Gambia
Jumapili, Desemba 30, 2018
Gambia

Kaulimbiu ya taifa: Progress, Peace, Prosperity (Maendeleo, Amani, Ustawi)
Wimbo wa taifa. (Kwa Gambia nchi yetu)
Lokeshen ya Gambia

Mji mkuu ( Banjul)
(13°28′ N 16°36′ W)
Mji mkubwa nchini (Serrekunda)
Lugha rasmi (Kiarabu)
Serikali ( Jamhuri)
Rais (Adama Barrow)
Uhuru ( Kutoka Uingereza 18 Februari 1965)

{Eneo ( 10,689 km² (ya 164
Jumla 11.5)
Maji (%)}-
-

Idadi ya watu (ya 150)1,882,450}

- [[]] kadirio {171.1/km² (ya 74)
- 2013 sensa
- Msongamano wa watu

Fedha {Dalasi (GMD)}
Saa za eneo
- Kiangazi (DST) { GMT (UTC)(UTC]

Intaneti TLD {.gm}
Kodi ya simu {+220}
-

Ramani ya Gambia.
Gambia (jina rasmi: Republic of The Gambia) ni nchi ndogo kabisa ya Afrika bara. Eneo
lake lote linazungukwa na Senegal kwa kufuata mwendo wa mto Gambia hadi Bahari ya
Atlantiki.

Kimsingi nchi yote ni maeneo ya kandokando ya mto huo; urefu ni takriban km 500,
upana kati ya 10 na 50.

Yaliyomo
1 Historia
2 Wakazi
3 Uchumi

Historia
Zamani eneo la Gambia lilikuwa sehemu ya Dola la Mali na Dola la Songhai.

Nchi kama ilivyo leo imepatikana kutokana na mvutano kati ya Uingereza na Ufaransa
wakati wa ukoloni.

Mwanzoni Uingereza ulitafuta tu njia ya maji kwa ajili ya biashara, bila kujali utawala wa
nchi.

Mapatano kati ya Ufaransa na Uingereza baada ya vita vya Napoleon Bonaparte
yaliimarisha hali hiyo. Wafaransa walichukua eneo lote kubwa la Senegal, na
Waingereza ile kanda ndogo ndani ya Senegal.

Tangu uhuru wa nchi zote mbili palikuwa na mpango wa kuziunganisha kwa njia ya
shirikisho lililoanzishwa mwaka 1982 lakini Gambia ilitoka katika mapatano hayo mwaka
1989.

Hadi mwaka 1994 Gambia ilifuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi lakini mwaka
ule uasi wa wanajeshi ulipindua serikali na kuwa chanzo cha utawala wa Yahya
Jammeh aliyekuwa kiongozi, kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya kijeshi, baadaye
kama rais aliyechaguliwa mwaka 1996 na kuchaguliwa tena miaka 2001, 2006 na 2011.
Isipokuwa mwaka 2001 wapinzani na watazamaji wa nje walilalamika ya kwamba kura
hazikuwa huru.

Mwaka 2013 Jammeh alitoa Gambia katika Jumuiya ya Madola kama chombo cha
ukoloni mamboleo.

Mwaka 2015 Jammeh alitangaza Gambia kuwa nchi ya Kiislamu.

Katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 vyama vya upinzani viliungana, na mgombea
wao Adama Barrow alishinda, ilhali Jammeh awali alikubali kushindwa, lakini baada ya
siku nane alitangaza ya kwamba alitaka kubatilisha matokeo na kuwa na uchaguzi

mpya.[1]

Wananchi walianza kukimbilia nchini Senegal.

Tarehe 19 Januari 2017, rais mteule aliapishwa katika ubalozi wa Gambia huko Dakar,
halafu wanajeshi wa Senegal, Nigeria na Ghana walivamia nchi ili kumuondoa
madarakani kwa idhini ya Umoja wa Mataifa.

Tarehe 21 Januari Jammeh alikubali kuachia.

Wakazi
Wakazi wa nchi ni hasa wa kabila la Wamandinka, halafu Wafulani na Wawolof, jumla
milioni 1.9 hivi.

Makabila ya Gambia
asilimia Kabila
42 % Wamandinka
18 % Wafula
16 % Wawolof-Waserer
10 % Wadiola
9 % Waserahuli
1 % Wamanjago
1 % Waaku
0,4 % Wabamana
0,9 % wengine
Namba za mwaka 2003
Lugha rasmi ni Kiarabu, si tena Kiingereza (kuanzia mwaka 2016).

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 90% za wakazi, Ukristo (hasa Kanisa Katoliki)
na 8%, wakati wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 2%.

Uchumi
Uchumi unategemea kilimo, uvuvi na hasa utalii. Mwaka 2008, thuluthi moja ya
wananchi hawakuwa na kipato cha $ 1.25 kwa siku.