Sudan
Alhamisi, Desemba 27, 2018
Sudan

Jamhuri ya Sudan ama Sudan ni nchi ya tatu kwa ukubwa katika bara la Afrika na ya kumi na sita duniani. Imepakana na Misri kaskazini, Bahari ya Shamu kaskazini-mashariki, Eritrea na Ethiopia mashariki, Sudan Kusini kusini-mashariki, Afrika ya Kati na Chadi magharibi, na Libya kaskazini-magharibi.
Kijiografia nchi hii huhesabiwa kama sehemu ya Afrika ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Khartoum.

Jiografia

Sudan iko upande wa Afrika ya kaskazini, ina pwani kwenye bahari ya Shamu kati ya Misri na Eritrea. Imetamalikiwa zaidi na mto Nile na mikono yake.

Ina eneo la kilomita mraba 1,886,068 (728,215 sq mi).

Ardhi yenyewe ni kiwara, lakini kuna milima upande wa mashariki na magharibi.

Hali ya anga ni ya mwangaza kusini, na mikuranga kaskazini.

Mvua yapatikana mwezi wa Aprili na Oktoba.

Uharibifu wa mazingira hasa ni kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo na utapakazi wa jangwa.

Watu na makabila

Kadiri ya sensa za mwaka 1993, wakazi walihesabiwa kuwa milioni 26. Hakuna sensa nyingine ya hakika iliyofanyika baada ya mwaka huo kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kadirio ni kwamba wakazi ni milioni 40 mwaka 2015.

Umma wa miji kama Khartoum (na pia Khartoum, Omdurman, na Khartoum ya kaskazini) waongezeka zaidi: umma wa miji hii yakadiriwa milioni 6-7 na wengine wahamiaji milioni 2 ambao wamekimbia vita vya kusini, magharibi, mashariki na pia wengine kwa sababu ya ukame.

Sudan ina aina mbili za utamaduni — Waafrika walio na Uarabu na Waafrika wasio Waarabu — na maelfu ya makabila na migao ya kabila, lugha tofautitofauti kwa makundi au kabila – migawanyiko hii uleta siasa za utengo na ubaguzi.

Majimbo ya Kaskazini hasa ndio makubwa nchini Sudan, na pia miji mikubwa iko katika majimbo haya. Zaidi ya milioni 22 wanaoishi katika majimbo haya ni Waislamu-Waarabu na wanaongea Kiarabu, lakini wengi pia huongea lugha 70 za kikabila hasa Kinubi, Kibeja, Kifur, Kinuban, Kiingessana, kwa kikundi hiki kuna wale wavutia zaidi kama: Wa-Kababish kutoka kaskazini Kordofan, watu hawa wanaofuga ngamia; Ga’alin, Rubatab, Manasir na Shaiqiyah; makabila ambao kikao chao ni karibu na mito ni kama Baggara wa Kurdufan na Darfur; Wakiham Beja eneo ya bahari ya Shamu na Wanubi wa kaskazini Nile, ambao wengine wamehamishwa karibu na mto Atbara. Eneo la Shokrya kwa Wa-butana, Wa-bataheen wamepakana na Waga’alin na Washorya, upande wa kusini-magharibi eneo ya Butana. Pia kuna Warufaa, Wahalaween na makabila mengine mingi eneo la Gazeera na kwa ufuo wa Bluu Nile na eneo ya Dindir. Hata Wanubi kusini mwa eneo la Kurdufan na Wafur upande wa magharibi.