Libya
Jumapili, Januari 06, 2019
Libya

Mji mkuu wake: Tripoli, na ni jiji kubwa zaidi , na mji maarufu zaidi ni Misratah, Banghazi, na Sirte.

 

Mahala: Iko Kaskazini mwa Afrika, imepakana na Bahari ya Mediteranea kwa upande wa Kaskazini, Misri kwa upande wa Mashariki, Sudan kutoka Kusini Mashariki, Chad na Niger kutoka Kusini, Algeria na Tunisia kutoka Magharibi.

Pwani ya Libya huzingatiwa ndio pwani ndefu zaidi ya nchi yoyote ya Kiafrika inayopakana na Bahari ya Mediteranea.

 

Eneo: milioni 1.77 kilomita za mraba.

Libya ni nchi ya nne kwa ukubwa wa eneo barani Afrika, na ni ya 17 kama nchi yenye eneo kubwa zaidi duniani.

Mgawanyiko wa kiidara: Idadi ya majimbo ya Libya ni ishirini na mbili.

Hali ya Hewa : Libya ipo kati ya latitudo 19 o na 34 o   kaskazini na katikati ya longitudo 9 o na 26 o mashariki.

 

Dini: Dini kuu ni Uislamu - Madhehebu ya Sunni.

Makabila: Kiarabu, Tabu, Berber (Amazigh), na Karagalh ambao ni mchanganyiko wa Kiarabu- Kituruki-Berber.
Libya inahifadhi haki za kilugha na kiutamaduni za vikundi visivyo vya Kiarabu, na miongoni mwa vikundi hivi ni Amazigh, Tabu, na Tuareg.

 

Bendera ya Libya: Kulingana na katiba ya uhuru ya mwaka wa 1951, bendera ya Libya inaundwa na rangi tatu: nyekundu, nyeusi na kijani na kijani na nyota nyeupe katikati yake, na huitwa "bendera ya uhuru." Na mnamo Agosti 21, 2011, bendera hii iliinuliwa juu ya taasisi rasmi za serikali katika mji mkuu wa Tripoli baada ya ukombozi wake.

Lugha kuu: Kiarabu - Kiingereza - lugha ya kiitalia imenea sana miongoni mwa wazee.

 

Idadi ya watu: Kulingana na tovuti ya Worldometer, Libya ilishika nafasi ya kumi na tatu, na idadi ya watu ni milioni 6.5 takriban.

Mgawanyo wa wakazi: idadi kubwa ya watu wanakaa katika maeneo ya pwani, na asilimia 78% ya wakazi wanaishi mijini.

Likizo rasmi:

 • Disemba 24: Siku ya Uhuru, Tarehe hii inaadhimisha yaliyotokea siku hii 1951 wakati Libya ilitangaza uhuru kutoka kwa udhibiti wa Uingereza-Ufaransa.
 • Februari 17: Siku ya Mapinduzi, ambayo husherehekea mwanzo wa mapinduzi ambayo hatimaye yalimuondoa Muammar Gaddafi.
 • Machi 19 : siku ya likizo rasmi huko Libya inayoitwa "Makumbusho ya Ushindi juu ya Gaddafi", NATO iliamua kuingilia kati ikiwaunga waasi, na wakati Jeshi la Anga la Ufaransa lilipowasili Libya Machi 19, 2011, ilikuwa hatua iliyo pelekea mabadiliko ya vita. Hatua hii ya mabadiliko imekuwa tarehe ya kusherehekea ushindi kwa Siku ya Gaddafi.
 • Oktoba 23: Siku ya Ukombozi, ambayo inatofautiana na "Siku ya Uhuru," ambayo inakumbusha anguko la udikteta wa Muammar Gaddafi.
 •  Septemba 16 : Siku ya shahidi wa Libya, "Eid Al-Shaheed ambayo ni likizo rasmi ya kila mwaka ya kukumbuka na kuheshimu wale waliokufa wakati wa mapigano kwa ajili ya uhuru wa Libya na wakati wa mapinduzi ya 2011 ambayo yalimaliza utawala wa Muammar Gaddafi.

 

Jeshi: Hugawanyika katika sehemu kuu 4: Vikosi vya Ardhi – Vikosi vya Majini – Vikosi vya Anga - Vikosi vya Ulinzi wa Anga vya Libya.

 

Sera ya Mambo ya nje:

Hali ya ndani nchini Libya imeibua kivuli juu ya sera ya nje ya Libya, kama moja ya hatua maarufu katika sera ya nje ya Libya ambayo ni ushirikiano wa usalama wa pamoja na nchi za jirani ili kudhibiti mipaka, kuwasaka magaidi, na kuondoa shughuli haramu kama biashara ya silaha, mafia ya usafirishaji viungo vya binadamu na uhamiaji haramu, hasa Libya ndio huzingatiwa lango la kwanza la uhamiaji haramu kwenda Ulaya.

Mashirika ya kimataifa:

Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Uchumi Barani Afrika ABEDA, Benki ya kiafrika kwa Maendeleo AfDB, Mfuko wa Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi na ya Kijamii AFESD, Mfuko wa Fedha wa Kiarabu AMF, Umoja wa Magharibi wa Kiarabu AMU, Umoja wa Afrika AU, Benki ya Maendeleo kwa nchi za Afrika ya Kati BDEAC, COMESA, Shirika la Chakula na Kilimo FAO, Kundi la 77, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Chumba cha Kimataifa cha Biashara ICC (NGOs), Shirikisho la kimataifa la Maendeleo IDA K, Benki ya Maendeleo ya Kiislam IDB, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD, Shirika la Kazi la Kimataifa ILO, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF, Shirika la kimataifa la Bahari IMO, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Shirika la Umoja wa Mataifa UN, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuelimisha, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Shirika la Utalii la Kimataifa UNWTO, Shirika la Afya la Kimataifa WHO.

 

Uchumi wa Libya:

Uchumi wa Libya unategemea usafirishaji wa mafuta na gesi, kwa hivyo huathiriwa sana na kiasi cha uzalishaji mkubwa.

Usafirishaji wa mafuta na gesi ndio chanzo kikuu cha mapato nchini Libya, 94% ya mapato ya fedha za kigeni za nchi hiyo. Libya inajivunia akiba ya mafuta inayofikia mapipa bilioni 41, ambayo ni kubwa zaidi barani Afrika. Mafuta na gesi yapo kwa kiasi kubwa katika maeneo ya Sirte, Ghadamis na Murzuq na katika maeneo ya Baharini kaskazini Magharibi mwa Libya, na tafiti za uchunguzi bado zinaendelea.

 

Sekta ya Utalii :

Libya ina sifa ya urithi wa kihistoria ambao unachanganya kati ya mitindo ya kiuturuki, kiitalia, kirumi na kigiriki, hasa katika miji ya Sabratah, Leptis, Tolmieta, Sousse, na mingine. Libya huzingatiwa ni nchi ya pili inayomiliki zaidi milki ya Kirumi, baada ya Italia.

Libya ina pwani ndefu zaidi barani Afrika inayozunguka Bahari ya Mediteranea, na urefu wake ni kama kilomita elfu moja na mia tisa na thelathini na tano, kwa hivyo mikoa katika pwani hiyo ina hali ya hewa ya wastani, ambayo ni hali ya hewa ya Mediteranea.

Libya inajumuisha jangwa kubwa zaidi ulimwenguni, pamoja na ziwa lenye chumvi nyingi la Qabr Aoun katika upande wa kusini Magharibi, na hakuna tukio hata moja la kuzama limerekodiwa ndani yake. Na pia inamiliki maeneo mazuri, pamoja na mlima wa kijani mashariki mwa nchi

Libya inamiliki vivutio kadha kama Makumbusho ya Al-Saraya Al-Hamra au Ngome la Tripoli, ambayo ni mkusanyiko wa majumba makubwa zaidi na ya zamani ya Libya, yamegawanywa katika makumbusho 4, kuonesha urithi na historia ya Libya kupitia nyakati tofauti.
Kuna pia miji 5 ambayo imesajiliwa na UNESCO miongoni mwa urithi wa ulimwengu, na ambayo ni : Leptis, Sabratah, Tripoli, Shehat na Ghadames

Viwanda vya kienyeji :

Viwanda vya kienyeji ni dhihirisho la ustaarabu, bali ni njia yake ya msingi ili kuelezea utamaduni na uhalisi wa jamii.

 

 • Viwanda vya kienyeji nchini Libya vinatofautiana na vinajumuisha :
  Viwanda vya Ngozi.
  Viwanda vinavyotegemea bidhaa za mitende.
  Viwanda vya pamba .
  Viwanda vya chuma.

 

Vyombo vya habari vya Libya:


Hivi karibuni, vyombo vya habari vya ndani vilikuwa chini ya serikali ya Libya, mnamo Januari 29, 2006, mtoto wa Muammar Gaddafi Saif Al-Islam Gaddafi alitangaza kwamba serikali ya Libya itaruhusu Runinga na Redio binafsi, na baada ya mapinduzi ya Februari 17, magazeti,Runinga na Redio binafsi ziliibuka lakini zaidi ya vituo hivi vinarusha matangazo yake kutoka nje ya Libya.

Shirika rasmi la habari la Libya ni WAL.