Sierra Leone
Jumatano, Februari 12, 2020
Sierra Leone

 

Sierra Leone ni Jamhuri ndogo Magharibi mwa bara la Afrika, kwenye pwani ya Bahari ya Atlantiki, ambayo ilipata uhuru wake Mwaka  1961, baada ya Ukoloni wa Uingereza kuitawala kwa muda Mrefu. Neno Sierra Leone limeundwa kwa silabi mbili, neno Sierra ambalo  linamaanisha "urefu wa kitu au mlima na "Leone", Ambalo linamaanisha simba. ( Jina linamaanisha Mlima wa Simba)                         

Mahali na eneo: Imepakana na Guinea kaskazini, na Liberia kutoka kusini mashariki.

Hali ya hewa: Hali ya hewa Sierra Leone ni ya kitropiki nyevu yenye hali ya joto.

Mji mkuu: Freetown ni Mji Mkuu wa Sierra Leone, uko Magharibi mwa nchi, na ni wenye Bandari inayoangalia pwani ya Atlantiki ya Peninsula ya Freetown, ambapo uchumi wa Freetown unategemea sana Bandari ambayo vifaa vya msingi na usafirishaji wa bidhaa za serikali husafirishwa kupitia Bandari hiyo, na moja ya usafirishaji wa nje muhimu zaidi ambao hutoka Bandari hii: usafirishaji wa samaki, mchele, sekta sigara, na kusafisha mafuta ya petroli

       

Lugha nchini Sierra Leone: Lugha rasmi nchini Sierra Leone ni lugha ya Kiingereza.

Idadi ya watu Sierra Leone: Idadi ya watu wa nchini Sierra Leone karibu ya watu milioni 7.557, kwa mujibu wa sensa ya 2017.

Bendera ya Sierra Leone: Bendera ya kitaifa ya Sierra Leone iliinuliwa Rasmi Aprili 27, 1961 , na ina rangi 3, kijani, nyeupe na Bluu kwa Mtiririko kutoka juu hadi  chini, kijani huashiria kilimo, milima na Rasilimali asili, nyeupe huashiria haki na umoja, na bluu huashiria kwamba matumaini kuwa bandari ya Freetown itachangia kujenga amani ya ulimwengu.

Mfumo wa Utawala: Jamhuri ya Katiba.

Rais wa sasa wa Sierra Leone: Julius Maada Bio.

Siku ya Kitaifa: Jamhuri ya Sierra Leone inaadhimisha Siku ya Uhuru. Aprili 27 ya kila mwaka.

Sarafu au Fedha: Fedha rasmi ya Sierra Leone ni (Lyon).

Miji muhimu zaidi katika Jamhuri ya Sierra Leone: Freetown, Koidu, Yu, Kinema na Sierra Leone imegawanywa katika majimbo 14.

 

Uchumi wa Sierra Leone:

 Watu wengi wa Sierra Leone wanafanyakazi katika kilimo, Ukataji miti, na uvuvi. Kati ya mazao muhimu ya kilimo yanayojulikana nchini Sierra Leone ni mahindi, mchele, tangawizi, Kahawa, na kakao. Watu kadhaa hufanya kazi katika Utengenezaji wa almasi, lulu, dhahabu, chuma, bauxite, Kwa Upande wa mifugo iliyopo, inalenga zaidi katika ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, na kondoo.

Mchele uko mstari wa mbele kati ya mazao ya chakula,pia kuna machungwa, karanga, nyanya, na mihogo.

Kuhusu Mauzo ya nje ya mazao ya kilimo ni kama Kahawa, Tangawizi, kakao na karanga za Cola.  Sierra Leone ndio muuzaji Mkubwa zaidi wa Mitende ya Brazil (bisava), na fukwe za Sierra Leone hutoa samaki wengi wa aina ya chapa.

 

Historia ya Sierra Leone:

Sierra Leone haikutambuliwa na wanahistoria hadi Mwaka 1460, wakati mabaharia wa kireno walipoingia nchini. Na  Mwanzoni mwa karne ya kumi na sita, meli za biashara za Ulaya  Zilifanya eneo hili  kama kituo cha kusafirisha mamia ya raia kwenda Marekani. Tangu mwaka 1725, makabila ya Fulani, ambayo yanaishi katika mashariki mwa eneo hilo  Iinalojulikana 

sasa hivi kwa jina la Sierra Leone, walianza Juhudi kubwa ili kuwajulisha  wananchi  wa maeneo ya karibu Uislamu na kuwaunganisha chini ya bendera yake.

 

Maeneo muhimu zaidi ya Utalii katika Sierra Leone

Kisiwa cha Ponce: Kisiwa cha Ponce kiko katika umbali wa kilomita thelathini kutoka Freetown mji mkuu wa Sierra Leone. Pia kinazingatiwa moja wapo ya maeneo maarufu zaidi ya Utalii Barani Afrika, Ni mahali maarufu  kwa watalii wa Ulaya na haswa Marekani.