Jamhuri ya Guinea ya Ikweta
Jumanne, Januari 01, 2019
Jamhuri ya Guinea ya Ikweta

Kaulimbiu ya taifa
( Umoja, Amani, Haki)
Mji mkuu Malabo
Mji mkubwa nchini Bata
Lugha rasmi Kihispania, Kifaransa, Kireno
Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Waziri mkuu vicente Ehate tomi


Uhuru Kutoka Uhispania 12 Oktoba 1968
Kiangazi (DST) CET (UTC+1)- Jumla - Maji (%) 28,051 km² (141)
Idadi ya watu- Julai 2014 kadirio(22,254 (150)722,254 (150)
- Msongamano wa watu 24.1/km² (187
Fedha CFA franc (XAF)
Saa za eneo Kiangazi (DST) CET (UTC+1)
Intaneti TLD .gq
Kodi ya simu +240 Río Muni

 

Jamhuri ya Guinea ya Ikweta (kwa Kiswahili pia: Ginekweta) ni nchi mojawapo ndogo ya bara la Afrika iliyopo upande wa magharibi wa Afrika ya Kati.

Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon upande wa kusini na mashariki, na Ghuba ya Guinea upande wa magharibi, ambapo visiwa vya São Tomé na Príncipe vinapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya Ikweta.

 

Jina
Jina la nchi linatokana na kuwa karibu na Ikweta na pia karibu na Ghuba ya Guinea.

 

Historia
Makala kuu: Historia ya Guinea ya Ikweta
Ilikuwa koloni la Hispania kwa jina la Guinea ya Kihispania likiwa na maeneo mawili ambayo yalijulikana kama Río Muni (bara na visiwa vidogo kadhaa), na kisiwa cha Bioko ambako uko mji mkuu, Malabo (ambayo iliitwa awali Santa Isabela).

Mikoa
Mikoa ya Guinea ya Ikweta
Guinea ya Ikweta imegawiwa katika mikoa 7:

Mkoa wa Annobón (mji mkuu wa mkoa: San Antonio de Palé)
mkoa wa Bioko Norte (Malabo)
Mkoa wa Bioko Sur (Luba)
Mkoa wa Centro Sur (Evinayong)
Mkoa wa Kié-Ntem (Ebebiyín)
mkoa wa Litoral (Bata)
Mkoa wa Wele-Nzas (Mongomo)
Watu
Makala kuu: Watu wa Guinea ya Ikweta
Lugha
Ni nchi pekee ya Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya taifa, hasa ukiacha Ceuta na Melilla (maeneo ya Hispania yaliyozungukwa na Moroko) na Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu (nchi-isiyotambulika-kimataifa). Pamoja nacho, Kifaransa na Kireno pia ni lugha rasmi.

Dini
Wananchi wengi wanafuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (87%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (5%). Wanaofuata dini asilia za Kiafrika ni 5%.