Siti binti Saad
Jumamosi, Februari 15, 2020
Siti binti Saad

Siti binti Saad alizaliwa katika mwaka wa 1880, kijijini cha Fumba, kisiwa cha Unguja ambacho sasa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. katika mwaka wa 1911 alihamia Zanzibar mjini. Na hapo alianza kufanya kazi na wanamuziki, na akawa muimbaji maarufu wa muziki wa aina ya Taarabu, na aliendelea katika nyanja ya uimbaji wa Taarabu hadi uzeeni na aliaga dunia katika mwaka wa 1950.

Alikuwa na sauti nzuri sana inayowavuta wasikilizaji na nyimbo zake zilipendwa sana na watu kwani zinazungumzia maisha ya watu ya kila siku na matukio  halisia.

Binti Saad alitunga na kuimba nyimbo zaidi ya 250 na baadhi ya nyimbo zake zimebaki hadi leo. Na katika mwaka wa 2017, ulizinduliwa ufadhili wa mfuko wa Siti binti Saad, lengo lake ni kuhifadhi nyimbo zake na kukuza maadili na utamaduni wa Zanzibar.

Shaaban Robert ambaye ni Mshairi mashuhuri aliziita nyimbo za Siti binti Saad kuwa ni fahari ya Afrika Mashariki na pia aliandika wasifu wa “Siti binti Saad” uliochapishwa katika mwaka wa 1956 baada ya kifo chake.