Tanzania
Alhamisi, Desemba 27, 2018
Tanzania

Maelezo ya historia: Tanzania ilipata uhuru wake  Tarehe 9 Desemba 1961, na Julius Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo  … Na rais wa sasa wa Tanzania ni  John Pombe  Magufuli tangu 2015.

Jina la Tanzania linatokana na kuunganishwa kwa majina mawili: Tanganyika na Zanzibar, ambazo ziliungana mwaka 1964 ili kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambayo jina lake hilo lilibadilishwa mwaka huo na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 • Jina rasmi: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 • Mfumo wa madaraka : Urais

 • Tarehe ya uhuru kutoka kwa Uingereza :Tarehe 9 Desemba1964.  
      
 • Mji Mkuu: Dodoma.

 • Miji muhimu zaidi: Arusha – Zanzibar – Mwanza – Dar es salaam – Tanga

 • Mahali: Mashariki imepakana na Bahari ya Hindi, Kaskazini Kenya na Uganda, Magharibi  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Burundi na Kusini Msumbiji, Malawi na Zambia.

 • Hali ya hewa: Hali ya hewa ya Tanzania ni aina ya kitropiki.

 • Eneo: 945,087 km2.

 • Idadi ya watu: Idadi ya sasa ya watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni watu 59,746,844, na hayo ni kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika Tarehe 20 Novemba , 2018.

 • Ukabila: Tanganyika ina makabila asilimia 99%,  ya Kiafrika, makabila ya Kibantu asilima 95%, idadi ya Wazungu, Waarabu na Waasia inafikia asilimia 1%  ama Zanzibar inakaliwa na Waarabu na wenyeji  Waafrika.

 • Lugha:  Kiswahili ni lugha ya taifa,  Kingereza ni lugha rasmi na ni lugha ya elimu na biashara, Kiarabu hasa ni Zanzibar pamoja na lugha za kienyeji.

 • Sarafu: Shilingi ya Kitanzania.

 • Bendera: Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitishwa rasmi Juni 30, 1964. Inayo rangi nne: nyeusi, kijani, bluu na manjano, ambapo rangi nyeusi inawakilisha watu, kijani huashiria nchi, bluu inaashiria bahari, na manjano inawakilisha madini