Mohamed Salah
Jumatano, Februari 06, 2019
Mohamed Salah

kuzaliwa kwake na maisha yake:

Mo. Salah amezaliwa tarehe 15 Juni, Mwaka 1992, Katika Kijiji cha Nigreek Mji wa Basion katika Mkoa wa Al-Gharbiya. Salah alianza kucheza katika klabu za Umoja wa Basion na Othmathon Tanta na hapo ni kabla ya kuingia kama mchezaji mdogo katika klabu ya Arab Contractors mwaka wa 2006. Mohamed Salah amecheza mechi yake ya kwanza dhidi ya klabu ya Mansoura katika ligi kuu ya kimisri  Tarehe 3 Mei, 2010 na wakati huu alikuwa na umri wa miaka kumi na nane. Uwezo wake, vipaji vyake vya juu na kasi yake yamechangia kumweka Salah katika mahali makini katika vyombo vya habari.

Alikuwa karibu achukuliwe na klabu ya Zamalik kabla yakujiunga klabu na Bazel ya Uswisi lakini  Mamdoh Abass rais wa klabu ya Zamalik kwa wakati huo alipinga uhamiaji wake akisema kwamba " Umri wake ni mdogo na hana uzoefu wake "

Mo. Salah alisaini mkataba na klabu ya Bazel ya Uswisi kwa miaka nne tarehe15 Juni, 2012
Na katika tarehe 26 Januari, 2014 klabu ya Chelsea ilitangaza uhamiaji wa Mohamed Salah.

Katika tarehe 3 Februari, mwaka 2015 Mo. Salah alihamia klabu ya Fiorentina  ya kiitalia kwa njia ya kuazimwa kwa muda wa miezi sita, na kwamba klabu ina haki ya kumsajili upya kwa msimu mwingine.


Katika tarehe 6  Agusti, 2015 Mohamed Salah aliingia klabu ya kiitalia Roma kwa njia ya kuazimwa  akikuja kutoka klabu ya Chelsea kwa muda wa mwaka moja, na kwamba klabu ya Roma  ina haki ya kumnunua katika siku za usoni  kwa gharama iliyofikia Euro Milioni 5. Na katika  mwisho wa msimu huu Mo. Salah alipata tuzo ya mchezaji wa msimu huko Roma, Na katika tarehe 3 Agusti, 2016 klabu ya Roma ilimnunua  Mo. Salah kutoka klabu ya Chelsea kwa gharama iliyofikia Euro  Milioni15.   

 
    
                  

Na katika tarehe 22 Juni, 2017 Mo. Salah aliingia klabu ya kiengereza  Liverpool  na Liverpool ilitangaza kusaini mkataba  wake na Mo. Salah, mkataba huu kwa  gharama iliyofikia Milioni Euro 42.

Mohamed Salah alichangia katika kufika kwa timu ya Misri mwisho wa kombe la mataifa ya Afrika 2017 Na kupatia nafasi ya pili, ambapo Mo. Salah alifunga mabao manne kutoka asili ya mabao matano yaliyosajiliwa kwa Timu ya Misri , na  Mo.  Salah alisajili mabao mawili mazuri sana katika timu ya Ghana.

na katika kombe la dunia 2018 Salah alisajili bao la kwanza la nchi yake katika mchuano mbele ya Urusi kutokana na pelanti, na katika mechi hiyo Mo. Salah na wenzake walishindwa kwa matokeo 3-1, Na kwa hivyo Salah anakuwa ni mchezaji  wa tatu wa kimisri aliye sajili mabao katika kombe la dunia.