
Kaulimbiu ya taifa: Unity, Liberty, Justice
Wimbo wa taifa: Namibia, Land of the Brave (Namibia, nchi ya mashujaa)
Lokeshen ya Namibia
Mji mkuu ( Windhoek)
(22°33′ S 17°15′ E)
Mji mkubwa nchini (Windhoek)
Lugha rasmi (Kiingereza1)
Serikali (Jamhuri)
Rais (Hage Geingob)
Waziri Mkuu (Saara Kuugongelwa)
Uhuru ( Kutoka Afrika Kusin 21 Machi 1991)
{Eneo {825,615 km² (ya 34)
- Jumla (kidogo sana)
- Maji (%)}
(Idadi ya watu (2,030,6922 (ya 147){
- Julai 2005 kadirio (2,113,077)
- 2011 sensa
- Msongamano wa watu) ( 2.54/km² (ya 235)
Fedha (Namibia dollar (NAD)
Saa za eneo (UTC+1)
- Kiangazi (DST) (UTC)
Intaneti TLD (.na)
Kodi ya simu (+264)
-Namibia ni nchi ya Afrika ya Kusini kwenye pwani ya Atlantiki.
Imepakana na Angola, Zambia, Zimbabwe Botswana na Afrika Kusini.
Imepata uhuru wake kutoka Afrika Kusini mwaka 1990.
Mji mkuu ni Windhoek (wakazi 322.500).
Jiografia
Sehemu kubwa ya nchi ni kavu sana na jangwa la Namibia na Kalahari zinafunika asilimia kubwa
ya uso wa nchi.
Jangwa la Namibia liko upande wa magharibi likifuata pwani ya Atlantiki kuanzia Afrika Kusini
hadi Angola. Upande wa mashariki kuna jangwa la Kalahari linalovuka mpaka wa Botswana.
Katikati ya majangwa hayo kuna nyanda za juu zinazofikia kimo cha mita 1700 kwa wastani.
Historia
Makala kuu: Historia ya Namibia
Historia ya kale
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Chini ya ukoloni
Namibia katika mipaka ya sasa ilianzishwa katika karne ya 19 kama koloni la Ujerumani kwa
jina la Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani.
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Uingereza na Afrika Kusini. Tangu
mwaka 1919 ilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa chini ya serikali ya
Afrika Kusini.
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia serikali ya Afrika Kusini ilieneza siasa yake ya apartheid pia
katika Afrika ya Kusini-Magharibi ikijaribu kulitendea eneo hilo kama sehemu kamili ya Afrika
Kusini. Hii haikukubaliwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingi za dunia.
Mwaka 1978 Umoja wa Mataifa uliamua ya kwamba Afrika ya Kusini-Magharibi unapaswa
kupewa uhuru. Baada ya miaka ya vita vya kupigania uhuru kati ya SWAPO na jeshi la Afrika
Kusini, mchakato wa kimataifa wa kuelekea uhuru ulianza mwaka 1988 na hatimaye mwaka
1990 nchi ilipata uhuru wake kwa jina la Namibia.
Watu
Wakazi wengi ni wa makabila ya Wabantu, hasa Waovambo (49.5%). Pia wako wengi wa jamii
ya Khoisan, ambao wametokana na wenyeji wa nchi.
Asilimia 7 wana asili ya Ulaya, hasa Makaburu na Wajerumani, na asilimia 8 ni machotara.
Oshiwambo ni lugha ya kwanza ya karibu nusu ya wakazi, lakini Kiingereza ndicho lugha rasmi
ingawa ni lugha ya kwanza ya 3% pekee za wakazi. (Angalia Orodha ya lugha za Namibia.)
11.3% za wakazi wanatumia lugha za Kikhoisan.
Kijerumani na Kiafrikaans zilikuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza hadi uhuru. Wakazi wengi
hutumia Kiafrikaans kama lugha ya pili, na 10.4% kama lugha ya kwanza. Kijerumani ni lugha
ya kwanza wa 32% za wakazi wenye asili ya Ulaya.
Kireno kinatumiwa na 4-5% za wakazi, hasa wenye asili ya Angola.
Upande wa dini, 80-90% za wakazi ni Wakristo (hasa Walutheri, Wakatoliki ni 13.7%).
Waliobaki kwa kawaida wanafuata dini asilia za Kiafrika.