Thomas N'Kono (kameroon)
Jumamosi, Juni 29, 2019
Thomas N'Kono (kameroon)

Nguli wa magolikipa.. Jina aliloitwa mchezaji wa kameroon  "Thomas N`kono", ambaye ni mmojawapo wa wachezaji bora zaidi ambao  walichukua nafasi hii katika bara la Afrika.                                                                                                   

Thomas N'Kono amezaliwa  Julai 20, 1956.                                   

Thomas N`kono alianza safari yake ya kimichezo katika ligi  za nchini kwake Cameroon  katikati ya miaka ya sabini katika timu za "Kanon Yaounde" (1974-1975) na Toner Yaounde (1975-1976) – timu hizo ni kubwa zaidi nchini Kameroon wakati huo - na ameweza kuongoza timu ya Toner Yaounde na kushinda  michuano ya   Afrika, Mabingwa wa Makombe 1975.

na aliihama timu ya Kanon Yaunde (1976-1982) na alichukua ubingwa  wa Afrika na timu hiyo mara mbili katika michuano ya kombe la Afrika: Mchuano wa Mabingwa wa Ligi mwaka 1978 na 1980 (Ligi ya Mabingwa ya Afrika kwa  sasa) na mchuano wa Mabingwa wa makombe mwaka  1979, kwa hivyo alichaguliwa na gazeti la "Francis Football" kama mchezaji bora zaidi barani Afrika kwa mwaka wa 1979 naye ni golikipa wa kwanza aliyechukua tuzo hii (Alishinda tuzo hii kwa mara ya pili katika mwaka wa 1982).

Alicheza na timu ya Taifa ya nchi yake Kamroon katika kombe la dunia mwaka wa 1982, na wakati huu Kameroon ilikuwa katika kundi gumu sana pamoja na Italia, Poland na Peru na lilifungwa goli moja tu na timu ya Taifa ya Italia, na hilo lilimrahisishia kujiunga kwake na timu ya Hispania "Espoaniol" nje ya kameroon.

N'kono alikuwa mchezaji muhimu sana katika mchuano wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1984 ambapo timu ya Kameroon ilishinda, na katika mchuano wa mwaka 1986 ambapo timu ya Kameroon ilishindwa mchuano huo kwa penanti na timu ya Misri.                                                                                                                                             
Thomas N'kono alikuwa mchezaji muhimu sana katika timu ya Espaniol  kwa misimu saba katika ligi ya Hispania (1982 - 1991), na aliweza kuongoza timu yake ya Espaniol katika msimu wa 87-88 kwa fainali ya Kombe la Umoja wa Ulaya mbele ya timu ya Bayar Liverkozn na katika fainali hii  kila timu ilishinda mabao matatu juu ya ardhi yake na Espaniol ilishindwa kwa penanti ingawa N`kono alidaka penanti ya kwanza lakini wachezaji wenzake walipoteza penanti tatu ambazo ziliondosha ndoto ya kupata Kombe la Umoja wa Ulaya.                                                
Baada ya timu ya"Espaniol" kushuka daraja la pili,  N`kono alicheza na baadhi ya timu za daraja la pili nchini Hispania na kisha alicheza miaka mitatu  katika timu ya "Bolivar Club"  hadi mwaka wa 1997 na alishinda ligi mara mbili na timu ya "Bolivar Club" na alistaafu kucheza mpira wa miguu baada ya kutimiza miaka arubaini na moja.