Senegal
Jumatatu, Machi 02, 2020
Senegal

 

Ni nchi ya Kiafrika iliyoko Magharibi mwa bara , na ni moja wapo ya nchi maarufu kwenye bara. Senegal imeitwa kwa jina hilo kutokana na Mto wa Senegal ambao unapakana na nchi kutoka kaskazini.

Bendera: Bendera ya Senegal ina rangi tatu kuu, ambayo ni kijani, manjano, nyekundu , na  katikati nyota ya kijani yenye umbo la pembe tano. Na kuhusu  maana ya rangi ya bendera ya  nchi ya Senegal na nyota kijani yenye umbo la pembe tano, ni kama ifuatavyo:

Rangi ya Kijani: Rangi ya kijani kwenye bendera huashiria Nabii wa Allah Mtume Muhammad, S.A.W  kwa Waislamu nchini, huashiria pia  matumaini kwa wafuasi wa dini ya Kikristo, na huashiria uzazi kwa wanasaikolojia.

Rangi ya manjano: Kuhusu rangi  ya manjano, iliopo katikati ya bendera kwa usawa, huashiria maliasili ambayo hupatikana nchini Senegal.

Rangi Nyekundu: Kuhusu  rangi nyekundu huashiria damu, pia maisha na ni dalili  ya wazi juu ya kujitolea kwa damu kwa ajili ya  maisha na maendeleo ndani ya nchi.

Nyota yenye umbo la pembe tano: Katikati ya Bendera ya nchi Senegal rangi ya manjano kuna nyota yenye umbo la pembe tano yenye rangi kijani nayo huashiria uwazi kwa ulimwengu na uhuru wa nchi , na  kuhusu pembe tano za nyota hiyo huashiria nguzo tano za dini ya Kiisilamu kwa Waislamu.

Mahali na Eneo: Senegal iko magharibi mwa bara la Afrika, upande wa  Magharibi pwani ya Atlantiki. Senegal  inashirikiana katika  mipaka yake  na nchi tano, na eneo la Senegal ni Kilomita 196,722 km2.

Mji mkuu: Mji  wa "Dakar""

Senegal imegawanywa katika majimbo 14:

Dakar - Ziguinchor - Linguere- St. Louis - Diourbel - Kolda - Bignona - Podor - Kaolack - Kedougou - Matam - Tiebo - Thies – Tambacounda.

Siku ya Kitaifa : 

Aprili 4: Senegal Ilipata uhuru wake kutoka Ufaransa  Aprili 4, 1960.

Hali ya hewa

Kwa sababu ya tofauti ya kijiografia kati ya maeneo ya Senegal , kuna hali kuu tatu za hewa nchini , ambayo kila moja huonekana katika eneo tofauti, ambayo ni :

Hali ya hewa ya pwani au Canary  : Inaonekena maeneo  ya Magharibi ya Senegal , ambayo inaangalia pwani ya Bahari ya Mediterania.

Hali ya hewa ya pwani ya Afrika : Hali ya hewa hii inaonekana katika Maeneo ya kaskazini karibu na Mto wa Senegal .

Hali ya hewa ya Sudan: Ni hali ya hewa inayopatikana maeneo ya Kusini mwa Senegal .

Idadi ya watu :idadi ya watu  kwa mujibu wa sensa ya mwaka  wa 2018 ni  ( 15,020,945).

Dini: Waislamu 95.9% - Wakristo 4.1%.

Lugha: lugha rasmi nchini ni Kifaransa.

Katiba: Januari 7, 2001, kura ya maoni ilifanyika kwa rasimu ya katiba , na Januari 22 katiba hiyo ilitolewa.

Mfumo wa Utawala : Bunge, Rais.

Vyanzo vya mapato ya kitaifa

(Asilimia% 70) ya watu  wa Senegal wanafanya kazi katika kilimo , na Mimea muhimu zaidi ni pistachio , miwa , mchele , mahindi na pamba.

Uvuvi , Senegal ina  pwani kubwa baharini..

Utalii , Senegal  inafahamika kwa pwani na misitu mikubwa.

Waandishi:

 Fasihi ya Senegal ni moja wapo ya fasihi muhimu sana huko Afrika Magharibi, Senegal kwa muda mrefu imejulikana ulimwenguni haswa kupitia mtu wa kipekee Leopold Cedar Senghor , mshairi na mwanasiasa  na mtetezi Mkubwa kwa Francophonie na mwimbaji wa Waafrika. Kazi nyingi za  Fasihi ya Senegal zimeandikwa kwa kifaransa, lakini kuna matini kwa Kiarabu au kwa Lugha ya Bulowov.

Waandishi wengine wa jadi ni pamoja na waandishi wa riwaya Sheikh Hamidu Kane , Bravo Diop , Boubacar Boris Diop na Alion Badara Beye , na vile vile Othman Sembene ambaye ameshatoa baadhi ya riwaya zake kwenye televesheni , Kwa kuongezea kazi za Sheikh Anta Diop , kazi na Machapisho ya mtaalamu na mwanathropolojia Tidiane Ndiaye zilizopata umaarufu ulimwenguni.

Utamaduni wa Senegal:           

Tangu mwanzo wa uhuru wa Senegal, Rais Leopold Cedar Senghor amechagua utamaduni kuwa ni nyenzo ya mwelekeo wa kisiasa . Alikuwa akisema kwamba utamaduni uko mwanzo na mwisho wa kila maendeleo.

Sera ya Mambo ya nje

Senegal iko mahali pa juu katika mashirika mengi ya kimataifa, na ilikuwa mshiriki wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1988-1989 na  2015-2016. Na ilichaguliwa kuwa katika Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu mwaka 1997.

Senegal ni mwanachama katika Benki ya Dunia, na ni mwanachama endelevu katika taasisi za kikanda zinazoongoza kama shirika la Uchumi wa Mataifa ya Afrika Magharibi (ambayo ni miongoni mwa nchi Zilizoanzisha) , Jumuiya ya Afrika (AU) , Jumuiya ya  nchi za Sahel-Sahara (CES) na pia Jumuiya ya Uchumi na Fedha ya Afrika Magharibi (UEMOA) , Mamlaka ya Maendeleo ya Mto Senegal (OMVS) na Shirika la Maendeleo la Mto wa Gambia (OMVG), Senegal ni miongoni mwa nchi za kwanza zinazotetea wazo la kuanzisha  nchi za Afrika zilizoungana.

 

Senegal pia ni mwanachama wa Shirika la Kimataifa la Francophonie (OIF) tangu mwaka wa 1970 , na Dakar imethibitisha yenyewe kama mshirika mkuu , na kwa miaka 12 Rais wa zamani wa Senegal Abdo Diouf  aliliongoza shirika hili.  na chini ya  Uenyekiti wa Macky Sol , Senegal iliandaa Kongamano la kwanza la Uchumi la Francophone huko Dakar Novemba 2014 .