Togo
Alhamisi, Oktoba 24, 2019
Togo

Muhtasari wa historia


Katika kipindi cha karne ya kumi na moja na kumi na sita makabila mengi yaliingia nchini kutoka pande mbalimbali, na kati ya karne ya kumi na sita na kumi na nane, ilikuwa kama eneo la pwani lenye kituo muhimu cha biashara kwa watu wa Ulaya.
Na katika mwaka 1884 Ujerumani ilitangaza kwamba Togo ipo chini ya utawala wake na Ujerumani baada ya vita vikuu vya kwanza vya dunia, Utawala wa Ujerumani kwa Togo ukahamia kwa Ufaransa. Katika mwaka 1960 ukatangazwa uhuru wa Togo, na katika mwaka 1967 Gnassingbé Eyadéma akawa Rais wa nchi, na alifariki mwaka 2005, na mwanaye Faure Gnassingbé alichaguliwa kuwa Rais wa nchi (aliopo madarakani kwa sasa).

Jina rasmi :Jamhuri yaTogo.

Mfumo wa Serikali : Jamhuri ya urais.

Tarehe ya Uhuru  : kutoka Ufaransa  Aprili 27 ,1960 nayo ni Sikukuu ya Taifa ya nchi.

Mji mkuu:Lome.

Miji muhimu zaidi: Atakpame ,Bassar,Kpalime,Tsevie.

Mgawanyiko wa Idara
• Togo imegawanyika maeneo matano , ambayo yamegawanywa katika majimbo 30.
Kutoka maeneo ya kaskazini hadi kusini ni Savana, Kara ya Kati, na uwanda wa baharini..
Idadi ya watu: milioni 7,889,759 (sensa ya 2018))
Lugha: Kifaransa ni lugha rasmi ya Taifa pamoja na kiingereza na lugha za kienyeji.

Rais wa nchi wa sasa: Faure Essozimna Gnassingbé Eyadéma .

 

Vyama muhimu zaidi

 

Tume ya uboreshaji.
Mkutano wa Kidemokrasia watu wa Afrika.
Muungano wa Kitaifa kwa ajili ya Mabadiliko.
Muungano wa Qoz kazah.
Chama cha Kidemokrasia kwa ajili ya Uboreshaji.
Muungano kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya kidemokrasia.
Mkataba wa ujamaa kwa ajili ya kuboresha.
Umoja wa Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.

Uchumi                              

unategemea  kilimo,  Kakao na kahawa na  zinafanya  asilimia 35 ya Uchumi wa Togo wa mauzo ya nje    pia Pamba inazingatiwa ni zao muhimu zaidi la fedha. Sekta ya kilimo inachukua  asilimia 72 ya nguvu kazi.

Kuna mwelekeo ili kutumia rasilimali asili ya ardhi kwa madini  kama phosphate ,  Bauxite,na chuma ,pia utajiri wa miti ambayo inaweza kutumika katika utengenezaji wa mbao katika baadhi  ya maeneo,  pamoja utengenezaji wa nguo, pia mwelekeo wa nchi kwenye ghuba ya ghinea hutumiwa katika shughuli za kuingiza na kusafirisha nje.

Jumla ya pato la ndani: Dola  bilioni 4.813 (makadirio ya 2017)

Sarafu: CFA franc ya Afrika ya magharibi.

Mazao muhimu zaidi ya kilimo : Pamba,kahawa ,kakao, Mchele ,Mahindi, Tumbaku, Maharagwe.

      Utengenezaji muhimu zaidi: Madini ya Phosphate - Saruji - Nguo - Viatu –    Sabuni. 

Vyombo vya Habari

Redio inazingatiwa ni chombo cha kawaida kilichoenea zaidi, hasa maeneo ya mashambani, pia serikali ina mtandao wa redio, pamoja na vituo kadhaa vya redio binafsi .
Kuna vituo vitano vya Televisheni vinavyomilikiwa na serikali katika maeneo kadhaa ya kurusha matangazo, na kituo kikuu cha Televisheni ni Togolaise.
Serikali inalimiliki gazeti la " Togo Press " la kila siku, pamoja na magazeti mengine ya sera ya kigeni.
Togo inafuata sera endelevu ya kigeni na inashiriki katika mashirika kadhaa ya Kimataifa,Togo pia ina sera endelevu maalumu katika masuala ya kikanda Afrika Magharibi na Umoja wa Afrika na mahusiano kati ya Togo na nchi jirani kwa ujumla ni mzuri.