Tirunesh Dibaba
Jumanne, Aprili 16, 2019
Tirunesh Dibaba

Tirunesh Dibaba alizaliwa tarehe 1 Juni,1985 katika  Ersa, Jimbo la Uromia ametoka katika familia yenye watoto 6. Na alianza safari yake ya mbio wakati alipokuwa na umri wa miaka 14, kisha alihamia Mji mkuu Addis Ababa katika mwaka wa 2000.

Na alishinda mashindano kadhaa  ya dunia katika mbio huko Paris na Luzane 2003, Fukuoka 2006, Edinburgh 2008, Heilisnky 2005, na Osaka 2007.

Alishinda medali ya dhahabu ya mita 5,000 katika michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008,  na mita 10,000 katika mzunguko huo, kabla ya kushinda medali ya dhahabu ya mita 10,000 katika michezo ya Olimpiki ya London 2012.