Gamal Abdel Nasser
Jumamosi, Desemba 29, 2018
 Gamal Abdel Nasser

JINA LISILOSAHAULIKA KATIKA AFRIKA

Haikuwa ni jambo la mshangao picha yake kuwepo katika uwanja wa Tahriri
na viwanja vyote vilivyoshiriki katika mapinduzi ya Januari, mwaka 2011 kwa
vijana ambao hawakuwepo katika kipindi cha uongozi wake bali walizaliwa
baada ya kufa kwake kwa miaka mingi.
kwa hakika yeye ni kiongozi Mmisri na Mwaafrika Gamal
Abbel-Naser au  NASER ambaye alitoa kauli mbiu ya
Ewe ndugu yangu nyanyua kichwa chako juu ,wakati wa
udhalimu na utumwa umekwisha, alipokuwa akiongoza
mapinduzi ya 23 Julai mwaka 1952 ambayo ilikuwa ni
ishara si tu katika historia ya Misri ya leo bali katika
historia ya bara letu la kiafrika kwa ujumla ambapo
ilikuwa ni mlango kwa mapinduzi na harakati za uhuru
zilizoenea maeneo mengi katika Bara la afrika.
Na kwa ajili ya msimamo wake wa kuunga kuonga mkono
mapinduzi haya na harakati za uhuru katika nchi nyingi
za kiafrika. Naser alipewa jina la baba wa afrika na
alipata upendo mkubwa wa mamilioni ya watu na mpaka
leo.
Kwa hakika hakuna Mji Mkuu wowote na barabara katika
bara la Afrika isipo kuwa zilibeba jina lake Na sanamu

yake imeenea katika viwanja vingi vikubwa vya kiafrika,
hakika miongoni mwa masana hayo makubwa ni sanamu
kubwa zaidi iliyokoJohansberg ambayo ilifunguliwa rasmi
na kiongozi Mkuu wa Afrika Mhe Nelson Mandela kwa
ajili ya kuwakumbusha Waafrika umuhimu wake mkubwa
katika mnasaba huo.

Abde Naser alisisitiza sana kupitia utawala wake juu ya
kuwepo kwa Misri katika Afrika ni hii inaonekana wazi.

Kiongozi Gamal Abdul Naser alizaliwa mjini Alexandria nchini Misri kabla
ya mwanzoni mwa mapinduzi mwaka 1919.
Rais Naser ni mmoja wa viongozi maalumu waliotaka uwepo
umoja wa nchi za Kiarabu,ambapo pia Rais Naser
Aliungamkono suala la Palastina ,na Alishiriki kwa binafsi yake
katika vita vya mwaka1948 na alijeruhiwa.
Aidha Naser Alikuwa na shughuli muhimu katika kuunga mkono
mapinduzi ya Algria na Akakubaliwa suala la uhuru ya watu wa
Algeria katika mikutano ya kimataifa, na amesaidia kufanikisha Umoja
wa nchi za Kiarabu.
Na miongoni mwa mafanikio yake maalumu kwa Misri ni Kutaifisha mfereji wa
Suez na kujenga bwawa la Al-Aliy la kuzalisha umeme na pia alifanya mabadiliko
katika kanuni ya marekebisho ya kilimo.
Ingawa Abbul Naser Alikufa tarehe 28-9-1970 lakini kumbukumbu
zake zitabaki milele katika nyoyo za Waarabu na pia Waafrika.