Zembabwe
Jumatano, Oktoba 23, 2019
Zembabwe

Mahali na eneo:

Jamhuri ya Zimbabwe ipo kusini mwa Afrika ya Kati, na eneo lake linafikia kilomita za mraba 390,000, na kaskazini inapakana na Mto wa Zambezi, Mashariki inapakana na Msumbiji, Mto wa Limpopo unawakilisha mipaka ya kusini mwa Zimbabwe na Afrika Kusini.

Hali ya hewa:

Hali ya hewa ni ya Kitropiki na mwanzo wa msimu wa mvua ni mwishoni mwa mwezi wa Oktoba hadi mwezi wa Machi. Na katika maeneo ya juu hali ya hewa ni ya wasatani.

Sikukuu ya kitaifa: Aprili 18.


Sarafu:
Dola ya Zimabwe , Pauni (£), Dola ya Marekani($), Pula ya Botswana(P) na Randi ya Afrika kusini(R).

Bendera :

Bendera ya Zimbabwe inaundwa na mistari saba iliyolala kwa utaratibu ufuatao: kijani, manjano, nyekundu na nyeusi, pamoja na pembetatu yenye rangi nyeupi kwenye upande wa kushoto, na pembetatu hii ina nyota yenye rangi nyekundu na ndege aliyekaa juu ya kiota chake mwenye rangi ya manjano. 

Mji Mkuu:

Mji wa Harare, nao ni mji wenye idadi kubwa zaidi ya watu katika Jamhuri ya Zimbabwe.


Idadi ya watu :

Zimbabwe ina idadi ya watu 13.771.721  (Kulingana na takwimu ya mwaka wa 2014)

Lugha:
Lugha ya Kingereza ni lugha rasmi nchini Zimbabwe, pamoja na lugha za Kishona, Kikosi, Kisotho, Tswana, Kishishiwa, Kivenda, Kitsonga.


Mfumo wa serikali ni Jamhuri ya Urais.

Vyanzo:
Wizara ya Mambo ya Nje ya Zimbabwe.