Uganda
Alhamisi, Januari 10, 2019
Uganda

Eneo la Kijiografia

Uganda ipo katika eneo la Afrika Mashariki, inaojulikana kama "Lulu ya Afrika", iliopakana na Kenya upande wa Mashariki, na Kaskazini imepakana na Sudan kusini, na Magharibi imepakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Kusini Magharibi imepakana na Rwanda, na kusini imepakana na Tanzania. Na kwa hivyo Uganda ni nchi isiyo na pwani.

Eneo : 236.40 km2.

Mji mkuu: Kampala.

Lugha rasmi: Kiingereza na Kiswahili,  aidha kuna makumi ya lugha zingine za kienyeji ambazo hutumiwa.

Wakazi :

Idadi ya wakazi takribani  milioni 35.

Mgawanyiko wa kiidara :

Uganda ina mikoa  25.

Miji muhimu zaidi: Entebbe - Jinja - Mbale - Fort Portal - Gulu.

Mfumo wa serikali : Jamhuri ya urais

Uganda imechukua jina lake kutoka Ufalme wa Buganda, ambao ulijumuisha sehemu kubwa ya kusini mwa nchi ikiwa ni pamoja na mji mkuu, na Uganda ilipata uhuru wake kutoka kwa utawala wa Uingereza tarehe 9 Oktoba 1962.

Hali za Kisiasa :

Uganda imeshuhudia utulivu wa kisiasa tangu chama cha Kitaifa cha Upinzani kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni chukua madarakani mwaka 1986.

Uganda ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki zinazopokea misaada ya kijeshi ya marekani, pamoja na nafasi ya Uganda katika Somalia na Sudani Kusini kama sababu ya kusaidia kuleta utulivu katika eneo hilo, na pia nafasi muhimu ya kikanda iliyonayo Uganda katika kupambana na ugaidi na ushiriki unaoendelea wa vikosi vya kulinda amani katika nchi kadhaa (Somalia, Demokrasia ya Kongo, Afrika ya Kati, Sudani Kusini).

Uchumi :

Uganda ni moja wapo ya nchi inayokua kiuchumi kwa kasi barani Afrika yenye viwango vya ukuaji wa karibu asilimia 4.7 mwaka 2017 kama ambavyo marekebisho ya kimuundo yaliyofanywa na Rais Museveni tangu kuchukua madaraka yanasifiwa na Benki ya Dunia.

Benki ya Dunia inatarajia kwamba viwango vya ukuaji wa Uganda vinaongezeka hadi asilimia 6 mwaka 2019, kulingana na ubora wa kiasi cha mvua, kuongezeka kwa uwekezaji wa kigeni katika sekta ya mafuta, na kuongeza matumizi ya serikali katika sekta ya miundombinu.

Akiba ya fedha za kigeni ni dola bilioni 3.5, na utalii huzingatiwa ni chanzo cha kwanza cha fedha za kigeni (dola bilioni 1,2), utumaji wa fedha za wanaofanya kazi  nje ya nchi huchukua nafasi ya pili (dola bilioni 1), halafu kahawa inakuja kama mauzo ya nje muhimu zaidi (dola milioni 400).

Mauzo ya nje muhimu zaidi ya Uganda :

kahawa, chai, tumbaku, saruji na samaki zinachukua nafasi ya mwanzo ya mauzo ya nje ya Uganda ambapo nyingi ya bidhaa hizo husafirishwa kwenda nchi za jirani kama Kenya,  Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Rwanda na Sudani Kusini , wakati India, China, Kenya, UAE na Japan zipo mstariwa wa mbele wa nchi zinazosambaza bidhaa zake nchini Uganda.

Uwekezaji :

Uganda inafuata sera ya uchumi wa soko la wazi na biashara huru, pamoja na motisha ya kodi wanayopewa wawekezaji wa nje, hasa katika miradi ya kati na ya muda mrefu, hali ya uwekezaji nchini Uganda ni ya wazi kabisa kati ya nchi za Afrika Mashariki.

China na India ndio wawekezaji wakuu nchini Uganda, ikifuatiwa na Uingereza, Kenya na Sudani, wakati Kenya na Afrika Kusini zinatawala uwekezaji katika sekta ya huduma kama vile benki, kampuni za bima na mawasiliano.

Biashara ya Uganda kwa ujumla inategemea bandari ya Mombasa nchini Kenya, kwa hivyo Uganda kwa sasa inataka kutumia njia ya reli badala ya malori.

Hifadhi za mafuta za Uganda ni karibu mapipa bilioni 3.5, na Uganda inatarajiwa kuwa moja ya nchi zinazozalisha mafuta wakati wa uzalishaji wa bishara wa mafuta unaotarajiwa kufikiwa mnamo 2020, kwani 40% tu ya maeneo yenye mafuta mengi yamegunduliwa, kulingana na ripoti ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Inatarajiwa kwamba mapipa 10,000 ya mafuta yatazalishwa kwa siku, ambayo yatazidisha kwa kikubwa uchumi wa Uganda, Serikali pia inafanya kazi ili kukamilisha mradi wa kusafisha mafuta na njia ya bomba ili kusafirisha  kutoka eneo la Hoima Magharibi mwa Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Uganda ilifanikiwa kudhibiti mfumko wa bei baada ya kuongezeka kwa kasi ya viwango mwaka 2014 na 2015 kutoka asilimia 2 hadi asilimia 9 Oktoba 2015, ambapo iliweza kwa kushirikiana na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kuleta utulivu wa kiwango cha mfumko kwa  asilimia 7 na inatarajiwa kupungua katika kipindi kijacho.

Uanachama katika mashirika ya kikanda :

Uganda ni mwanachama wa UNGOGO - COMESA – EAC -  Umoja wa Afrika -  Kikundi cha 77 - Shirika la Ushirikiano wa Kiisilamu.