Moroko
Jumatatu, Oktoba 21, 2019
Moroko

Ufalme wa Morocco ni nchi iliopo kaskazini Magharibi mwa Afrika na inapakana na bahari ya Mediterania kaskazini na  Bahari ya Atlantic Magharibi na ina pakana na Algeria upande wa Mashariki na Mauritania upande wa kusini.

 Na Morocco ilipata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka 1956 na iliingia Umoja wa Mataifa tarehe 22 mwezi Aprili  mwaka huo huo na ilijiunga na Umoja wa nchi za Kiarabu mwaka 1958  na Waislamu wameifungua Morocco mwaka 683 kupitia Oqba Bin Nafe.

Eneo : Morocco ina eneo la  710,850km² na Urefu wa pwani yake unafikia 3500 km.

 

Mji Mkuu : Rabat.

 

Miji Muhimu : Mji mkuu wa kisiasa ni Rabat , mji wa kiuchumi ni Casablanca , mji wa kiutamaduni ni Fes , Marakesh , Tangaa na Agadir

 

Bendera : Nyekundu na katikati kuna  Nyota ya kijani.

 

Fedha ya ndani : Morocan Dirham, na bei ya dola ni kati ya dirham 9 hadi 9.55.

 

Lugha ya kiarabu : Ni lugha rasmi na Katiba ya 2011 iliongeza lugha ya   Amazigh kama lugha rasmi na lugha ya Amazigh  ina lahaja tatu.

 

Siku ya Kitaifa : Julai 30  kila mwaka.

 

Hali ya Hewa :  Nchi ina hali ya hewa ya rutuba iliyo athiriwa na Bahari ya

 Mediterania na Bahari ya Atlantic kutoka Magharibi na Kazkazini Magharibi, ama ndani ni sifa ya  hali ya hewa ya bara , wakati Kusini ni sifa ya hali ya hewa ya joto la jangwani.

 

Eneo la ardhi.

Morocco ina eneo la ardhi tofauti, Milima , Pwani na Jangwa  ambapo kila eneo lina mvuto wake maalumu na wa aina yake ya kipekee katika utofauti ya rasilimali yake ya asili

Tambarare na Milima  : Morocco  kwa juu inaonekana kupanuka  kati ya Bahari ya Mediterania na Bahari ya Atlantiki ikiingiliwa na safu ya milima kutoka mashariki hadi magharibi na kutoweka kwenye mchanga wa Jangwa kusini mwa mipaka ya Mauritania

Na Morocco ina mandhari ya asili yenye sifa nzuri tofauti ambapo theluji zinafunika vilele vya milima mikubwa ya atlas , Milima ya mashambani yenye miinuko mikubwa,

 Misitu minene ya mwaloni iliopo  katika Platea ya kati , Tambarare zenye rutuba katika eneo la Magharibi, ardhi kavu katika matawi ya juu na mafuta yaliyotawanyika katika Bonde la Sos na Daraa na matuta ya mchanga Jangwani.

Maeneo ya hifadhi: Uhandisi wa majengo na makazi yanaonesha utajiri wa tamaduni mbalimbali zilizoundwa za utambulisho wa Morocco.

Na huko Morocco, Kuna mito mikubwa minane , muhimu zaidi ambayo ni : Alkous wenye urefu wa km1000 , Spo wenye urefu wa km 500 , Bouregreg wenye urefu wa km 250 , Daraa wenye urefu wa km 1200 na yote hutiririka katika  Bahari ya Atlantiki na Mto wa Moulouya unatiririsha katika Bahari ya Mediterania wenye urefu wa km 45 ,  Mto wa Umm El-Rabi ambao unatiririsha katika Azemmour katika Bahari ya Atlanki wenye urefu wa km 600, Mto wa Tensift katika Bahari ya Atlantiki wenye urefu wa km 260 na Mto wa Ziz katika  Bahari ya Atlantiki wenye urefu wa km270.

Idadi ya watu : Kulingana na sensa ya hivi karibuni , idadi ya watu wa Morocco ni milioni 33,848, 242 ( takwimu ya Septemba 2014 )

 

Mfumo wa kisiasa :

Ufalme wa Morocco kulingana nakatiba ya Morocco ,ni Ufalme wa kikatiba chini ya  Katiba ya 2011 ambayo iligusia mabadiliko ya kifalme ya kikatiba, inapunguza nguvu za Mfalme na inateua Waziri Mkuu kutoka chama kinachoshinda idadi kubwa zaidi za viti katika chaguzi za bunge, na kupitishwa kwa Amazigh kama lugha rasmi ya pili nchini.

Vyama vya kisiasa :

Morocco kuna vyama 32, ambayvo vingine ni vya zamani vilishuhudia  uhuru wa nchi na vingine  ni vipya  vimeibuka kutokana na maendeleo ya kisiasa au vilivyotokana na sababu za kijamii na migogoro, na vyama vingi vya kisiasa nchini Morocco ni vya kidunia na sheria ya vyama vya kisiasa inazuia uanzishaji wa vyama  kwa misingi ya kidini lugha au kabila na Morocco inazingatiwa ni miongoni mwa nchi zilizo na vyama  vya  siasa mapema mwaka 1934 katika muktadha wa harakati zamaandamano dhidi ya ukoloni wa Kifaransa.

 

Bunge la Morocco

Morocco ilijua taratibu za bunge mwaka 1962 baada ya kupitishwa kwa katiba ya 1962 na bunge likagawanywa na kuwa mabaraza mawili kwa mujibu wa katiba ya 1996 : Baraza la wabunge na linajumuisha wanachama 395 wanaochaguliwa moja kwa moja kwa muda ya miaka 5  na baraza la washauri na linajumuisha wanachama 265 na wanachaguliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa wawakilishi wa makundi ya kitaifa na wanaochaguliwa katika vyumba vya kitaalamu kwa miaka 9 na theluthi yake huboreshwa kila miaka 3.

 

Katiba:

Katiba ya 2011 iliyopigiwa kura Julai 1, 2011 na ilipata idhini ya wapigaji kura asilimia 98.49 kwa wapiga kura waliofikia asilimia 72.65

 

Sera za nje:

Morocco inashuhudia mabadiliko mengi katika sera za nje zinazoambatana na vipaumbele vya na masilahi yake ya kimkakati , muhimu zaidi ni kujikita zaidi Kiafrika na Kilatini na Afrika ilipata umuhimu mkubwa kutoka Morocco uliofasiriwa katika ziara zaidi ya 50 za  Mfalme wa Morocco kwa nchi 29 za kiafrika tangu kuchukua jukumu la utawala na alizindua miradi ya maendeleo katika nchi nyingine za bara na umuhimu huu ulikamilika kwa Morocco kurejeshwa tena uanachama wake katika Umoja wa Afrika mwezi wa kwanza 2017 baada ya kukosekana  kwa zaidi ya  miaka 30 kutoka AU.

Uchumi:

Tangu Uhuru, Morocco ilichagua siasa ya vyama vingi na uhuru wa kiuchumi kupitia kufanya haki ya umiliki na uhuru wa kuamua ndani ya haki za kimsingi zilizo hakikishwa na Katiba.

Uchumi wa Morocco upo wazi kwa nje . tangu mwanzoni mwa miaka ya themanini karne iliyopita ilipitisha sera ya uwazi ya kiuchumi na kifedha ili kukomboa biashara ya nje,kukuza ushirikiano wa uchumi wa kimataifa na kuchangia katika kuimarisha mfumo wa biashara wa pande mbalimbali na kwa hivyo uchumi wa Morocco unashuhudia maendeleo makubwa katika nyanja ya kurekebisha miundo ya kiuchumi na kifedha na kuinua kiwango cha mfumo wake wa kisheria na wa taasisi ,  na lengo la mageuzi haya ni kuharakisha kasi endelevu ya ukuaji wa uchumi wa Morocco na kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

 

Taarifa za msingi kuhusu Morocco:

Katika suala hili Morocco  imerahisisha ajenda ya biashara ya nje, imepunguza ushuru wa forodha na kuondoa taratibu zisizo za ushuru na kuboresha hali ya kazi na uwekezaji na imepanua mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na kuchangia kwa njia  iliyopangika katika kuimarisha mfumo wa kibiashara wa pande mbalimbali , pamoja na hayo, yamefanyika mabadiliko kadhaa  ya sheria kwa lengo la kuendelea na marekebisho haya.

 Kwa mfano : Mkataba wa uwekezaji , sheria ya biashara , sheria ya mahakama ya biashara , sheria ya forodha, sheria inayohusiana na uhuru wa bei na ushindani, mfumo unaohusiana na mikataba ya umma nasheria  inayohusiana na ulinzi wa mali ya Viwanda na Biashara.

Morocco ni ya tano Afrika kwa nguvu za kiuchumi baada ya  Misri , Algeria , Nigeria  na Afrika Kusini. Uchumi wa Morocco unafikia pato la jumla   ambalo ni dola za Kimarekeni bilioni 109 na ukuaji unaongezeka  kati ya  asilimia 2.5 na 3.5 katika miaka kumi iliyopita na mfumuko wa bei ni asilimia 1.4  kufuatana na takwimu za mwaka 2014 .

 

Utalii:

Morocco inasifika kwa aina mbalimbali za Utalii kutokana na urithi wa Ustaarabu wa zamani , na maeneo ya kijiografia na  kimkakati, mandhari za asili za kuvutia  pamoja na muundo muhimu wa Utalii na wa hoteli muhimu, huko Morocco kuna maeneo mengi ya urithi wa ulimwengu : Eneo la Akiolojia ya Lolili, ikulu ya Ait Ben Haddou , Mazakan ( mpya ), mji wa kale wa Swaria , mji wa kale wa Fez , mji wa kale wa Marrakech , mji wa kale wa Tetouan, mji wa kihistoria wa Maknes, eneo la kitamaduni la uwanja wa Msikiti wa Alfanaa , mji wa Tantan na mji wa Tangier.

 

Kuna sehemu kadhaa muhimu zinazowavutia Watalii kwenda Morocco na miongoni mwake: Milima ya atlas iliyofunikwa na theluji na hali ya hewa ya joto Jangwani , maeneo ya kihistoria , Mahekalu ya kidini ,  fukwe na masoko ya wenyeji .

Maeneo yanayovutia watalii nchini Morocco yanazingatiwa ni mojawapo ya  sehemu za   vivutio kwa Watalii nchini Morocco na miongoni mwake ni kama yafuatayo:

Uwanja wa msikiti wa Alfanaa : Huu uwanja mkuu unatambuliwa na UNESCO na kuanzishwa kwake unarejea enzi ya  Almorabeten (Almoravids) na umejaa masoko, sauti , maonesho,Wauzaji wa mitishamba , Wasimulizi wa hadithi na wasanii na kwa hivyo ni mojawapo ya Sehemu za kupendeza zaidi katika mji wa Marrakech wa morocco.

Msikiti wa Al-Katiba: Nao ni Msikiti wa zamani kabisa miongoni mwa misikiti mitatu duniani na Una Madirisha yaliyopindika, matao ya mapambo mzuri na vijiwe vyyekundu, na urefu wake ulifikia mita 70.

Ikulu ya  Al-Budaiya:Ikulu hiyo ndio sura ya mwanzo ya  Marrakech na katika kila mwaka katika mwezi wa Juni , Sherehe za sanaa maarufu za watu wa Marrakech hufanyika katika Ikulu hiyo.

Msikiti wa bin Youssef : Historia ya kujengwa kwake inarejea mwishoni mwa karne ya 12 , nalo ni

Jengo la kale na muhimu zaidi mjini kama ambavyo ni kivutio maalumu cha kiislamu.

Mabaki ya Saadani: Nayo ni mabaki ya yaliyo tawanyika ya watu wa ukoo wa Saadi na labda chumba chenye nguzo 12 na ndio sehemu muhimu kabisa ya eneo hili.

Jumba la  Murabetia : Nalo ni jengo pekee lililobaki la himaya ya  Al-Murabetin.

Bustani ya Maguril: Bustani hii kubwa inajumuisha Mabwawa ya kuogelea na chemchem na aina zaidi 15 ya ndege mbalimbali na sanaa ya kiislamu inaonekana hasa katika kuta zake na mapambo yake ya ufinyanzi.

Moroko ina kilomita 3,500 za fukwe, theluthi yake juu ya Bahari ya Mediterania na iliyobaki ni juu ya Bahari ya Atlantiki , hii inaifanya morocco kupendekeza na mahali pa kivutio kwa Watalii nchini Moroccao na wageni, na wakati wote fukwe zimekuwa kivutio kinachopendelea kwa  watalii hasa kupitia majira ya joto.

 

Utamaduni na vyombo vya habari:

Ufalme wa Morocco unakumbatia idadi kadhaa za tamaduni na staarabu za zamani ambapo historia imeshuhudia, kwani ardhi za Morocco zilikaribisha idadi kadhaa za watu kutoka

makabila ya Kaskazini, Kusini, Mashariki, hivyo  Kila kikundi miongoni mwa vikundi hivi viliacha athari  ya kina katika muundo wa kijamii wa nchi hiyo , na pamoja na hayo ni  kuwa kila eneo miongoni mwa  maeneo ya Morocco yana sifa zake ambazo zinatofautiana  na zingine.

Na kwa hivyo Utamaduni wa morocco umejiunda kama jinsi ulivyo na kuwasilisha urithi wa ustaarabu wa kipekee kwa historia.

Na kuhusu yanayohusiana na muziki na sherehe , sikukuu kadhaa zinazopangwa na Ufalme wa Morocco zinafanyika nchini Morocco kama Sikukuu ya kimataifa ya urithi wa mdomo na kongamano la kimataifa la Ukumbi wa michezo ya watoto na na sherehe nyingine nyingi, na katika sherehe  hizi kuna idadi kadhaa za tamaduni za kitaifa ambazo Morocco inazikaribisha katika sherehe hizo.

Ama yanayohusiana na muziki wa Morocco, na moja ya muziki maarufu wa Morocco ni Binder na Witra,  ambayo ni mchanganyiko wa muziki wa mashariki na  Morocco, na kila eneo katika maeneo ya Morocco yana muziki wake.

Morocco ina Makumbusho 14 yaliyoenea pande zote , muhimu zaidi : Makumbusho ya Kaskazini , Dar Al Makhzen, nyumba ya sanaa ya kisasa mjini Tangier , makumbusho ya urithi wa Amazigh huko  Agadir na makumbusho ya  kumbukumbu ya Archaological ya Rabat katika mji mkuu , na Morocco inajumuisha maeneo mbalimbali 71 ya akiolojia ambayo yameshuhudia ustaarabu uliofuata miongoni mwake ni maeneo 7 yaliyosajiliwa katika urithi wa kimataifa , muhimu zake zaidi : Jumba la Al-Murabitia mjini Marrakech, mji wa zamani waTitwan , Mlango wa chuma wa fez , mji wa zamani wa Rabat na pango la Tafughalt.

Morocco inashuhudia maendeleo katika nyanja ya vyombo vya habari na uandishi wa habari kufuatia kutangazwa sheria  ya vyombo vya habari iliyorekebishwa  mwaka 2002 ambayo inatoa  haki ya kupata habari, na idadi za vituo vya redio viliongezeka na hadi vituo 65,vituo vya Televisheni 8 , magazeti ya kila siku na ya kila wiki 29 na tovuti za kielektroniki 280.