Ghana
Jumapili, Desemba 30, 2018
Ghana

Ghana

Ghana au Jamhuri ya Ghana ni Jamhuri ya Afrika ipo kwenye pwani ya kaskazini ya Ghuba ya Guinea Afrika Magharibi. Imepata uhuru wake kutoka  kwa Muingereza mwaka 1957. Jina lake la zamani lilikuwa Pwani ya dhahabu. Jina lake la sasa imeitwa kama jina la nchi ya kihistoria inayojulikana kama Himaya ya Ghana, ingawa haiingi ndani ya mipaka ya nchi hizo.

Mahali

Jamhuri ya Ghana ipo Afrika Magharibi ambapo upande wa Kusini inapakana na Ghuba ya Guinea na mipaka yake kwa upande wa Mashariki inashirikiana na Togo, na upande wa Magharibi inashirikiana na Ivory coast na upande wa kaskazini inashirikiana na Burkina Faso.

Jiografia

Ardhi ya Ghana ni ya tambarare zaidi  ambapo tambarare imeenea kusini na kaskazini. Ama katikati ni ufuo wa mchanga ulionyanyuka katika baadhi ya maeneo yake hadi mita mia sita na pia Mashariki. Mito yake maarufu zaidi ni Volta nyeupe , Volta nyeusi na Awati na limejengwa Bwawa la Volta ambalo ni moja wapo ya miradi maarufu zaidi ya maendeleo nchini Ghana.

Hali ya hewa

Hali ya hewa ya Ghana ni mchanganyiko kati ya hali ya hewa ya kitropiki na orbital.

Mji mkuu wa Ghana

Accra ni mji mkuu wa kisiasa wa Ghana ambapo ni moja wapo ya miji mikubwa ya nchi na pia unazingatiwa kuwa ni  kituo cha kiuchumi na kiutawala na vilevile ni mji wa mawasiliano makuu nchini Ghana ambapo mji huu upo kwenye pwani ya kaskazini ya Ghuba ya Guinea na mji huu una vifaa vingi vya usafirishaji kama reli na uwanja wa ndege wa kimataifa mji huu ni maarufu kwa viwanda vingi, ambavyo vilivyo  muhimu zaidi ni vya utengenezaji wa matofali pia usindikaji wa almasi na kuni, na mji huu unajumuisha   Chuo Kikuu cha Ghana huko, Lejeune, katika makala hii tutatoa maelezo mafupi ya mji mkuu wa Ghana.

Sarufu ya nchi

Sarufu ya Ghana  ni Ghanaian cedi  yenye alama ya GHC.

Lugha

Lugha rasmi nchini Ghana ni kiingereza na kuna lugha zingine kama Toi, Hausa, na Pidgin.

Idadi ya watu

Idadi ya watu wa Ghana hivi sasa inafikia 29,694,224 kwa mwaka 2018 kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya umoja wa mataifa.

Bendera ya nchi

Bendera ya kitaifa ya Ghana inajumuisha rangi tatu. Bendera ina mistari iliyochorwa kwa kulala ambayo ni nyekundu, manjano na kijani pamoja na nyota nyeusi yenye pembe tano katikati ya mstari wa manjano.

Mfumo wa utawala

Jamhuri ya katiba, na mpaka wa bunge ambapo nguvu ya kisheria ipo mkononi mwa bunge la Ghana, baraza Kuu lipo mkononi mwa Seneti ya Ghana na Baraza la chini lipo mkononi mwa Baraza la Wawakishi la Ghana na kauli mbio yao ya kitaifa ni : Muungano na Haki.

Rais wa Jamhuri ya Ghana

Nana Akufo Addo

Sikukuu ya kitaifa

Jamhuri ya Ghana inaadhimisha siku ya uhuru machi 6 kila mwaka

Miji muhimu zaidi katika Jamhuri ya Ghana

Kumasi, Tamale, Tema, Takoradi na pwani ya cape. Na Ghana imegawanywa katika majimbo 10 na majimbo hayo yamegawanywa katika wilaya 216 na majimbo hayo ni:

Jimbo la Ahafo

Jimbo la Accra Kuu

Jimbo la kati

Jimbo la Mashariki

Jimbo la kaskazini

Jimbo la Magharibi

Jimbo la Mashariki ya juu

Jimbo la Magharibi ya juu

Jimbo la Volta

Jimbo la Ashanti

Historia ya Ghana

Hapo zamani ilijulikana kama Pwani ya dhahabu, ilikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza tangu (1314 AH -1896 BK) na ilipata uhuru wake katika mwaka (1377 AH- 1957 BK) baada ya ukoloni uliodumu zaidi ya miaka sitini. ilikuwa koloni la kwanza ambalo lilipata uhuru wake katika Afrika Magharibi.

Uhuru wa Ghana mwaka 1957 ulikuja baada ya maandamano ya kitaifa yaliyoongozwa na Kwame Nkrumah Rais wa kwanza wa Jamhuri huru ya Ghana tangu kumalizika vita vya pili vya dunia na kuenea wimbi la uhuru wa kitaifa kati ya nchi zilizo tawaliwa barani Asia na Afrika. Harakati za uhuru wa kitaifa nchini Ghana zilianza na mkutano wa Umoja wa Pwani ya dhahabu ulioongozwa na Nkrumah  mwaka 1947 baada ya kurudi kwake kutoka Uingereza ambapo ilisababisha kukamatwa kwake. Na baada ya kuachiliwa kwake , aliunda chama cha wananchi ili kufikia serikali ya kujitegemea  ya Ghana. Na chama kilishinda uchaguzi wa Manispaa uliofanywa mwaka 1950. Na Nkrumah akawa Waziri Mkuu wa Pwani ya Dhahabu  ( Ghana ) mwaka 1952.

Sera ya mambo ya nje ya Ghana

Sera ya nje ya Ghana ni pamoja na  wito wa Afrika ya umoja kufikia umoja wa kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa nchi za Afrika. Inaweza kusemwa kuwa uzinduzi wa umoja wa Afrika katika mwaka wa 2001 ilikuwa tu kurudi kwa mradi wa Afrika ambao uliongozwa na maono ya  Rais wa kwanza wa Ghana DK. Kwame Nkrumah. Ili kuonesha kuunga mkono maoni haya ya umoja , katiba ya Jamhuri ya Ghana ilirekebishwa katika utawala wa Rais Nkrumah kwa ajali ya kuandaa misingi ya kuondoa sehemu ya uhuru wa nchi hiyo, kwa ajili ya muungano kati ya Ghana, Guinea na Mali.

Uchumi wa Ghana

Idadi kubwa ya watu nchini wanafanya kazi ya kilimo. Na Kakao inazingatiwa ni mojawapo ya mazao yake maarufu ambapo imekuwa mstari wa mbele katika orodha ya mauzo ya nje tangu nusu karne. Pamoja na hayo kuna mazao kama : Kahawa, Mitende ya mafuta, Mpira, Mananasi, Mchele, Mihogo na mmea wa Yam, Idadi ya watu pia ni wachungaji na wafugaji wa ng'ombe katika maeneo yenye nyasi za Savannah. Pia uchumi wake unategemea  uuzaji wa dhahabu nje na mbao zinazofaa kwa kazi ya fanicha na ujenzi. Vile vile inatoa Almasi, Nikeli na Bauxite. Viwanda vingi vimeenea huko kama vile: vya alumini, nguo na kemikali.

Moja ya rasilimali muhimu zaidi za kiuchumi za Ghana ni utengenzaji wa dhahabu. Hapo zamani, Ghana ilikuwa inajulikana kama " Pwani ya dhahabu" kwa sababu ni moja ya nchi maarufu katika uzalishaji na uuzaji wa nje wa madini ghali na adimu; kama vile Almasi, Dhahabu, Manganizi, Buxite na Chuma . na hii inafanya kutazamwa kwa makini na  wawekezaji wengi wa nje na mabepari wa kigeni ambao wanakwenda kuwekeza ndani yake. Na nchi hiyo inachukua nafasi ya kumi ulimwenguni katika uzalishaji wa dhahabu.

Maeneo muhimu zaidi ya utali nchini Ghana

Jumba la makumbusho la kitaifa la Ghana.

Mji wa Accra : maeneo maalumu ya utalii ya Ghana katika mji mkuu wa Accra ambapo kuna makumbusho ya kitaifa ya Ghana , Chuo cha Sanaa na sayansi cha Ghana, Maktaba kuu, ngome ya kikristo ya burg, Jengo la kitaifa la Ghana, Makao ya Serikali, ukumbi wa michezo wa kitaifa, Mnara, Ahini Djan, kituo cha utamaduni cha kitaifa cha Accra, makumbusho ya Kwame Nkrumah ambayo yapo katikati ya Accra, pamoja na kituo cha mikutano ya kimataifa cha Accra.

Mji wa Kumasi

Mji wa Kumasi : ni moja wapo ya miji iliyoko Kusini- katikati ya nchi. Mji huu ni mbali na mji mkuu kwa takriban kilomita 250. Mji huu una sifa ya misitu kwa hivyo huitwa " Bustani ya mji " kwa sababu ya idadi kubwa ya mimea, maua na waridi huko, ambayo inampa mgeni mtazamo mzuri wa mji. Pia inajulikana kwa  milima mingi iliyofunikwa na miti.

Ngome ya pwani ya cope

Ngome ya pwani cape : Ngome hii inazingatiwa kuwa ni moja ya vituo muhimu kwa uhamiaji wa watumwa wakati nchi ilipokuwa ikitawaliwa na ukoloni wa Uingereza. Ndani yake kuna athari kwenye kuta kwa rangi ya kijani na hizi ni athari za minyororo ambayo watumwa walikuwa wakifungwa kwa maandalizi ya kusafirishwa kwao. Ngome hiyo ndani yake ni giza na nje yake ni yenye saruji nyeupe.

Ngome ya El- Mina

Ngome ya El- Mina : Ngome hii ipo kusini mwa Ghana, ilijengwa na Wareno mwaka wa 1482 AD, ambapo ilikuwa kituo cha kwanza cha biashara katika jangwa kuu kwa Ulaya, na ngome hii ilitumiwa kama kituo cha dhahabu.

Bustani ya kitaifa

Bustani ya kitaifa: Bustani hii ipo karibu kilomita 20 kaskazini mwa ngome ya pwani ya Cope,imezungukwa na mashamba hasa mashamba ya " Kakao" na ina miti mingi na wanyama wa porini. Ndani yake kuna daraja linalotumiwa na watalii kwa kutembelea bustani hiyo. daraja hilo ambalo lina urefu wa mita 350 na urefu wake kutoka ardhini ni mita 40.

 

Chanzo:

, Ministry Of Foreign Affairs and Regional Integration

 

Ghana", nationsonline

 

"Climate", ghanaweb