivi kandoni kwa mto
Kwango, upande wa kaskazini wa nchi ya kisasa ya Angola. Lilianzishwa na viongozi kutoka
Dola la Lunda.
Mwaka 1910 lilivamiwa na Wareno na kuingizwa katika koloni lao la Angola.

Siasa
Kaulimbiu ya Angola ni "Virtus, Unita Fortior", kumaanisha "umoja utupe nguvu"

Watu

Mwanamke wa Angola pamoja na watoto nje ya kliniki.
Wakazi wengi ni Waafrika, hasa wa makabila ya Waovimbundu (37%), Waambundu (25%) na
Wakongo (13%). Machotara ni 2%, Wachina 1,4% na Wazungu 1%.

Ingawa lugha za Kibantu zinaongoza, na 6 kati yake zina hadhi ya lugha ya taifa, lugha rasmi ni
Kireno.

Upande wa dini, inakadiriwa kuwa zaidi ya nusu ni Wakatoliki na robo ni Waprotestanti wa
madhehebu mia tofauti.